Nimekipata Kigori,wenye wivu jinyongeni,

mhh ukatulie ndoani usimletee mtoto wa watu mabalaa na haya mashairi yaendelee hivi hivi hata miaka kumi mbele. hapo kwa wasukuma ndio penyewe upole upo, unyenyekevu upo, ukarimu ndio penyewe, heshima kwa nduguzo na wazazi tele.hongera mungu akujalie
Sifa nampa muumba,aliemuumba kigori,
kamwe kwake sitoyumba,kama wana wa misri,
hata akina liyumba,kigori kwake makafri,
Mwaliko ukiupata,waambie na wengine,

sikutaka kuwaleti,chini wazazi wangu,
chini nao niliketi,kuhusu kigori changu,
mamangu alinileti,nijue maisha yangu,
Mwaliko ukiupata,waambie na wengine,

tabiaye sio kama,yule wa profu jei,
togwa taka boga mama,faidisha pedejei,
twanga pepeta mama,mwanamasanja jjei,
Ukiupata mwaliko,waambie na wengine,
 
Daahhh
hii kali mkuu
kwa kweli nimeipenda
duuhh kipaji mnacho .. namzidi kuongezewa..

Nipo safarini naelekea kunani pale haya mambo yetu sisi watu wa pwani Naenda kusalimia ndugu sio ukweni, naenda kwa furaha na sio matangani Namuona Ilahi anireshe salama, mji wetu mtoni mtongani. Jamani nipo safarini nitawashushia vina nikirusi salama
 
mmmhh nime kukubali..
 
mmmhh dear..
hiii inaonekana ni ya mwalimu kabisa..
hahahhaha lol

na mie nauhakika ni kipaji hicho..

Dadangu Afrodenzi, wanipa furaha yakini,
Heri ingekuwa benzi, kwake ndipo akilini,
Kwa hayo ulonienzi, umefuliza nafsini,
Asante umenijuza, kuwa ni changu kipaji

Jambo usilolijua, hilo li sawa na kiza,
Rafiki nayekujuza, huyo zaidi ya piza,
Ndiye anayekukweza, wengine waje kutuza,
Asante umenijuza, kuwa ni changu kipaji

Umeniita mwalimu, japo sijui mtala,
Waona hiyo elimu, kwa hii fupi makala,
Sasa umetia hamu, ubongo katu kulala,
Asante umenijuza, kuwa ni changu kipaji

Huyo nguli akijua, ndimi wake mshindani,
hakika hatadengua, kuleta vyote vidani,
la sivyo atajichua, japo yu kwake chumbani

sasa nimekosa la kusema ...

I hope thank you is good enough ..
Je umefikiria kuandika kitabu cha poem..??
maaana watu kama sisi tutavinunua kwa wingi
especially kama ni Swahili language
 
Loh, Safi sana kwa hizi tenzi. Kipaji maalum hicho.

Kila mtu ayaweza,hata wewe mwana mpevu,
hata sungura kilaza,kutamani zile mbivu,
kwa sauti alipaza,akionyesha kwa wivu,
hii kamwe si kifani,mdundiko ngoma yetu,

njo muone mwanawane,msukuma mejilaza,
pitia hata saa nane,kisiwa kilicho mwanza,
chesa na manemane,katu kutomliwaza,
hii kamwe si kifani,mdundiko ngoma yetu,

njo utoe lako dua, kamwe lisilo la kuku,
piga bandika bandua,daima mambo iko huku,
rangi yake mulua,yalabi sio mamburuku,
hii kamwe si kifani,mdundiko ngoma yetu,
 
Si utani hii kitu imetulia. Hongera sana. Hivi utunzi wa mashairi ni kipaji mtu anazaliwa nacho au naweza kujifunza na nikaweza?

utunzi sio siasa,ya makamba na kikwete,
wanadhani kama anasa,linganisha na obote,
kwa majungu wamenasa,wameshiba kwa ubwete,
Mungu daima kakupa,kipaji wewe unacho,

Kumi moja yetu sita,udini wauhubiri,
bungeni wamemsuta,eti wamuita kafiri,
ni muono wake sita,sisiemu kwa sifuri,
Mungu daima kakupa,kipaji wewe unacho,

kamwe usije kudata,siasa penzi mfita,
mshumbuzi wamemhata,maji miksi mafuta,
Arusha aliko mahita,za moto zilitupita,
Mungu daima kakupa,kipaji wewe unacho,

Ngoja rudi kwenye mada,ya mapenzi dadavua,
siasa sina shahada,slaa kashusha mvua,
eti ana wa makinda,sisiemu kumuezua,
Mungu kakupa kipaji,daima wewe unacho,
 
Magulumangu nakupongeza
Kigori wewe kumpata
Najua mimi ulikopita
Wivu mi ninao,kujinyonga sijinyongi!!

