Nimekipata Kigori,wenye wivu jinyongeni, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimekipata Kigori,wenye wivu jinyongeni,

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Magulumangu, Jan 22, 2011.

 1. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hayawi yawi jamani,mwenzenu nimeopoa,
  Ndoto ile singizini,kamwe sijapata doa,
  Kipenzi wangu mwandani,ya maisha pingu ndoa,
  Nimekipata Kigori,Wenye wivu jinyongeni,

  Upepo wa baharini,mawimbi kutuimbia,
  ufukweni kigamboni,ndiko tulikotulia,
  Hii ni hanemooni,kithungu sikilizia,
  Nimekipata kigori, wenye wivu jinyongeni,

  Sitaki ushakudaku,mwenyewe natoa onyo,
  Shuga mami marufuku,utulie wangu moyo,
  Toa yangu dukuduku,asali wangu wa moyo,
  Nimekipata kigori,wenye wivu jinyongeni,

  Umbo lake namba nane,kipotabo nasifia,
  Kama kizazi cha nne,watengenezaji nokia,
  Kiamshe wa manane,uzuri sio fifia,
  Nimekipata kigori,wenye wivu jinyongeni,

  Brand nimefungua,bado kuchakachuliwa,
  Fyuzi hazijaungua,kitu tight muruwa,
  Msukuma si mzigua,pongezi kwako mtawa,
  Nimekipata Kigori,wenye wivu jinyongeni,

  Hata da yetu Saida,kisha toa hili onyo,
  Usije jiita akida,kuja kuonja nyonyo,
  Kwa panga bila shida,nitaja kutoa moyo,
  Nimekipata kigori,wenye wivu jinyongeni,

  Mwisho naishilia,mwanzo wangu kumpenda,
  Ishara naashilia,mapenzi chati kupanda,
  Roho kaishikilia,sitaki tena kimada,
  NIPE MAMA NIPE,TUFAIDI PENZI LETU.
   
 2. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,838
  Likes Received: 1,999
  Trophy Points: 280
  asante kwa ushairi
   
 3. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  duuuuuuuhhh
  kumbe hata kwenye hii idara umekamilika hahaha lol
  :amen::amen:
   
 4. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  MAlenga wetu asante sana vina vimetulia
   
 5. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wengi walinisuta,wakidhania mi sifai,
  Wangu ameniita,penzi langu bado hai,
  Jina sio Mwamvita,hajatokea kandahai,
  Mungu kanionyeshea,lililo penzi la kweli,

  Kwenye yake macho lipo,penzi la kweli jamani,
  Sio yule ndege popo,Mwanakijiji porini,
  Mawimbi hata upepo,nywele zake nyumani,
  Mungu kanionyeshea,lilipo penzi la kweli,

  mafataki walijaribu, mafisadi kuchakachua,
  lulu wamemharibu,wangu kawaumbua,
  hata wetu nyani ngabu,dhahiri anatambua,
  Mungu kanionyeshea,lilipo penzi la kweli,

  Afrodenzi nakualika, masanilo naye mokoyo,
  Rose lete gharika,judi mama wa kimoyo,
  msije kuferudhika,mumuonapo wa moyo,
  Mungu kanionyeshea,lilipo penzi la kweli,

  Sio ki hivi hivi, magoti niliyapiga,
  wazee hata wa mvi,salani walizipiga,
  kafundwa sio kwa muvi,kina mama wameaga,
  mungu kanionyeshea,lilipo penzi la kweli,
   
 6. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280

  Kwa kweli umebarikiwa Magulumangu wangu...
  mmhhh shahiri tamu hilo..

  mie itanichukua wiki kuandika shairi moja wewe umeandika
  2 ndani ya nusu saaa..
  ama kweli umebarikiwa..

  halafu una maneno maataamuu saana..
  mmhh utaniingiza pabaya/pazuri hahahh lol
  mwaliko nimesha upokea na kwao nimeshafika lol
   
