Elly official
JF-Expert Member
- Sep 16, 2018
- 767
- 1,038
Kwema wakubwa aisee mamlaka ya maji tanzania inabidi ijitathmini sana. Huduma zao mbovu kupitiliza.
Hivi karibuni kuna mradi mkubwa sana wa maji umekamilika hap mkoani kwetu uliokula mabilioni mengi tu. Na tukaaminishwa kuwa sasa maji hakuna haja ya kuchemsha tena ni unakinga na kutumia tu. Kwa kawaida mimi huwa ni mhanga mkubwa wa uchafu utokanao na maji hivo lazima nichemshe.
Sasa juzi hapa maji yalikatika nyumbani kwangu siku ya kwanza nikajua wamekata tu, siku ya 2, ya 3 ikabidi nitafute fundi kufuatilia.
Katika kufuatilia akasema shida ipo kwenye mita imeziba, maana kabla ya mita kuna jirani yangu ametap maji kwenye bomba langu na kwake yanatoka kama kawaida.
Japo ni najua ni makosa nikamwambia fungua mita tuangalie. Kufungua hivi nakutana na chura amefika kwenye mita ameingiza kichwa kikaziba maji yanapopita. Nlisikitika na kuonea kinyaa maji yanayosukumwa na hii mamlaka ya mkoani kwangu.
Hawa watu hawapo makini na afya za walaji. Hebu fikiria ni vyura wangapi wamo kwenye mambomba tunakunywa mizoga ya vyura, mavi na kila ghasia