Nimeiona syllabus ya ICT huko sekondari

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
611
Reaction score
727
Ukipitia hii syllabus ni nzuri sana imejaa topics ambazo kama kweli zingefundishwa kwa vijana wetu, wengi wao wangemaliza elimu ya kidato cha nne wakiwa na maarifa ya kutosha kuweza kujitegemea na kujiajiri wenyewe.

Mfumo wetu wa elimu, unafundisha elimu ambayo ni traditional sana ,haina kabisa msaada kwa vijana kuweza kupambana na changamoto ya ajira.

Bado tunawalazimisha watoto wetu wakariri mambo ambayo hayawasaidii sana katika maisha ya kila siku .

Tuweke mkazo kwenye hii elimu ya "information and computer studies" itawasadia sana kushindana na vijana wengine huko duniani.
 
Sio seco tu hadi primary ipo,nafikiri tuwekeze ktk miundombinu sio kupiga stori za namna ya kuendesha gari kwa picha na maelezo pekee then useme umeshazalisha madereva
 
Sio seco tu hadi primary ipo,nafikiri tuwekeze ktk miundombinu sio kupiga stori za namna ya kuendesha gari kwa picha na maelezo pekee then useme umeshazalisha madereva
Mkuu, ni kweli kabisa .Taifa ambalo halitaki kuwekeza kwenye elimu ya vijana wake ,taifa hilo litakuwa ni taifa la watumwa.
 
Tatizo watawala wa giza wanajaribu kuua elimu ili watoto wa masikini wasielimike ili waendelee kuwatawala na kuwagandamiza ilihali wanaandaa watoto watoto wao kupitia shule,go beyond u will prove this!
 
I am computer science teacher holding first degree but am jobless,as if we are no longer needed in industrialization of the country .so sad
 
I am computer science teacher holding first degree but am jobless,as if we are no longer needed in industrialization of the country .so sad
Pole mkuu ,hii ni aibu sana kwa taifa .Wasomi wa kufundisha hii taaluma kumbe mpo halafu hakuna anayejali!!!!
 
Sasa watoto watasoma theory pekee maana najua kuna shule hata taa ya sola hazina
Nini kinazuia kupeleka umeme kwenye hizo shule?

Tatizo letu tunapenda kutumia pesa nyingi kwenye mambo ya hovyo ambayo hayalisadii taifa.
 
Nini kinazuia kupeleka umeme kwenye hizo shule?

Tatizo letu tunapenda kutumia pesa nyingi kwenye mambo ya hovyo ambayo hayalisadii taifa.
Tatizo baba mwenye nyumba anatuchanganya anasema elimu bure michango tuliochanga kwaajili ya ujenzi tusharudishiwa na hatuwezi changa tena
 
Madarasa hakuna, madawati bado shida, walimu na maslahi yao bado ni shida.
Maabara na maktaba ndiyo usiseme. Leo ndiyo tuweze kununua computers kwa ajili ya shule zetu za umma!!!? Thubutuu!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…