Nimekamata tunguri za limbwata za mke wangu, nimfanyaje?

Mkuu, mimi sijaoa lakini nilishakutana na hivi vitimbwi mara kazaa mara kwenye mto kitandani mara mezani! karibu mara mbili lakini mara zote nikiona nilikuwa nachukia siwaambii wala sifanyi kitu ila nafukuza. Lakini siku zote nimekuwa nikijiuliza, hivi haya yataendelea hadi lini? Niliye naye sasa hivi ambaye ndo nimepanga kumuoa hapo mwakani na mwaliko kwa wanaJF ni lazima, nikiona anafanya vitu vya ajabu! namtafutia muda safi tunaenda sehemu tunakaa hapo hata siku mbili tunayamaliza, tena anajisikia vizuri.

Tatizo kubwa inawezekana ulishakuwa mtumwa wa kazi/pesa huna muda wa kutosha kukaa nyumbani, inakera sana hiyo! maisha yanakuwa siyo ya ndoa tena bali ni kutafuta pesa tu kila wakati which is totally different. Inabidi utafute muda kaa na mkeo ongea naye vizuri, fanyeni maombi mara kwa mara, jiwekeni wazi, muwe huru kuelezana mambo yenu ukifanya hivyo mkuu mtakuwa kama ndo mumeonana jana, mapenzi moto moto kaka.

Ni hayo tu, ila pole na hakuna haja ya kumkimbia au kumuacha au kununa, huyo ni mke wako wekeni sawa mambo yenu ya ndani hayoooo. Hapa kuna mazuri na mabaya kwa hiyo uwe makini tu, saa nyingine kuna ukweli unasemwa hapa sasa inabidi uupuuze au uufanyie kazi kwa faida ya familia yako.
 
mi hata sioni tatizo kama hiyo story hapo ya first lady, kama hilo limbwata ni kwa ajili ya wewe kumpenda mkeo poa tu tena mpe ushirikiano ila mapenzi yawe motomoto as long as sio la kukudhuru kiafya au kuondoa uhai
ni mimi wa tanga handeni,nawakilisha
Mzuanda unasema "limbwata ni kwa ajili ya wewe kumpenda mkeo poa tu tena mpe ushirikiano ila mapenzi yawe motomoto as long as sio la kukudhuru kiafya au kuondoa uhai"

nina uhakika limbwata linadhuru afya kwa kuwa ni aina ya uchawi wa kupumbaza akili na mtoa topiki ameelezea dozi ilivyo kwa maana hiyo kama akizidisha dose inaweza ikaleta madhara mengine nimewahi kushuhudia mama mmoja alimpeleka mumewe kanisani alikuwa chizi na yule mama akatubu kuwa alimwekea dawa ili ampende akakosea masharti mumewe akawa mwendawazimu akaachishwa kazi wakapoteza mwelekeo na yule mama alikuwa mama wa nyumbani hana kazi na mwisho wake akaamua kuokoka
 
Anko, hiyo bahati mbaya ndio sera ya mabinti kadhaaa-kwamba lazima umdhibiti mumeo ili kila anachotaka yeye umpe-awe na sauti juu yako. Haihusiani kabisa na mume kubadilika !!! Mrudishe kwao kwanza kwa muda mpaka hapo atakapo omba msamaha na ahidi kuwa hatorudia !
 
Ushauri wangu ni kwamba kama wewe umeshapata jibu kuwa hayo madubwasha yalikulenga wewe na yeye anakataa basi mweleze ukweli na wala usiendelee na malumbano nae na huyo mdogo wake mfukuze hapo kwako na pia acha kula hapo nyumbani kwako na maji ya kuoga jiandalie mwenyewe na umweleze wazi kuwa hautokula hapo mpk a-confess kuwa hayo mavitu ni yake na akuombe radhi ndipo ulegeze masharti na pia kama kuna chumba kingine hamia huko weka mgomo hata kulala nae na nguo zake peleka kwa dobi kabisa.

kuna watu wengi sana wanapumbazwa akili na wake zao na kudhurika sana na huu uchawi kuna wengine wanawekea limbwata (wanaopenda sana kazi) ili ashau kazi hawai kurudi home, wengine wanawekea haya mauchawi ili kama akikuomba hela umpe tu bila kufikiria na matokea yake ni kurudisha maendeleo ya taifa nyuma.

Katika vitu ambavyo sivipendi katika maisha yangu ni 1. wizi 2. uchawi na hata kama nataka kuishi sehemu lazima niangalie sana hivyo vitu viwili kwa umakini sana kabla sijafanya decision.

Kwenye sheria ya ndoa ya mwaka 1974 inasema kuwa vitu ambavyo vinaweza kusababisha ndoa kuvunjwa ni Uzinzi (wanandoa kutoka nje ya ndoa) ugomvi uliokithiri, vipigo, uchawi (ushirikina) na kunyimana tendo la ndoa

kuwa mkali kaka usilete mzaha katika ili jambo chukua hatua mapema sio kwa kunyenyekea pia jiangalie mapungufu yako ujirekebishe na wala usimtoe out huyo mkeo na kuenda kuongea nae kama hajatubu utakuwa unampigia mbuzi gitaa akikisha anakubali kosa ndio mtoke mkaongee na kujadili wapi kwenye tatizo ili muende sawa. Narudia huyo mdogo wake mtimue haraka sana atavuruga ndoa yenu inaonyesha anashirikiana nae kukuroga
 
Mkuuu huku utapata wezi wa ndoa yako tuuuuu basii we kaa na mkeo tafuta sababu za yeye kufanya hivyo na mwambie anataka uweje mkae msuluhishe hata familia awatakusaidia nasema hivi kama mwanandoa nikiwa nimesimama na ndoa iliopita kwenye mabonde na milima wewe na mkeo ndio suluhisho la hili na kama uamini mpigie hata wazazi wako hii issue uone kama mtakaa kwa amani la maana simama na mungu kama aujaokoka anza sasa bado ujachelewa karibu sana pale biafra kwenye nyumba ya ibada kwa mwakasege upate neema ya bwana mungu asimame na ndoa yako tunaitaji kumwachia mungu asimame na ndoa zetu watu wengi wanahisi ukiwa na pesa nyumba nzuri shule nzuri na mengineyo ndoa imetulia kwa info wenye haya yote waulize usiku wanalalaje wacha ukiwaona mjini wanacheka kama si mngo wa 4 basi gorofa ya chini na ya juu isiwe kwako in jesus name

Ni ushauri mzuri sana kumtaka mwuliza swali amtegemee Mungu. Ila ingefurahisha kama keyboard yako ingekuwa na alama za mikato na vituo.
 
Muondoe Shemeji yako kwako. Ongeza ukaribu na mke wako ili kumpa uhakika kwamba bado unamthamini pia uweze kuangalia nyendo zake kwa karibu.
 
Mpe likizo.. aende kwa wazazi wake akajifunze upya...!!!! hala hala usije ukawa ulioa kwa zinguo la hiyo kitu!!!
 
Sina uhakika na umri wa Shemejio, lakini usije shangaa ikawa ni kweli kwamba Shemeji yako ndiye mwenye huo mzigo anataka kuwadhibiti wewe na mkeo ili kila atakachosema mumkubalie.
i think soo pia. au hg nao wanakuwa wamo. kama yeye ndo mpishi, mwandaaji maji ya kuoga anaweza akateki advantage hiyo. vunja ukimya sema na mkeo kwa taratibu atasema yote. hata huyo shemejio mhoji iweje ayaweke majina yenu badala ya yake ikiwa kweli ni mzigo wake.ukweli husimama daima
 
Mpe likizo.. aende kwa wazazi wake akajifunze upya...!!!! hala hala usije ukawa ulioa kwa zinguo la hiyo kitu!!!

Sidhani kama hili litasaidia... Sana sana akienda huko ndo ataanza kuzunguka wa hao walozi ili arudi kwa nguvu mpya...

Kaa na mkeo, muonye... hizo ni kazi za shetani, ajue wazi kuwa dawa sio nzuri, zinaweza kufanya ukawa chizi au taahira, sasa mweleze kama hiyo ndio nia yake na kama litamfurahia...

Otherwise, Kesheni Mkiomba... Maana shetani hachoki
 
daah hawa kina mama tunawapenda lkn sometimes...................acha tu.............mungu ndiye anayetulinda bro.................sometimes tunalishwa mauchafu mengi...................!
 
Pole sana mkuu! Ndoa ni ngumu na hilo ni jaribu kubwa sana kutoka kwa mwovu. Usitake talaka, bali chukua siku muondoke nyumbani mwende mahali penye mandhari mazuri alafu muelezani yote moyoni. Anataka kukuuza kwa shetani hivi hivi! Ivi unajua kuwa mke/mume anaweza kukuuza kwa shetani? Maana nyie sasa ni mwili mmoja na atakachoruhusu hapo nyumbani kitakuwa kitapata full permission! chunga sana aise!
 
Pole sana! Rudisha kwao mpaka aseme ukweli na ahaidi hatarudia tena.. Nimeona MADHARA ya hiyo kitu kwa jamaa yangu... Mwishowe ataleta mtoto sio wako na utamkubali bila shida bila hatua yoyote,,, Na mengine mengi sana tu.. Pole Kiongozi.
 
Hapo Bro tatizo halijaisha, najaribu kufikiria maisha ya kawaida hakuna migogoro na anajua unampenda aanze mambo ya matunguri. Mbaya zaidi amekana katu katu halafu mtu anakwambia mwache tu. Hivi kweli kama alikuwa na nia njema ya kukutafutia dawa umpende kulikuwa na haja gani ya kukataa wakati kwenye maadishi kuna jina lako na la mkeo!
Usilichukulie kwa wepesi suala hili! Nimeona watu wakidhurika kwa malimbwata haya! Mwambie kinagaubaga kabisa kwamba we have to talk. Na ikibidi upige mkwara wa kufa mtu usipopata majibu yasiorithisha. Utautambua tu ukweli kama atakwambia ukweli! Tafuta kisa na mkasa wa yeye kuleta matunguri ndani ya nyumba! Kuwa mkali bro na siku zote take charge of your house, have your final say, be authentic, mheshimu na umthamini mkeo na kama unahisi wewe kwa namna moja ama nyingine unaweza kuwa chanzo cha yote hayo, Jirekebishe!
Lakini kwanza kitendawili hicho lazima ukitegue! Otherwise you will never be at peace with your wife!
 
Back
Top Bottom