Kila la kheri nakutakia
Furaha katika ndoa
Watoto nao kupata
Wivu mi ninao kujinyonga sijinyongi

Changamoto kwenye ndoa
Ni sehemu ya maisha
Uvumulivu uwe nao pia
Wivu mi ninao kujinyonga sijinyongi

Michele wake Obama,heshima daima kwako,
Fisiti ledi wetu mama,marekani si bamako,
Kamwe wewe chetu kisima,simpi heko Saluma,
Sema mama tena sema,yesi we kani do sema,

Kigori fuatilia, siasa kwake si kiduchu,
mapenzi namlilia,nikionyesha kwa uchu,
nguo nitamfulia,nikimwona sio mchu,
Sema mama tena sema,yesi we kani do sema,

Kalindima kama soweto,wakidai wao uhuru,
sio chama cha mseto,alitaka penzi lilo huru,
hakuingia kwa gheto,kama walio ma guru,
Sema mama tena sema,yesi we kani do sema,

la moyo wangu azizi,sasa amejilaza,
kutungua sio wizi,namiliki si kilaza,
kibo uhuru na mawenzi,kilele sauti paza,
sema mama tena sema,yesi we kani do sema,
 
dada Afrodenzi, asante kwa kunisoma,
nashukuru kwa kunienzi, vilevile kunipima,
japo sitoshi konzi, hukuninyima alama
asante kwayo mapenzi, yadumu enzi na enzi

yule mtoa posa, alikuja na mizani,
akatujuza mkasa, aloufumba vinani,
akakifunga kitasa, cha shairi tusighani
asante kwayo mapenzi, yadumu enzi na enzi

Mwenyezi katukirimu, shairi kulithubutu,
japo sinayo elimu, nimeushinda ubutu,
pamoja naye hirimu, sijekuwa mtukutu
asante kwayo mapenzi, yadumu enzi na enzi

bwa harusi ndiye nguli, wa mashairi na vibonzo,
mie kama kibakuli, yeye kwangu kisonzo,
mengi yake maakuli, ya kale kama maganzo,
asante kwayo mapenzi, yadumu enzi na enzi

nimeyatoa mahari,mila zetu kudumisha,
sikutaka iwe shari,roho yangu kimerusha,
yeye alikuwa mwari,kijijini yake maisha,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

Sio lake mentali,walomwimba kina necha,
wala sio geti kali,judi wewe kama ticha,
mapenzi sio kibakuli,na hii isiwe ticha,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

thelathini zetu ngombe,kwa heshima zimeenda,
msijetaja yule zombe,hapa na isiwe mada,
bakuli hata vikombe,masheto kwake ziada,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

mihogo maji yeye hula,msifananishe nyani,
chipisi ni kwa muhula,wasije sema mtaani,
kafundwa nasema hula,wengi walimtamani,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

sipo kumlinganisha,na malaika wa mbunguni,
tabia naainisha,tipu topu kileleni,
kama wataka kubisha,kunako maliwatoni,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

Alipo mie ndo nipo,kama si rohoni mwake,
bahari kunako upepo,twaitwa mume na mke,
kanipenda bila malipo,japo roho suuzike,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,
 
mhh ukatulie ndoani usimletee mtoto wa watu mabalaa na haya mashairi yaendelee hivi hivi hata miaka kumi mbele. hapo kwa wasukuma ndio penyewe upole upo, unyenyekevu upo, ukarimu ndio penyewe, heshima kwa nduguzo na wazazi tele.hongera mungu akujalie

miaka kumi ni kiduchu,kwangu yeye ndo kikomo,
kila siku kwake nina uchu,limee kama killimo,
uchakachuaji sio ishu,vicheche sina kipimo,
sukuma nimedondoka, acha msininyanyue,

Mpole kama shubira, heshima jina la pili,
vicheche sina mpira,ona kama pilipili,
moyoni kama manira,msela sichezi mbali,
sukuma nimedondoka,acha msininyanyue,

Mie sio mfisadi,mapenzi hata siasa,
natoa zote ahadi,japo sio wa malisa,
natekeleza zote jadi,napa mbali kama nasa,
sukuma nimedondoka,acha msininyanyue,

Pongezi nyingi kwa mama,ndie aloona chungwa,
ingawa yote ni kiama,kupenda kusiko igwa,
ilinino ije tema,ya mapenzi kama pegwa,
sukuma nimedondoka,acha msininyanyue,
 
Wakuu mko safi sana. Big up to ya self. Ushairi unahitaji akili iliyo shapu kufikiri na ndio maana wachache sana wamebarikiwa pande hizi. Nime enjoy sana kila mstari wa mashairi yenu.
 
Wakuu mko safi sana. Big up to ya self. Ushairi unahitaji akili iliyo shapu kufikiri na ndio maana wachache sana wamebarikiwa pande hizi. Nime enjoy sana kila mstari wa mashairi yenu.

wangu nguli wa jabali,kitambo umenisuta,
kadi uliikubali,kwa harusi hukusuta,
alipokuona mwali,busu tama hukusuta,
Salamu zako pokea,toka kwakekigori,

Kasema nikupe hai,japo tu kukusabahi,
Kilimanjaro pitia,uje kwetu asubuhi,
jina lake malkia,si uingereza walahi,
Salamu zako pokea,toka kwake kigori,

ananiita kinywani,mate ni haki yake,
tunaishia kitandani,kuenzi mapenzi yake,
kunako sio maskini,kajaaliwa mana ake,
Pokea zako pokea,toka kwake kigori,
 
nimeyatoa mahari,mila zetu kudumisha,
sikutaka iwe shari,roho yangu kimerusha,
yeye alikuwa mwari,kijijini yake maisha,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

Sio lake mentali,walomwimba kina necha,
wala sio geti kali,judi wewe kama ticha,
mapenzi sio kibakuli,na hii isiwe ticha,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

thelathini zetu ngombe,kwa heshima zimeenda,
msijetaja yule zombe,hapa na isiwe mada,
bakuli hata vikombe,masheto kwake ziada,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

mihogo maji yeye hula,msifananishe nyani,
chipisi ni kwa muhula,wasije sema mtaani,
kafundwa nasema hula,wengi walimtamani,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

sipo kumlinganisha,na malaika wa mbunguni,
tabia naainisha,tipu topu kileleni,
kama wataka kubisha,kunako maliwatoni,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

Alipo mie ndo nipo,kama si rohoni mwake,
bahari kunako upepo,twaitwa mume na mke,
kanipenda bila malipo,japo roho suuzike,
Nimempenda mwenyewe,japo mama kachagua,

Mbona waukimbilia, uzi wala si wako,
mwenyewe katulia, wewe waanza vituko,
ama umefulia, tukupe japo ukoko
huba na wako kigori, huwezi jaza kibaba

Hima sasa urudie, uzi ulio wakwako,
Afrodenzi atulie, kwani yeye si wako,
na majibu ututajie, ya hayo yaliyo yako
huba na wako kigori, huwezi jaza kibaba

Waghani umenasa, jinasua hutotaka,
hata kama ni tasa, mitala huwezi taka,
huachi vyako visa kwa kuwa umeishadata,
huba na wako kigori, huwezi jaza kibaba

Mapenzi kweli matamu, ila kunasa laumu,
waweza tokwa fahamu, kujinasua muhimu,
kama haiishi hamu, hiyo ndiyo ze utamu
huba na wako kigori, huwezi jaza kibaba
 
Originally Posted by Miss Judith
Dadangu Afrodenzi, wanipa furaha yakini,
Heri ingekuwa benzi, kwake ndipo akilini,
Kwa hayo ulonienzi, umefuliza nafsini,
Asante umenijuza, kuwa ni changu kipaji

Jambo usilolijua, hilo li sawa na kiza,
Rafiki nayekujuza, huyo zaidi ya piza,
Ndiye anayekukweza, wengine waje kutuza,
Asante umenijuza, kuwa ni changu kipaji

Umeniita mwalimu, japo sijui mtala,
Waona hiyo elimu, kwa hii fupi makala,
Sasa umetia hamu, ubongo katu kulala,
Asante umenijuza, kuwa ni changu kipaji

Huyo nguli akijua, ndimi wake mshindani,
hakika hatadengua, kuleta vyote vidani,
la sivyo atajichua, japo yu kwake chumbani
Asante umenijuza, kuwa ni changu kipaji

sasa nimekosa la kusema ...

I hope thank you is good enough ..
Je umefikiria kuandika kitabu cha poem..??
maaana watu kama sisi tutavinunua kwa wingi
especially kama ni Swahili language

Karibu tena wewe mama, wa kiroho nakuaminia,
natamani uje boma,uone livyo malkia,
lake jina kiama,futa kote rumania,
Asante wako mchango,wa harusi niliupata,

Kigori kakusabahi,kwa wako ule ushauri,
wa maana ulimsihi,kamwe asije kiburi,
unaondoka subuhi,ulimpa tafakuri,
Asante wako mchango,wa harusi niliupata,

lipi kalisema masa, nilo wetu mchungaji,
tusizipende anasa,hotuba yake mchungaji,
mpitishie na Rosa,mwambie aje kwetu ujiji,
Asante wako mchango,wa harusi niliupata,

Afrodenzi dada asante,pia hukuwa nyuma,
kigori dada kaka wote,salamu wametuma,
wanajamvi sio wote,walokuja kwetu yama,
Asante wako mchango,wa harusi niliupata,
 
Mbona waukimbilia, uzi wala si wako,
mwenyewe katulia, wewe waanza vituko,
ama umefulia, tukupe japo ukoko
huba na wako kigori, huwezi jaza kibaba

Hima sasa urudie, uzi ulio wakwako,
Afrodenzi atulie, kwani yeye si wako,
na majibu ututajie, ya hayo yaliyo yako
huba na wako kigori, huwezi jaza kibaba

Waghani umenasa, jinasua hutotaka,
hata kama ni tasa, mitala huwezi taka,
huachi vyako visa kwa kuwa umeishadata,
huba na wako kigori, huwezi jaza kibaba

Mapenzi kweli matamu, ila kunasa laumu,
waweza tokwa fahamu, kujinasua muhimu,
kama haiishi hamu, hiyo ndiyo ze utamu
huba na wako kigori, huwezi jaza kibaba

Mapenzi kwenye vituko,ni mahali yake dia,
Unyuzi wake mfuko,ni mwangu umetulia,
sihitaji ukoko hata kama nimefulia,
Mapenzini mwake kwangu,sabuni ya roho yangu,

Kunasa nilitaka,sema muda ulibana,
Talaka sitoitaka,itoke japo nitabana,
matatizo kutatika,ikija tokea runa,
Mapenzini mwake kwangu,sabuni ya roho yangu,

Afrodenzi kuwadi,wangu toka za enzi,
alimpa mazawadi,kigori wangu kipenzi,
tulia wewe judi,fisadi sio fdenzi,
Mapenzini mwake kwangu,sabuni ya roho yangu,

pakajimmy alikuja,mweusi paka ye pia,
melo pia alifuja,siri jamvini fichia,
zanziba hata unguja,wageni kwa malkia,
Mapenzini mwake kwangu,sabuni ya roho yangu,

Ngoja niachie hapa,isije kuwa tabu,
kamwe wengi waliapa,sitompata mahabibu,
masanilo nipe chapa,nisije pata hathibu,
Mapenzini mwake kwangu,sabuni ya roho yangu,
 
Magulumangu kama uko single na Miss J yuko single kaaeni chini myamalize kiutu uzima. Na pledge 20 kwa harusi. Naona zina click kinoma.
 
Magulumangu kama uko single na Miss J yuko single kaaeni chini myamalize kiutu uzima. Na pledge 20 kwa harusi. Naona zina click kinoma.

Si utani NJ, hawa wawili wata make a wonderful couple ha ha haaaa.. :car:
 
mkuu umenikumbushia enzi za malenga wetu.. saa saba natoka shule nafikiria ugali mchicha tu

hongera kwa kumpata
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom