Nimekamata tunguri za limbwata za mke wangu, nimfanyaje?

katika nyumba watu wanaosali pamoja huishi pamoja.hiyo ni dalili mbaya. weka msimamo wazi usije kuwekewa sumu kwa sababu ya ujinga.Muulize keo taratiiiiibu,kwani ulipoamua kumuoa alitumia tunguli au upendo ulitawala.kama ndio hivyo asitafute shortcut; hazipo maana atakuja kudanganywa kumbe dawa alizopewa ni sumu ikakumaliza taratibu.Maana nami kwa namna fulani niliaathiriwa na ujinga huu toka kwa wamama
 
Nina umri wa miaka 37 na nimeoana na mke wangu huyu miaka mitani iliyopita na tumejaaliwa mtoto mmoja wa miaka mimme na nusu sasa.

Maisha yetu kiuchumi na kimahusiano ni mazuri...kama kuna mikwaruzana ni ile 'ya kawaida' ndani ya ndoa.


Sie wote ni asili yetu ya bara na tumekulia katika maadili mazuri ya Kikristo. Wazazi wetu wote hawakuwavalisha watoto wao yale 'makolokolo' ambayo watoto wengi huwa wanavaa na hadi sasa kati yetu wawili hakuna aliye na 'chale' mwilini kumaanisha kwamba hatukuwa waumini wa mambo ya kienyeji!


Last week nilikuwa safarini kikazi lakini nikarudi nyumbani siku 1 kabla ya siku iliyokuwa ikijulikana pale nyumbani. Nyumbani hakukuwa na mtu maana wote huwa tunaenda makazini na shuleni except housemaid aliyekuwa amesafiri wakati huo. Kwa kuhitaji Pasi (Iron) iliyokuwepo chumba cha wasichana kinachotumiwa na housemaid na mdogo wake wife, niliifuata. Next to ilipokuwepo Pasi, kulikuwa na mfuko mdogo wa plastic (Rambo) ambao nilivutiwa kuuangalia.


Nilipoufungua-nilikaribia ku-faint kwa niliyoyaona!!!!! Kulikuwa na karatasi kama 3 zenye maandishi ya kiarabu na in between some lines kulikuwa na ama jina la mke wangu au langu. Pia kulikuwa na karatasi kadhaa zilizoandikwa kiarabu na maelezo kama 'CHOMA OGA 1 X 2 SIKU 3, CHOMA MWINAMO' pia kulikuwa na vitu kama unga unga kwenye makaratasi yenye maelekezo 'CHAKULA LIMBWATA' na 'KUNYWA 1 X 3 SIKU 6 na KUNYWA USIKU TU SIKU 2'.

Kiufupi ni tunguri za limbwata. Nikaenda mjini kuwatafuta wanaojua maandishi haya na kuongeza uhakika niliwaulizia watu wawili tofauti sehemu tofauti na wote walinitafsiria kitu kimoja kwamba ni dawa toka kwa mganga za mtu anaeitwa (jina la mke wangu ndani ya baadhi ya karatasi zile) akitaka kumtia kwenye chupa mtu anaeitwa (jina langu) yaani nisisikie wa kuona wala kupinga chochote!
Nilipowauliza, eti shemeji yangu anasema mzigo ni wa kwake ambapo kwa mimi naamini kaamua kuji-sacrifice. Wife yeye ameendelea kuukana katkata ule mzigo.

My take:
Kama ameshaanza biashara ya waganga wa kienyeji, leo kwa hilo, next time ataniendea kwa lipi? Mke wangu hakuwa mshabiki kabisa wa mambo kama hayo, sasa hofu yangu ni kwamba ameshaanza mambo ya mjini likely kudanganywa na wanawake wa mjini (Tanga) maana ni mambo common.
What should I do?
Tafakari na chukua tahadhari kabla hujawa zezeta
 
Maadamu umeyaona hayana nguvu tena hayo, ila mwambie kwa upole asirudie kitendo hicho pia jiangalie nawe umebadirika wapi katika mienendo yako
 
msamehe mkeo tatizo ni uelewa mdogo alionao...
na pia labda umemfanya afeel insecure kuhusu hio ndoa..
jichunguze wewe mwenyewe kwanza...uhusiano wako na yeye ukoje
 
Kwanza kabisa nakupongeza maana naona pamoja na kukuta vitu hivyo bado umekuwa mtulivu na hukupanic kama watu wengi wanavyofanya. Pia nakupongeza umegundua kuwa mke wako huenda amedanganywa kiasi cha kujiingiza kwenye mambo hayo ambayo kimsingi hayana maana na sidhani kama sayansi hiyo ingekuwa na msaada kwake. Unachotakiwa kukifanya kwa utaratibu kabisa kaa na mke wako mueleze kuwa imani za namna hiyo haziwezi kumsaidia chochote na umfahamishe bayana kuwa hana sababu ya kujiingiza katika vitendo hivyo kwani wewe utaendelea kumpenda bila hata ya yeye kufanya juhudi kama hizo ambazo matokeo yake zinamtia kwenye aibu na kuhatarisha uhusiano uliopo. Mjulishe bayana kuwa lugha ya limbwata ni mambo ya kufikirika na laiti yangekuwapo kusingekuwa na talaka za kila wakati. Mjulishe na umfahamishe kuwa umemsamehe lakini iwe ni mwanzo na mwisho yeye kujihusisha na mambo hayo viginevyo hutavumilia tena na mambo ya kishirikina na ikitokea hivyo hutasita kuchukua hatua kali dhidi yake.
 
Nini chanzo? Si rahisi mwanamke akurupuke tu eti akutafutie malimbwata. Tangu Lini mwenye afya akamtafuta daktari?
Hakika kuna tatizo ndani ya nyumba yenu ambalo unaweza kuwa umeshindwa kulitatua. Lazima mkae na kuongea. Huenda aliona njia pekee ya kunusuru ndoa yake ni kutumia dawa hizi. Inawezekana kabisa amefanya hivyo kwa nia njema.

Nitoe mfano: Ninaye kaka yangu anakunywa sana pombe kiasi cha kutisha na inasababisha aharibu mfumo mzima wa familia. Ana elimu nzuri na alikuwa na kazi nzuri kwa miaka 16. Leo hii hana hata baiskeli au Tsh 20,000 za akiba. Tatizo ni pombe!! Nimejitolea kumtafutia dawa ili aache pombe. Tena nitampa bila yeye kujua. Up hapo???
 
kaka mtimue atakuua ayo matumguri so mazuri ata kidogo,tena una baati kama alikua ajaanza kukupa dozi umepona couse mi nshashuudia mtu mmoja wa karibu sana na mimi alinyweshwa na mke wake'sjui uyo mama alizidisha dozz au vp'ila kilichotokea ni kwamba yule mzee aliparalaizi kwa mda wa miaka 20yupo kitandani'kwa iyo basi fanya utafiti wako ukigundua kama ni kweli UYO MKE WAKO AKUFAIIIIIII ATA KJDOGO
 
KAKA jE UMEJIULIZA WEWE MWENYEWE KAMA UMEBADILIKA HASA KIMAPENZI KULIKO ULIVYOKUWA WAKATI UNAMUOA?

Hawezi mwanamke kukuendea kwa mganga au limbwata kama hajagundua mapungufu yeyote ndani ya ndoa yenu hasa mapenzi uliyo nayo sasa kulinganisha na yale wakati unamuoa labda kaka umepunguza kumjali na kumfariji kama ilivyokuwa awali hivyo lazima afanye kitu na kwasababu baadhi yetu wanaume hatuna muda wakukaa na wake zetu na kuongeo nao kama marafiki wa karibu na wapenzi wetu badala yake tunageuka mbogo hivyo hata kukuuliza linapotokea tatizo au kulegalega kwa mapenzi yenu anakuwa muoga matokeo yake badala ya kukuomba ushauri na kukueleza pindi linapotokea tatizo anakuogopa na kwenda kuomba ushauri kwa mashoga zake ambao wengine watamshauri kwenda kwa waganga

Zingatia haya kwa kuwa na maisha mazuri ya ndoa yasiyohitaji kwenda kwa waganga

  1. Love is a process and not a destination
  2. Mkeo au mpenzio mfanye kuwa rafiki yako wa karibu sana jenga mazingira ya kumuomba ushauri na kuongea naye kwa furaha
  3. Usichukue maamuzi yeyote wakati unapokuwa na hasira kwani hasira hasara jipe muda mpaka utakapokuwa kawaida huna hasira tafakari kwa kina ndipo uchukue uamuzi unaotaka kuchukua
  4. Jenga mazingira ya kuongea na mkeo/mpenzi wako wakati mwingine muwe mnataniana hapa na pale mf kupigana mito kama watoto na utani wa hapa na pale hii itamfanya mkeo awe karibu zaidi na wewe na wakati mwingine itafanya kwake kuwa rahisi zaidi kujieleza kwako
  5. Mkigombana hakikisheni kama mna watoto au majirani wasijue kuwa baba na mama au jirani wanagombana na kama mmojawapo kati yenu akiwa anafoka basi mmojawapo ajitahidi kufanya ashuke chini na kiri kosa na samehekama umeombwa msamaha na kama halisameheki jipeni muda wa kurekebishana ikishindikana achaneni kwa wema
  6. ombaneni Msamaha na hakikisheni mmesamaheana kabla hamjapanda kitandani
  7. Jenga mazingira ya kumsaidia mkeo baadhi ya kazi bila hata kukuomba kwa mfano kama uko nyumbani mkeo yuko bize na kukupikia chai basi wewe waweza saidia kunyoosha nguo zako na zake au jhata nepi za mtoto au kufua nguo za ndani/za kawaida za kwako na zake pia
  8. Pendelea kula pamoja na mkeo na wakati mwingine mlishe wakati wa usiku utakaporudi kazini na jenga mazingira ya kukaa nyumbani siku za mwisho wa wiki kama huna cha muhimu cha kufanya nje ya nyumba yako maana kuna wababa wengine wikitatu hajawaona watoto wake wakati analala hapo hapo nyumbani
  9. Tumia macho yako kumuangalia kwa mapenzi macho nikiungo kizuri sana kukitumia na kumfanya mkeo ajisikie kuwa hakuna mwingine zaidi yake. unaporudi toka kazini mkumbatie na umbusu mkeo na mpe ahsante kwa chochote atakachokufanyia mfano ukimbembea ukimaliza mshukuru, kakupikia ukala ukashiba kakufulia na kukunyooshea nguo mpe ahsante hii inamfanya ajisikie faraja sana.
  10. Ongea naye kwa upole na ustaarabu hata kama umekasirika na kama akiwa anakuja juu labda kunakosa umemfanyea jitahidi kumfanya apunguze hasira kwa kumkumbatia hata kwa nguvu kisha msugue mgongoni kwa mkono wako mmoja na mwingine ukiwa unamchezea nywele na kumsugua kisogoni huku ukimueleza maneno mazuri yakumfanya atulie akishatulia ombaneni msamaha kwani si vizuri kulala kitanda kimoja huku mmenuniana malaika wa riziki hawezi kuja hapo
  11. Kumbuka kutumia maneno haya matatu ni muhimu sana kwenye maisha yenu ya ndoa 1.Pole 2.Samahani 3.Ahsante
  12. kumbuka kubomoa ni rahisi kuliko kujenga nyumba kuijenga inachukua zaidi ya mwa\ezi lakini kuibomoa ni siku moja tu. EPUKA MAAMUZA YATAKAYOFANYA MTENGANI LABDA TU IKIBIDI NAITABIDI UJIULIZE MARA MBILI MBILI NDIO MAANA NAKUSHAURI KWENYE MAISHA HAYA YA MAHUSIANO USIJECHUKUA MAAMUZI WAKATI UKIWA NAHASIRA KWANI WAWEZAJUTA
YANGU NI HAYO TU
 
Back
Top Bottom