Nimekaribishwa Arusha ila sifa zake nilizosikia si sawa na nilivyoona ona

mr. loner

Senior Member
Aug 1, 2014
168
228
Wadau wa maendeleo poleni na miangaiko ya maisha. Hivi majuzi nilipata safari kwenda arusha nikiwa na rafiki yangu, tulipofika K.I.A ilikuwa mida ya saa moja hivyo nilianza kuangaza kwa nguvu nione mji ulivyo,

tulitembea umbali kidogo mpaka tulipoanza kuta makazi ya watu eneo la Chikatiti, mwenzangu aliniambia kipindi cha nyuma hapo palikuwa pori hivyo kuona nyumba sehemu ni ishara mji umepanuka, tuliendelea na safari na tulipofika usa tuliingia sehemu kidogo kupata kujua jambo fulani, baada ya kupata uhakika wa jambo lenyewe tuliendelea na safari, tulipokaribia eneo la Tengeru tulikutana na foleni ilibidi tuulize kwa wapitaji kulikoni wakasema inasababishwa na ujenzi wa barabara, niliamua kutoa kitablet changu ili kuweka record yangu vema, amadi bila kutegemea alikuja mtu akanipokonya akakimbia nilishuka fasta nimuwai ila sikufanikiwa ikabidi tusitishe safari ili kumtafuta aliyeibeba, katika kuuliza uliza tulitajiwa waporaji watatu ambao ni Yohana aka kipanga, Shombo na Max, na tuliambiwa aliyekuwepo jioni maeneo hayo anaitwa Shombo, tulielekezwa kituo cha polisi nikachukua RB, kesho yake mapema tukaanza msaka Shombo tulipelekwa mpaka kijijini kwake panaitwa Singisi ya mda ila kule tukaambiwa wapo Shombo wengi,

Naomba wadau kama mtu anamjua huyo jamaa anitumie picha yake pm maana mda ulituzidi tukaondoka bila mafanikio, ntatoa zawadi nono kwa atayenipa msaada huo.


Anayway jioni yake tuliendelea na safari hakika upanuzi wa barabara umepamba moto niliona vingi sana ikiwa ni pamoja na wale waliojenga barabarani ambao mpaka sasa hawajabomoa licha ya lami kufika hadi mlangoni, kuna hotel inaitwa snow crest yenyewe ukitoka reception unatua barabarani sasa sijui ni ubabe ama ilijengwa kwa kutojua,

Tulifika kimandolu hali ndio ilikuwa mbaya zaidi nadhani watu wa Arusha wana ubishi wa kijinga tuliamua kuingia ndani ndani huko tulikuta nyumba za udongo nyingine zimeezekwa kwa migomba hapo nikajua bakuli limeoshwa kwa nnje tu. Tuliamua kuenda hadi sakina tulikaa hadi usiku baada ya shughuli tulipita hotel moja nimesahau jina, huwezi amini walikuwepo hadi makakapoa na yana act kikekike nilishindwa kunywa ata soda yenyewe.

Tuliamua tuje mjini kabisa sasa hapa ndio maana wanaita mji wa Arusha jiji la kitalii, ghorofa zote zilizopo katikati ya mji ni hotel, ukiona ghorofa sio hotel jua ni nyumba za NHC tulizunguka usiku wote kujua hali inakuwaje.


Arusha ikifika saa nne ni vigumu sana kupata daladala za kwenda mitaani, daladala nyingi mwisho saa tatu zinaishia.


Arusha ndio mahala pekee na mji pekee makaburi yapo katikati ya mji, mfano ukiwa stand kuu ukiangalia kaskazini kuna eneo lenye ukubwa wa hekari moja nikaambiwa limejaa kaburi tupu, barabara hiyo hiyo ukinyooka nayo kuelekea kituo kikuu cha polisi pia kuna eneo la makaburi kama heka tano hivi alafu yote yamejengewa tofauti na yale ya stand.

Stand kuu ya Arusha haina ata chumba cha matangazo wala mahali unapoweza pata taarifa sahihi imekaa kihuni huni tu hakuna ofisi inayoeleweka, ili kusaidia hali hiyo, wameweka kibanda cha kukaa askari eneo la kutoa mabasi ili kufanya ukaguzi.

Arusha kuna taa za kuongozea magari japo madereva hawajui matumizi yake wengi tuliona wakatiza kienyeji tu.

Tuliamua kwenda unga Ltd huku tuliambiwa ukiangusha ata sh 100 unaweza usiione, tulipofika sheli pale tuliamua tukatize mitaa kwa miguu tuliutembea huu mji sana ila sikuona dalili ya vibaka japo nyumba za udongo zipo kama kawaida.

Arusha wanauza vitu bei ghali sana ila niliambiwa wanauza hivyo sababu ya watalii, wafanyakazi wa UN pamoja na wachimba madini maana wao ukiwaambia hii sahani ni TSHS 60000 hawabargain zaidi utasikia nipe nne.

Wale wazee mnaopenda Ambiance, maeneo ya Africa sana, kimboka na kwingine mnapopajua Arusha napo usikose mitaa ya Sakina ila uwe makini usijechukua kaka poa, alafu round about ya Florida unaingilia kushoto kuna baa kama 9zipo sehemu moja hapo utakuta wa kila aina.



Kwa atakayenisaidia nipate tablet yangu iliyoibiwa Tengeru nitampa zawadi naomba tusaidiane wana arusha mie nimeenda loliondo ntarudi baada ya wiki mbili
 
Hiyo dadapoa inachanganya hiyo taarifa au ulitaka sema kakapoa?au me ndo kilaza.
 
huyu jamaa hata haeleweki...lazima kasoma masomo ya sayansi,maana kuelezea ni zerlo kabisa,in mfalme voice!
 
Pole mzee kwa kuibiwa,A town wadada ndio wanaongoza kwa wizi.Daladala za kwenda Usa kua makini na kila dada utakae kaa nae kwenye gari.In fact mji ni mdogo na hautakiwi kukua sana maana ni mji unaohitaji hewa iwe safi.Hata sasa wamekosea sana kuubana hivyo.
 
madada poa ...wana act kike kike ...so wewe uliwah ona madada poa wana act kiume kiume ....acha fix
 
Arusha,ni_nomaa_sana.
Nimekaa_na_kuishi_uko_almost_2years.

Achana_na_snow_crest_hotel,ungeenda_ngarasero_mountain_lodge_hii_iko_poa_sana_lazima_ungeinjoy.

Wapi_ngaramtoni,vipi_daraja_mbili_ulifika?

Tablets_yako_sahau,hutoipata_hata,hiyo_zawadi_unayotaka_kutoa_fanya_ongezea_pesa_ukanunue_nyingine.

Machalii_ni_watu_wa_hovyo_sana,me_nina_bonge_la_kovu_mgongoni_nilipigwa_kisu_nikaporwa_simu_pale_round_about_ya_florida,,nashukuru_mungu,baada_mwezi_mmoja_wa_mateso_nilipona.
 
Unasema hujawaona hao vibaka mitaa ya mjini...ulitaka wakuibie nn wakat walishakuliza mapema....pengine hawajakuona na chathaman
 
Umeenda kumfufua babu wa kikombe au amerudi umefata huduma ya kikombe kjn
 
Una
Arusha,ni_nomaa_sana.
Nimekaa_na_kuishi_uko_almost_2years.

Achana_na_snow_crest_hotel,ungeenda_ngarasero_mountain_lodge_hii_iko_poa_sana_lazima_ungeinjoy.

Wapi_ngaramtoni,vipi_daraja_mbili_ulifika?

Tablets_yako_sahau,hutoipata_hata,hiyo_zawadi_unayotaka_kutoa_fanya_ongezea_pesa_ukanunue_nyingine.

Machalii_ni_watu_wa_hovyo_sana,me_nina_bonge_la_kovu_mgongoni_nilipigwa_kisu_nikaporwa_simu_pale_round_about_ya_florida,,nashukuru_mungu,baada_mwezi_mmoja_wa_mateso_nilipona.
Unanikatisha tamaa
 
Kutokea kwa mrefu kuelekea usa maeneo hayo chunga mzigo wako hasa simu,ni hatari kwa jinsi wanavyozipitia utadhani walikupa,pia maeneo ya ngarenaro kuanzia saa moja wakati wa foreni za magar,hapi pia kuwa makini zaid,
 
Back
Top Bottom