 7. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  kigori mzee wa kweli,desidii nakwambia,
  si mtoto wa Kimweli,chapa ya ng'ombe sikia,
  huwezi hata tabili,ugali akikupikia,
  Walisema haliwiki,jogoo la shamba mjini,

  Jogoo la shamba mjini,lisema halitawika,
  uzuri kisiginoni,ile mbaya kafunika,
  kwa tabia shukrani,mfano wake ni nyika,
  Walisema haliwiki,jogoo la shamba mjini,

  kawambia watajiju,mashambenga mashangingi,
  walidhani kama mwaju,hatishiki na shilingi,
  ndimu hata maukwaju,chipisi mayai tungi,
  Walisema haliwiki,jogoo la shamba mjini,
   
 8. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sifa nampa muumba,aliemuumba kigori,
  kamwe kwake sitoyumba,kama wana wa misri,
  hata akina liyumba,kigori kwake makafri,
  Mwaliko ukiupata,waambie na wengine,

  sikutaka kuwaleti,chini wazazi wangu,
  chini nao niliketi,kuhusu kigori changu,
  mamangu alinileti,nijue maisha yangu,
  Mwaliko ukiupata,waambie na wengine,

  tabiaye sio kama,yule wa profu jei,
  togwa taka boga mama,faidisha pedejei,
  twanga pepeta mama,mwanamasanja jjei,
  Ukiupata mwaliko,waambie na wengine,
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi kumbe washairi bado mnafurukuta?
  Hongera!
   
 10. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Loh, Safi sana kwa hizi tenzi. Kipaji maalum hicho.
   
 11. asam.thegunner

  asam.thegunner Member

  #11
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si utani hii kitu imetulia. Hongera sana. Hivi utunzi wa mashairi ni kipaji mtu anazaliwa nacho au naweza kujifunza na nikaweza?
   
 12. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hongera Magulumangu, heko ewe mla halwa
  kufika hata uvungu, japo weye si kulwa,
  wakiri heri za Mungu, kupata binti wamalwa,
  Sasa muweke nyumbani, upate heri za Mungu

  nilipokagua vina, mizani sikudharau,
  kuona langu jina, Judi hukusahau,
  yamoyo kufanya kina, katika yako nahau,
  Sasa muweke nyumbani, upate heri za Mungu

  Heko kupata kigori, uwajibike kwa huba,
  japo waona cha pori, yadumu hayo mahaba
  bila ogopa mahari, kibebe hadi kwa baba
  Sasa muweke nyumbani, upate heri za Mungu

  nimekubali mwaliko, harusiyo kujongea,
  bila kusahau mwiko, wifi yetu mchongea,
  siku afikapo kwako, apate kuyawezea
  Sasa muweke nyumbani, upate heri za Mungu
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160

  Owa s'andame hadaa, moyo ukahadaiwa
  Owa anaye kufaa, mke mwenye kusifiwa
  Owa upate kuzaa, kama ulivyozaliwa
  Owa ukijaaliwa, mupendane na mkeo

  Owa aliye na kheri, muandamane kwa dini
  Owa yai la johari, litiye nuru nyumbani
  Owa mdomo mzuri, ukupambie lisani
  Owa ungiye nyumbani, mupendane na mkeo


  Owa moyo wa imani, usozumbua mafuja
  Owa usiowe duni, anayeitwa kioja
  Owa mtenda wa dini, ndiye mke mwenye haja
  Owa utungiwe koja, mupendane na mkeo

  Owa siowe tambara, linukiyalo vibaya
  Owa mwanamke jura, mlekeze njema ndia
  Owa usiowe sura, kutaka kuzangaliya
  Owa mzuri tabiya, mupendane na mkeo

  Owa kijana kitoto, mteshi wa kutekeya
  Owa akwandike jito, mwenye kukuhurumiya
  Owa usiowe zito, jabali likakwemeya
  Owa aliye na haya, mupendane na mkeo

