Nimekubali yaishe, nimeukubali unjano wa nywele zangu

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Hali?

Niliketa uzi humu siku chache zilizopita kuhusiana na tiba ya nywele nyekundu/njano na nashukuru wengi walijitoa kunishauri kwa uchanya.

Baada ya kuwaza na kutafakari sana, ikiwa ni pamoja na kukumbuka maisha yangu tangu utoto mpaka umri huu wa utu uzima, nimeazimia kwa nia moja kuungana na memba fulani(nimeisahau id).

Nimeamua kuacha kuhangaika kutafuta dawa, nimejikubali na sijanyoa wala kupaka piko na kufanya waving kwa nywele zangu since then...

Zimekuwa kubwa nazihudumia, ni safi ila tu ni nyekundu. Namuonea aibu nani?
Nimevunja sheria? Kazi ya nywele kichwani ni ipi? Ni ya kutafuta ujiko kutoka kwa wanawake au ya kulinda kichwa dhidi ya mionzi ya jua?

Mkiona mtu ana nywele nyekundu anashuka kwenye gari aina ya ..., basi jueni 90+% kuwa ni mimi, najua nimetoa code somehow

Wa kunikataa anikatae hivi hivi nilivyo, wa kunikubali anikubali hivi hivi nilivyo. Nimeaga rasmi kutoka kwenye kuwa mtumwa wa jinsia fulani.

Sinyoi, na nikinyoa basi sababu si rangi, bali nimeamua tu.

Shukrani sana kwa wote!

NB: Nimewapata wawili mpaka sasa(mmoja anaishi Masaki mwingine Sea Breeze apartments, Mbezi Beach!

Wananipenda nilivyo, though hawafahamiani... ila nimewala wote simultaneously!

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
 
Nywele zisizo na matunzo utazijua, na usishevu ety kisa you don't care how watching you 🤣🤣🤣😂

Sema tu sina pesa ya kwenda babashop
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom