Nimekukumbuka Spika wangu Mh. Sita

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
Kwa uchungu namlilia spika wangu makini, mzee wa speed na viwango. Yaani nikiangalia hawa vilaza waliobaki naona kama vile wanatafuta umaarufu kupitia mgongo wa Bunge. Kiti kimechuja, kimepwaya,hakina mashiko, chabaridi, kwa mbaaali naona kina rangi ya kijani, nikasema labda kwa kuwa spika ni mwanamke, basi ngoja tumuone naibu spika labda atakuwa ngangari. Heee! kumbe ni kopo na mfuniko, sioni kabisa mwanga wa matumaini. Yaani ndo kweli anahitaji maombi ili mindset yake ibadilike. Jamani labda tuwe tunaazima spika nchi yoyote ya karibu atufutie hii aibu yetu.
 
Back
Top Bottom