Nimejifunza kitu kuhusu Sadaka

Nimejifunza kitu kuhusu Sadaka

Cornelius ilikuaje

MATENDO 10​

Petro na Kornelio
1Kulikuwa na mtu mmoja huko Kaisarea aitwaye Kornelio, jemadari wa kikosi kimoja kiitwacho “Kikosi cha Italia.” 2Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima. 3Yapata saa tisa alasiri, aliona dhahiri katika maono malaika wa Mungu akiingia ndani na kumwambia, “Kornelio!” 4Kornelio alimkodolea macho huyo malaika kwa hofu, akamwambia, “Kuna nini Mheshimiwa?” Huyo malaika akamwambia, “Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini wala hatazisahau. 5Sasa, watume watu Yopa wakamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro. 6Yeye yumo nyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngozi ambaye nyumba yake iko karibu na bahari.” 7Huyo malaika aliyesema hayo alipokwisha kwenda zake, Kornelio aliwaita watumishi wawili wa nyumbani na mmoja wa askari zake ambaye alikuwa mcha Mungu, 8akawaeleza yote yaliyotukia, akawatuma Yopa.
9Kesho yake, hao watu watatu wakiwa bado safarini, lakini karibu kufika Yopa, Petro alipanda juu ya paa la nyumba yapata saa sita mchana ili kusali. 10Aliona njaa, akatamani kupata chakula. Chakula kilipokuwa kinatayarishwa, akaota ndoto. 11Aliona mbingu zimefunguliwa na kitu kama shuka kubwa inateremshwa chini ikiwa imeshikwa pembe zake nne. 12Ndani ya shuka hiyo kulikuwa na kila aina ya wanyama: Wanyama wenye miguu minne, wanyama watambaao na ndege wa angani. 13Akasikia sauti ikimwambia: “Petro, amka uchinje, ule!” 14Petro akajibu, “La, Bwana; mimi sijaonja kamwe chochote ambacho ni najisi au kichafu.”
15Ile sauti ikasikika tena ikimwambia: “Usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa!” 16Jambo hili lilifanyika mara tatu, kisha ile shuka ikarudishwa juu mbinguni.
17Petro alipokuwa bado anashangaa juu ya maana ya hayo maono aliyokuwa ameyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, baada ya kuigundua nyumba ya Simoni, walifika mlangoni, 18wakaita kwa sauti: “Je, kuna mgeni humu aitwaye Simoni Petro?”
19Petro alikuwa bado anajaribu kuelewa yale maono, na hapo Roho akamwambia, “Sikiliza! Kuna watu watatu hapa, wanakutafuta. 20Shuka upesi na wala usisite kwenda pamoja nao kwa maana ni mimi niliyewatuma.” 21Basi, Petro akateremka chini, akawaambia hao watu, “Mimi ndiye mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?” 22Wao wakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote, ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote ulicho nacho cha kusema.” 23Petro akawakaribisha ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule.
Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatana naye. 24Siku ya pili yake walifika Kaisarea na huko Kornelio alikuwa anawangojea pamoja na jamaa na marafiki aliokuwa amewaalika. 25Petro alipokuwa anaingia, Kornelio alitoka nje kumlaki, akapiga magoti mbele yake na kuinama chini kabisa. 26Lakini Petro alimwinua, akamwambia, “Simama, kwa maana mimi ni binadamu tu.” 27Petro aliendelea kuongea na Kornelio wakiwa wanaingia nyumbani ambamo aliwakuta watu wengi wamekusanyika. 28Petro akawaambia, “Nyinyi wenyewe mnajua kwamba Myahudi yeyote amekatazwa na sheria yake ya dini kushirikiana na watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amenijulisha nisimfikirie mtu yeyote kuwa najisi au mchafu. 29Kwa sababu hiyo, mliponiita nimekuja bila kusita. Basi, nawaulizeni: Kwa nini mmeniita?” 30Kornelio akasema, “Siku tatu zilizopita saa kama hii, saa tisa alasiri, nilikuwa nikisali chumbani mwangu. Ghafla, mtu aliyekuwa amevaa mavazi yenye kungaa alisimama mbele yangu, 31akasema: ‘Kornelio! Sala yako na sadaka zako kwa maskini zimekubaliwa na Mungu. 32Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro; yuko nyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngozi karibu na bahari.’ 33Kwa hiyo nilikutumia ujumbe bila kuchelewa, nawe umefanya vyema kuja. Sasa, sisi tuko mbele ya Mungu, kusikiliza chochote ambacho Bwana amekuamuru kusema.”
Hotuba ya Petro
34Hapo Petro akaanza kusema: “Sasa nimetambua kwamba hakika Mungu hana ubaguzi. 35Mtu wa taifa lolote anayemcha Mungu na kutenda yaliyo sawa anapokelewa naye. 36Huu ndio ule ujumbe Mungu alioupeleka kwa watu wa Israeli, akitangaza Habari Njema iletayo amani kwa njia ya Yesu Kristo ambaye ni Bwana wa wote. 37Nyinyi mnajua jambo lililotukia katika nchi yote ya Wayahudi kuanzia Galilaya baada ya ule ubatizo aliohubiri Yohane. 38Mnamjua Yesu wa Nazareti na jinsi Mungu alivyomteua kwa kummiminia Roho Mtakatifu na nguvu. Mungu alikuwa pamoja naye; yeye alikwenda huko na huko akitenda mema na kuwaponya wote waliokuwa wamevamiwa na Ibilisi. 39Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyotenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu. Walimuua kwa kumtundika msalabani; 40lakini Mungu alimfufua siku ya tatu, akamfanya aonekane, 41si kwa watu wote, ila kwa wale Mungu aliokwisha wachagua wawe mashahidi wake, yaani sisi tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. 42Alituamuru kuihubiri Habari Njema kwa watu wote na kushuhudia kwamba yeye ndiye aliyeteuliwa na Mungu awe Mwamuzi wa walio hai na wafu. 43Manabii wote waliongea juu yake kwamba kila mtu atakayemwamini atasamehewa dhambi zake zote kwa jina lake.”
Kornelio na jamaa yake wanampokea Roho Mtakatifu
44Wakati Petro alipokuwa bado anasema maneno hayo, Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliokuwa wanasikiliza ujumbe huo. 45Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia kipawa cha Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia; 46maana waliwasikia wakiongea kwa lugha mbalimbali wakimtukuza Mungu. Hapo Petro akasema, 47“Watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi wenyewe tulivyompokea. Je, kuna yeyote atakayeweza kuwazuia wasibatizwe kwa maji?” 48Basi, akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Kisha wakamwomba akae nao kwa siku chache
 
