Nimekuomba twende outing, unachagua Kempisk hivi una nia na mimi kweli?

bobby dolat

Senior Member
May 18, 2015
167
263
Wadau,

Nina bahati mbaya sana, huenda niache mchepuko nitulie tu sasa maana sijatulia vizuri kutokana na ule mkasa wa pink panther wa Jf, weekend iliyokwisha nilimuomba binti wa IFM outing, hatujawah ikutoka date tangu tulipobadilishana namba zetu siku alipokuja kufuatilia pesa za mkopo kazini kwangu, Ijumaa nikamkumbushia suala hilo na kumpa uhuru wa kuchagua pa kwenda. Jumamosi mida ya saa moja jioni mtoto akaniambia nimpitie hapo chuoni.

Nilipofika nilimkuta amewiva hasa na vazi lililoonekana kuwa la gharama kubwa na manukato yenye harufu sana. Nikamuuliza amechagua twende wapi? Akaniambia kwa kujiamini kabisa twende tu nitakuonesha tukifika nashangaa anavyozidi kunielekeza ni kuelekea Hotel ya Kempisk (jina jipya sijalishika vizuri).

Mara ananielekeza kuingia kwenye Geti la hotel hiyo kwa kweli nilishtuka ila nikajikaza tu kisabuni maana mfukoni nilikua na shs 80,000 ambazo niliamini kwa viwanja nilivyozoea mimi Ie Rose garden, Hongera bar, au kwenye nguruwe ingetosha, akaniambia huko juu kuna kiwanja kinaitwa level 8 tupande tukapanda, kulikua na bendi ya wa Mexico ikitumbuiza huku watu wakiendelea na mazungumzo yao.

Akaja muhudumu na vitabu flani viwili viliahinisha vyakula, vinywaji na bei zake, ndipo nikahisi kama tumbo la kuhara linakuja kwa mbali na kurudi huku nikisweti pamoja na AC iliyokuwepo, kila chakula kilionekana kuanzia 45,000 na kuendelea yaani main course. Binti akaagiza pombe moja hivi ila sio bia walikuja kummiminia kwenye glass ndogo, kila wakimimina ni 15,000 kaletewa zaidi ya tano mimi niliagiza castle lite. Kwa vyovyote vile hadi hapo nilijua nahitaji rescue mission maana hadi hapo kwa hesabu za haraka ilishavuka hela niliyokua nayo, alishaagiza T-bone steak + chipsi na starter ya fish finger ambayo aliletewa kabla ya chakula (main course)3.

Nikaenda chooni kumpigia staff mwenzangu aliyekua anakunywa Meeda Bar Sinza kwamba kama hakufika in person Kempiski ndani ya lisaa limoja basi mwenzie naadhirika. Tulibishana sana kwenye simu kutokana na kuwa amelewa jamaa kaja saa tano kasoro usiku akiwa hoi kwa pombe akajiunga nasi na kumwambia binti kwamba ""huyu jamaa tunakunywa nae Meeda kila siku nashindwa kuelewa kafuata nini huku leo "" Akanigeukia mimi na kusema ""we ---- mi sina hiyo laki tatu unayotaka nina laki mbili tu naenda kula na mke wangu nyumbani.

Nilitaka kuinuka kumpiga ngumi ila nika refrain, Jamaa akaendelea kuniponda kwamba naleta mwanamke pale wakati sina hela, mwanamke akainuka na kuchukua mkoba wake na kutuaga bila hata kumruhusu aondoke na hakupokea simu yangu hadi Leo kwa mbinde sana tulichangishana na kuilipa bili hiyo shs 291,000 bila mimi kubaki hata na senti moja na sikula. Yote tisa, kumi mhudumu ambae alikua na roho ya utu sana baada ya kuona binti kakimbia akatueleza kuwa huwa anakuja hapo na jamaa zake kwa nyakati tofauti wenye kuwa nazo.

Binti wa chuo anawezaje kunipeleka Kempisk bila kujua status yangu? Binti wa chuo anaonekana kwenda level eight Mara kwa Mara na jamaa flani ni nani zake kumbe ni kahaba? Mabinti mnakuaje lakini? Au mnadhani zile hela tunazohesabu pale benki ni zetu? Wengine sisi ni makarani tu, mtuonee huruma mama zetu, ukinikuta pale benki huwa na deal na hela za wengine sio zangu kale ka Gari ulikokaona ni ka mkopo bado nadaiwa. Au nilifanya makosa kukwambia ukweli kuwa nimeoa? Ndo ukaamua unikomoe?

Sio vizuri kwa kweli
 
Utaendelea kuchunwa kwasbb akili huna Ulishindwaje kumwambia mkakae sehemu nyingine?,,. Leo umempata mtu wa kukusaidia cku nyingine utaliwa Jicho kwa kupenda sifa za kijinga pambaaf
 
Hahahaaaaa, pole sana mkuu. Lakini umeacha mke nyumbani, kwa nini ulikubali kwenda huko kwa wenye nazo?
Mshukuru sana jamaa ako, ila pia hilo ni fundisho, stop cheating kwa wadada wakufikia tu usiojua status zao.
 
dah..kumbe ni wewe jamaa tuliyeonana cku ile kempisk mi nilikaa karibu yenu nilivaa T-shirt nyekundu na kofia nyeusi...nilikuona mnavyobishana na jamaa yako na kisha demu kuondoka.
Huyo demu anaitwa Prisca japo hupenda kudanganya majina...mi nshapigaga cku nyingi ndo maana cku hiyo alivyoniona nimekaa na kifaa kingine cha chuoni kwao kila mara aligeuka na kunikata jicho..!
mi nshatafunaga wengi tu ila wanapenda vitu vya bei.
 
Haha hii ni kali. Ila kama ulimpa nafasi ya kuchagua pa kwenda na hukukataa hata mlipofika then hakuna haja ya kulalamika bro.

Na mtu ushamwambia una mke tayari, halafu unataka awe na nia na wewe...are you kidding me right now?
 
bobby dolat

Hahahahhahahh....duuuh!!!!!!!!!
Pole kwa yaliyo kukuta.
Ahhahahahaahhaaahahaahahahaa
 
Last edited by a moderator:
dah..kumbe ni wewe jamaa tuliyeonana cku ile kempisk mi nilikaa karibu yenu nilivaa T-shirt nyekundu na kofia nyeusi...nilikuona mnavyobishana na jamaa yako na kisha demu kuondoka.
Huyo demu anaitwa Prisca japo hupenda kudanganya majina...mi nshapigaga cku nyingi ndo maana cku hiyo alivyoniona nimekaa na kifaa kingine cha chuoni kwao kila mara aligeuka na kunikata jicho..!
mi nshatafunaga wengi tu ila wanapenda vitu vya bei.

Daaaah hiii sasa hatari tupu...
 
Hahahaha Levels baby levels, mtuliage nyumbani na wake zenu, hapo mkeo akiomba kuku wa Merry Brown tu haletewi alafu kwa ridhaa yako na akili yako timamu ukaingiza gari gate ya Hyatt salale hasara kabisa kuwa na mume kama wewe
 
tatizo watu hamuangaliii movie na kusoma matukio ya wenzio ungejua escaping plan. ungeweza fanya yafutayo.
1.Zimia kabisa shut down system yako ya mwili kana kwamba umepigwa konde na MAYWEATHER. Fikiria hapo kuhaibika ukijisemea moyoni nikiamka tu hapa napotea.

2. Itabidi uanze kuta waskaji mapolisi au wajanja ambae ukimpa situation atakupa escaping plan. yule unamwita akikukuta anajifanya ni hasimu wako wa siku nyingi mnachanpan kidgo bila kuvunja vitu ukipelekwa police mnatoa 50 mnaachiwa, hapo umesave pesa ingine.
3.Ukishndwa hayo heuka HUSSEIN BOLT, toka nduki mkuuu. aliye juu level 8, mngoje chini kwenye parking
 
Pole ndo tunajifunza hivo kupitia mikasa ya maisha pengine Mungu kakusave na tatizo kubwa kuliko thamani ya hiyo 291000
 
Back
Top Bottom