Tamu chungu
Member
- Dec 20, 2015
- 85
- 64
Najitahidi sana kutuma maombi ya kazi kila uchao lakini mpaka sasa sijabahatika kupata ajira ya kunisaidia kuendesha maisha yangu.
Haipiti siku bila kupitia website ya utumishi kuona kama kuna ajira mpya wametangaza.Nimekua muudhuriaji mzuri wa interview zao na mwaka jana nilifanikiwa kuingia mpaka stage ya oral interview lakini walipokuja kuita watu kazini sikuweza kuliona jina langu.
Nawaza kujiajiri lakini tatizo sina mtaji wa kuniwezesha kuanzisha biashara ambayo itanisaidia kusukuma maisha.Umri nao unazidi kwenda yani nachanganyikiwa kupita maelezo.Kuna wakati huwa nawazaaaa bila kupata majibu.
Muheshimiwa Magufuli tunajua uko bize katika kuliweka taifa katika mstari ulionyooka ila tukumbuke na sisi watoto wa wakulima ambao hatuna pakushika na tuna familia zinatutazama.
Kama kuna yoyote ambae amebahatika kupata ajira iwe serikalini au sekta binafsi nakusihi heshimu sana ajira yako mana unaweza ukaidharau lakini kuna mwenzako yupo mtaani hajui lini atapata ajira.