Safiiii
Jumapili iliyoisha Nilienda mwenye ibada kama kawaida, nikaketi Mistari kadhaa kutoka mbele, kwa kuwa nilikuwa nimewahi,

Ibada iliendelea kwa Kwaya za kanisani kwetu kutoa ujumbe kwa njia ya uimbaji na baadae Matangazo,

Katikati Ya ibada, Nilipata simu ya dharula Nikatoka nje kwa muda kidogo (Niliweka Vibration) Na ilikuwa ni simu muhimu kwa hyo ilibidi nipokee kisha Kurudi kuendelea Na Ibada.

Wakati narudi, Nilikuta sehem Niliyokaa Tayari kuna waumini wengine wamekaa na Kanisa lilishaanza kufurika, Mbele yangu kulikuwa na benchi 2 Za mwanzo ambazo bado zilikuwa bado na Ma gap, kwa hyo nikakaa benchi Moja wapo.

Mbele Yangu alikaa Mzee mmoja Ambaye nilipomwangalia, Ilikuwa tu Ni kama kapewa shati hilo sehemu, au hana option nyingine, lilikuwa ni shati Chafu, halijanyooshwa Na suruali vile vile, Pembeni alikuwa na mfuko aliobeba vitu ambavyo Sikuvijua.

Lakini pia alikuwa na kofia ambayo kwa Heshima na Madhabahu Alikuwa ameivua na kuiweka juu Ya Mfuko wake.

Mahubiri Yalianza, akawa na karatasi na kalamu anaandika na anafatilia kwa umakini,

Nilimwangalia miguuni Nikaona hana viatu na pembeni Yake kulikuwa na ndala zilizochakaa,

Muda wa sadaka ulifika, Hakusimama kwenda kutoa Sadaka. Kwanza kabla Ya sadaka nilianza kuwaza sana kuhusu Huyu mzee na passion aliyokuwa nayo licha ya kuonekana na Maisha magumu,

Alifatilia ibada, aliandika, alisikiliza kwa umakini, lakini nilimuona zaidi akiwa mnyonge wakati tunaenda kutoa sadaka na yeye hana.

Kabla hata ya kunyanyuka tayari linishawaza sana, Huyu baba huenda ana watoto tena wakubwa, Hana mavazi ya kuvutia kama wengine, Nikawa najiuliza anakula wapi? Amekujaje? Akitoka hapa anarudije? Anajisikiaje?

Nilipotoka kutoa sadaka Moyo wangu uliniambia "LEO SADAKA YANGU KUBWA NI KUMPA HUYU MZEE CHOCHOTE"
Nilimfata nikamshika mkono kama naongea nae kisha nikiwa nimekunja pesa mkononi nikampa, Akashtuka sana, kwa sababu nadhani hakutegemea, Alipoangalia mkononi, Niliona tabasamu kubwa sana kutoka kwake, Nikakunja mikono kumshukuru bila kuongea kisha nikaondoka..Alitamani aseme kitu lakini tayari Nikawa nimeshaondoka.

Jumapili ile, imenikumbusha KUTOA SADAKA sio tu kanisani au msikitini, Kuna aina Nyingi ya watu kama huyu mzee mtaani kwetu, kina mama wajane, n.k TUWAPE CHOCHOTE, tutenge siku hata moja tu unazunguka kidogo unamkuta mama anachoma mahindi nunua mhindi wako muachie hata elf 5 akawalishe wajukuu..Nadhani hizi ndio sadaka za kweli.

Poleni kwa kuwachosha na story Ndefu.
 
True kwenye mama mchoma mahindi kumuachia elf 5 hapa umemsaidia ni sadaka tosha.
Maana Hakuna mwanamke ambae hana mtoto au familia akahangaika kuuza mihogo,vitumbua,uji,mboga,mahindi nk.
Kuanzia leo nikitoa elf 10 kununua mahindi sidai chenji hio chenji inaenda saidia vijomba huko nyumbani
Yaani kuna watu wengi ambao ukimuona tu wala hajawahi kuwa omba omba, haombi watu na anahangaika na hizo hizo karanga za mia kujitafutia hela ya kula, unaweza ukawa unamfatilia hata siku 3 kujiridhisha, na siku moja ukapita tu ukanunua karanga hata 5 kisha ukamwachia chenji..

Kama tunao uwezo wa kula piza na mazaga kibao unaacha 80k mlimani city kwa nusu saa, ukimpa mhitaji hyo elf 5. atakushukuru na atakuombea.
 
Yaani kuna watu wengi ambao ukimuona tu wala hajawahi kuwa omba omba, haombi watu na anahangaika na hizo hizo karanga za mia kujitafutia hela ya kula, unaweza ukawa unamfatilia hata siku 3 kujiridhisha, na siku moja ukapita tu ukanunua karanga hata 5 kisha ukamwachia chenji..

Kama tunao uwezo wa kula piza na mazaga kibao unaacha 80k mlimani city, kwa nusu saa, ukimpa mhitaji hiyo elfu 5 atakushukuru na atakuombea.
 
Jumapili iliyoisha Nilienda mwenye ibada kama kawaida, nikaketi Mistari kadhaa kutoka mbele, kwa kuwa nilikuwa nimewahi,

Ibada iliendelea kwa Kwaya za kanisani kwetu kutoa ujumbe kwa njia ya uimbaji na baadae Matangazo,

Katikati Ya ibada, Nilipata simu ya dharula Nikatoka nje kwa muda kidogo (Niliweka Vibration) Na ilikuwa ni simu muhimu kwa hyo ilibidi nipokee kisha Kurudi kuendelea Na Ibada.

Wakati narudi, Nilikuta sehem Niliyokaa Tayari kuna waumini wengine wamekaa na Kanisa lilishaanza kufurika, Mbele yangu kulikuwa na benchi 2 Za mwanzo ambazo bado zilikuwa bado na Ma gap, kwa hyo nikakaa benchi Moja wapo.

Mbele Yangu alikaa Mzee mmoja Ambaye nilipomwangalia, Ilikuwa tu Ni kama kapewa shati hilo sehemu, au hana option nyingine, lilikuwa ni shati Chafu, halijanyooshwa Na suruali vile vile, Pembeni alikuwa na mfuko aliobeba vitu ambavyo Sikuvijua.

Lakini pia alikuwa na kofia ambayo kwa Heshima na Madhabahu Alikuwa ameivua na kuiweka juu Ya Mfuko wake.

Mahubiri Yalianza, akawa na karatasi na kalamu anaandika na anafatilia kwa umakini,

Nilimwangalia miguuni Nikaona hana viatu na pembeni Yake kulikuwa na ndala zilizochakaa,

Muda wa sadaka ulifika, Hakusimama kwenda kutoa Sadaka. Kwanza kabla Ya sadaka nilianza kuwaza sana kuhusu Huyu mzee na passion aliyokuwa nayo licha ya kuonekana na Maisha magumu,

Alifatilia ibada, aliandika, alisikiliza kwa umakini, lakini nilimuona zaidi akiwa mnyonge wakati tunaenda kutoa sadaka na yeye hana.

Kabla hata ya kunyanyuka tayari linishawaza sana, Huyu baba huenda ana watoto tena wakubwa, Hana mavazi ya kuvutia kama wengine, Nikawa najiuliza anakula wapi? Amekujaje? Akitoka hapa anarudije? Anajisikiaje?

Nilipotoka kutoa sadaka Moyo wangu uliniambia "LEO SADAKA YANGU KUBWA NI KUMPA HUYU MZEE CHOCHOTE"
Nilimfata nikamshika mkono kama naongea nae kisha nikiwa nimekunja pesa mkononi nikampa, Akashtuka sana, kwa sababu nadhani hakutegemea, Alipoangalia mkononi, Niliona tabasamu kubwa sana kutoka kwake, Nikakunja mikono kumshukuru bila kuongea kisha nikaondoka..Alitamani aseme kitu lakini tayari Nikawa nimeshaondoka.

Jumapili ile, imenikumbusha KUTOA SADAKA sio tu kanisani au msikitini, Kuna aina Nyingi ya watu kama huyu mzee mtaani kwetu, kina mama wajane, n.k TUWAPE CHOCHOTE, tutenge siku hata moja tu unazunguka kidogo unamkuta mama anachoma mahindi nunua mhindi wako muachie hata elf 5 akawalishe wajukuu..Nadhani hizi ndio sadaka za kweli.

Poleni kwa kuwachosha na story Ndefu.
Hakika
 
MATENDO 10​

Petro na Kornelio
1Kulikuwa na mtu mmoja huko Kaisarea aitwaye Kornelio, jemadari wa kikosi kimoja kiitwacho “Kikosi cha Italia.” 2Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima. 3Yapata saa tisa alasiri, aliona dhahiri katika maono malaika wa Mungu akiingia ndani na kumwambia, “Kornelio!” 4Kornelio alimkodolea macho huyo malaika kwa hofu, akamwambia, “Kuna nini Mheshimiwa?” Huyo malaika akamwambia, “Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini wala hatazisahau. 5Sasa, watume watu Yopa wakamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro. 6Yeye yumo nyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngozi ambaye nyumba yake iko karibu na bahari.” 7Huyo malaika aliyesema hayo alipokwisha kwenda zake, Kornelio aliwaita watumishi wawili wa nyumbani na mmoja wa askari zake ambaye alikuwa mcha Mungu, 8akawaeleza yote yaliyotukia, akawatuma Yopa.
9Kesho yake, hao watu watatu wakiwa bado safarini, lakini karibu kufika Yopa, Petro alipanda juu ya paa la nyumba yapata saa sita mchana ili kusali. 10Aliona njaa, akatamani kupata chakula. Chakula kilipokuwa kinatayarishwa, akaota ndoto. 11Aliona mbingu zimefunguliwa na kitu kama shuka kubwa inateremshwa chini ikiwa imeshikwa pembe zake nne. 12Ndani ya shuka hiyo kulikuwa na kila aina ya wanyama: Wanyama wenye miguu minne, wanyama watambaao na ndege wa angani. 13Akasikia sauti ikimwambia: “Petro, amka uchinje, ule!” 14Petro akajibu, “La, Bwana; mimi sijaonja kamwe chochote ambacho ni najisi au kichafu.”
15Ile sauti ikasikika tena ikimwambia: “Usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa!” 16Jambo hili lilifanyika mara tatu, kisha ile shuka ikarudishwa juu mbinguni.
17Petro alipokuwa bado anashangaa juu ya maana ya hayo maono aliyokuwa ameyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, baada ya kuigundua nyumba ya Simoni, walifika mlangoni, 18wakaita kwa sauti: “Je, kuna mgeni humu aitwaye Simoni Petro?”
19Petro alikuwa bado anajaribu kuelewa yale maono, na hapo Roho akamwambia, “Sikiliza! Kuna watu watatu hapa, wanakutafuta. 20Shuka upesi na wala usisite kwenda pamoja nao kwa maana ni mimi niliyewatuma.” 21Basi, Petro akateremka chini, akawaambia hao watu, “Mimi ndiye mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?” 22Wao wakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote, ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote ulicho nacho cha kusema.” 23Petro akawakaribisha ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule.
Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatana naye. 24Siku ya pili yake walifika Kaisarea na huko Kornelio alikuwa anawangojea pamoja na jamaa na marafiki aliokuwa amewaalika. 25Petro alipokuwa anaingia, Kornelio alitoka nje kumlaki, akapiga magoti mbele yake na kuinama chini kabisa. 26Lakini Petro alimwinua, akamwambia, “Simama, kwa maana mimi ni binadamu tu.” 27Petro aliendelea kuongea na Kornelio wakiwa wanaingia nyumbani ambamo aliwakuta watu wengi wamekusanyika. 28Petro akawaambia, “Nyinyi wenyewe mnajua kwamba Myahudi yeyote amekatazwa na sheria yake ya dini kushirikiana na watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amenijulisha nisimfikirie mtu yeyote kuwa najisi au mchafu. 29Kwa sababu hiyo, mliponiita nimekuja bila kusita. Basi, nawaulizeni: Kwa nini mmeniita?” 30Kornelio akasema, “Siku tatu zilizopita saa kama hii, saa tisa alasiri, nilikuwa nikisali chumbani mwangu. Ghafla, mtu aliyekuwa amevaa mavazi yenye kungaa alisimama mbele yangu, 31akasema: ‘Kornelio! Sala yako na sadaka zako kwa maskini zimekubaliwa na Mungu. 32Mtume mtu Yopa akamwite mtu mmoja aitwaye Simoni, kwa jina lingine Petro; yuko nyumbani kwa Simoni mtengenezaji wa ngozi karibu na bahari.’ 33Kwa hiyo nilikutumia ujumbe bila kuchelewa, nawe umefanya vyema kuja. Sasa, sisi tuko mbele ya Mungu, kusikiliza chochote ambacho Bwana amekuamuru kusema.”
Hotuba ya Petro
34Hapo Petro akaanza kusema: “Sasa nimetambua kwamba hakika Mungu hana ubaguzi. 35Mtu wa taifa lolote anayemcha Mungu na kutenda yaliyo sawa anapokelewa naye. 36Huu ndio ule ujumbe Mungu alioupeleka kwa watu wa Israeli, akitangaza Habari Njema iletayo amani kwa njia ya Yesu Kristo ambaye ni Bwana wa wote. 37Nyinyi mnajua jambo lililotukia katika nchi yote ya Wayahudi kuanzia Galilaya baada ya ule ubatizo aliohubiri Yohane. 38Mnamjua Yesu wa Nazareti na jinsi Mungu alivyomteua kwa kummiminia Roho Mtakatifu na nguvu. Mungu alikuwa pamoja naye; yeye alikwenda huko na huko akitenda mema na kuwaponya wote waliokuwa wamevamiwa na Ibilisi. 39Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyotenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu. Walimuua kwa kumtundika msalabani; 40lakini Mungu alimfufua siku ya tatu, akamfanya aonekane, 41si kwa watu wote, ila kwa wale Mungu aliokwisha wachagua wawe mashahidi wake, yaani sisi tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. 42Alituamuru kuihubiri Habari Njema kwa watu wote na kushuhudia kwamba yeye ndiye aliyeteuliwa na Mungu awe Mwamuzi wa walio hai na wafu. 43Manabii wote waliongea juu yake kwamba kila mtu atakayemwamini atasamehewa dhambi zake zote kwa jina lake.”
Kornelio na jamaa yake wanampokea Roho Mtakatifu
44Wakati Petro alipokuwa bado anasema maneno hayo, Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliokuwa wanasikiliza ujumbe huo. 45Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia kipawa cha Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia; 46maana waliwasikia wakiongea kwa lugha mbalimbali wakimtukuza Mungu. Hapo Petro akasema, 47“Watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi wenyewe tulivyompokea. Je, kuna yeyote atakayeweza kuwazuia wasibatizwe kwa maji?” 48Basi, akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Kisha wakamwomba akae nao kwa siku chache
Asante sana mkuu, ubarikiwe na bwana.
 
Back
Top Bottom