  Owa s'andame uhuni, upate juwa kuzawa
  Owa nami natamani, ela sijajaaliwa
  Owa utiye chandani, pete uloiteuwa
  Owa ujuwe kuowa, mupendane na mkeo

  Owa uvishwe kilemba, na joho na mahazamu
  Owa wapate kupamba, ukale twiba na tamu
  Owa upambiwe chumba, upate tanganya damu
  Owa usijidhulumu, mupendane na mkeo

  Owa kinda la tausi, alo nadhifu mibele
  Owa kiini cheusi, chendacho nyuma na mbele
  Owa siowe tetesi, apaye watu uwele
  Owa aliye lekele, mupendane na mkeo

  Owa ualike watu, wahudhuriye arusi
  Owa nawe uwe mtu, mkeo simnakisi
  Owa muonyane utu, mukae mutaanasi
  Owa mupane mepesi, mupendane na mkeo

  Owa akukubaliye, akuizao siowe
  Owa upendane naye, zamani sizo ujuwe
  Owa akuridhiyae, mujikubali wenyewe
  Owa mukae mutuwe, mupendane na mkeo

  Owa chenye asimini, kikuba cha asiliya
  Owa kilo na rihani, na waridi maridhiya
  Owa kilicho na shani, na manukato kutiya
  Owa ujuwe duniya, mupendane na mkeo

  Owa utukuze cheo, na jina lipate kuwa
  Owa apate mkeo, aambiwe meolewa
  Owa kama waowao, moyo usiliye ngowa
  Owa ujuwe kukuwa, mupendane na mkeo.

   
 14. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #14
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli nime kukubali ..
  nakuvulia kofia...
   
 15. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #15
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280

  duuuhh
  asante mwaya
  nafurahi kuona na we unawakilisha ...
   
 16. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #16
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280

  Daahhh
  hii kali mkuu
  kwa kweli nimeipenda
  duuhh kipaji mnacho .. namzidi kuongezewa..
   
 17. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Magulumangu nakupongeza
  Kigori wewe kumpata
  Najua mimi ulikopita
  Wivu mi ninao,kujinyonga sijinyongi!!

  Kila la kheri nakutakia
  Furaha katika ndoa
  Watoto nao kupata
  Wivu mi ninao kujinyonga sijinyongi

  Changamoto kwenye ndoa
  Ni sehemu ya maisha
  Uvumulivu uwe nao pia
  Wivu mi ninao kujinyonga sijinyongi
   
 18. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  dada Afrodenzi, asante kwa kunisoma,
  nashukuru kwa kunienzi, vilevile kunipima,
  japo sitoshi konzi, hukuninyima alama
  asante kwayo mapenzi, yadumu enzi na enzi

  yule mtoa posa, alikuja na mizani,
  akatujuza mkasa, aloufumba vinani,
  akakifunga kitasa, cha shairi tusighani
  asante kwayo mapenzi, yadumu enzi na enzi

  Mwenyezi katukirimu, shairi kulithubutu,
  japo sinayo elimu, nimeushinda ubutu,
  pamoja naye hirimu, sijekuwa mtukutu
  asante kwayo mapenzi, yadumu enzi na enzi

  bwa harusi ndiye nguli, wa mashairi na vibonzo,
  mie kama kibakuli, yeye kwangu kisonzo,
  mengi yake maakuli, ya kale kama maganzo,
  asante kwayo mapenzi, yadumu enzi na enzi
   
 19. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #19
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280

  Hii nai print out..

  kwa kweli nakupa heshma sana..
  na uzidi kubarikiwa dear..
  mtu smart anajulikana kwa asemayo..
  i consider your one of them..
  God Bless..
   
 20. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  haha, nilikuwa najaribu tu mpenzi. asante kwa kunitia moyo. ubarikiwe sana mpenzi
   
Loading...