Nimekuja kwenu kuomba ushauri

Uncle nlivo ona hata huyo mkeo hakufai make majibu anayo kupa hayaridhishi hata kidogo!!, lamsingi fungeni safari kama mwanzo nenda uwaambie kiasi hicho huna wala kukipata ni issue wao wataamua lakufanya! tena usizidishe laki 3!!..
 
Yaani ningekua wewe,namrudishaje hapo nyumbani nakuwa namtumia fedha za matumizi namwambia bado nafikiria kama nitamwoa au la!
Kwa kukusaidia mkuu, embu mrudishe kwao halafu usimwambie kama mmeachana uone Mambo yatakavyokuwa ila mbona mahari inapangwa kienyeji enyeji hivyo? Hawa hawajui maisha eeh?
 
4mill?kwa mahali tu!acha ujinga au anatoa madini hyo demu?ana uzuri gani;nenda katoe laki mbili tu kaka;mil hyo biashara?
 
Mahali siyo lazima ulipe yote kwa wakati mmoja! Wapoze na laki 5 weka kitu ndani then nitolee hiyo mpaka kifo. Yaani uwape 4M na still bado tu wataendelea kukupiga mizinga ukishaoa huyo mwanao.
 
mwambie umepata wa mahari ya laki 4,,,,,end of story......
 
kweli 4m mahari? wazee wengine bana kujidharaulisha tu..we tafuta mzee mtu mzima ikibidi wawili waambie mahari mwisho laki 5 ndio uwezo wako..kama hawataki basi wamchukue binti yao na wakuachie watoto wako..uone kama watasubutu..khaa wazazi wengine nuksi kweli
sisi nyumbani kwetu mahari anataja mtoto wa kike mwenyewe mahari yake na anapewa mwenyewe muolewaji na wala mzazi hachukui senti, binti akiamua ndio anampa/anawagawia wazazi kidogo lkn sio lazima.. wazazi wao wanapewa sijui blangeti, shuka, jembe n.k ambayo hata haifiki elf 40
 
4m hiyo mkomoeni wape laki 5 kaka zaidi ya hapo akupe risiti yenye VAT muulize huyo mkwe yeye alitoa sh gapi pengine anadaiwa anataka umlipie du! Hatari sana au ndio umeme umepanda
 

Mkeo ni mtu kutoka mkoa gani?
 

Mia mia
 
Huyo mkweo asikuchoshe

Kwanza mahari sio lazima iishe

Halafu milioni 4 anatafuta mtaji

Wagonge laki tano waambie nyengine mtamalizia then kaandikisheni mfunge ndoa

Wazazi wengine wanadhani shoda zao ItamaliWa na mahari???
 
Dah, sipati picha, ingekuwa mimi ningefanya kituko cha mwaka. Anyway, tunatofautiana, mimi nilitoa 150,000/= tena miezi sita baada ya ndoa. Siku nimeenda kujitambulisha, cha kwanza walisema vijana wamependana wakafunge ndoa, hayo mengine baadaye.

Siku hizi watu wanatafuta kuolewa, huyo naona anatafuta kuachika
 
Wanataka kukugeuzaa mtaji,kwan mahali nyingi inasaidia nin mahusiano yenu
Wewe cha kufanya piga kimyaa mpaka wanyookee
 
Dadangu alienda kutambulisha mchumba, na ukoo ukampangia mahari kubwa sana, kijana akawa mkali , na kususa ,kesho yake asubuhi sana wazzee walienda kumgongea wakimwomba asibadili uamuzi wake, na mahari waliyokuja kuipokea haikufika hata robo ya ile waliokua wanaitamani. Jaribu njia hii inaweza kukusaidia, sometimes wazee wetu wanakuaga na tamaa sana pasibokujua uwezo wa mtu, wakishajua kijana ana kazi na kagari kamoja bassss watakuliza kwenye mahari. Ila ukiona mkeo anakua upande wa wazee wake ujue hilo ni tatizo, anatakiwa awe upande wako maana yeye ndio anajua uwezo wako.
 
wote ni wanyakyusa wa mbeya ingawa yeye baba yake ni wa tukuyu na mama yake ni wa dodoma na yeye kakulia dodoma na mimi ni wa kyela

Kwa wanyakyusa mashangazi ndio wanaletaga ujinga. Tena usiombe wawe maskini, watataka kutajirika kupitia kwako. Waambie wakupe mchanganuo wa hiyo mahali uone wamepanga nini. Na njia rahisi ni kutoa vitu vya muhimu tu! Mfano mkaja wa mama, blanketi, majembe, mashuka, mbuzi wa mjomba, mbuzi wa shangazi. Hivyo vingine unawaambia najipanga ntakuja kuleta na ndio mwisho wa mchezo. Wala hata wasikuumize kichwa
 
Wakati mwingine hizi mira zetu za Kiafrika zinaturudisha nyuma sana. Baba kashaona mtaji huo! We kauka endelea kula vitu, mama akitaka kuleta za kuleta unamwambia utaacha watoto hapa umfuate baba yako. Hapa mzazi inabidi awe mpole tu mwanae kashatoa utamu na thamani imeshapungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…