Nimeingia choo cha kike .....Part (5) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeingia choo cha kike .....Part (5)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HorsePower, Mar 6, 2012.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nilishusha pumzi na kuinyanyua simu yangu ya mkononi ili niipokee simu hii huku mapigo ya moyo yakienda mbio. Sikutamani kuongea naye kwa muda huu, maana nilijua wazi kuwa sauti yake kwangu na vilio vya malalamiko vingetosha kunifanya nibadili mawazo. Nilijiuliza kuhusu suala la kutokuipokea simu, akili yangu ilishindwa kufanya kazi kabisa. Moyoni, sikuona kama alifanya kosa kunipigia simu wakati ule, ingawa niliumia kwa kufikiria kutokuipokea. Nilijihisi nataka kufanya jambo lisilo la kibinadamu. "Niipokee?" Nilijiuliza tena. "Yeah, kupokea siyo kitu, ila nini anataka kuniambia wakati huu? Na kwanini kuanza kumnenepesha ng'ombe wa jirani hali ukijua wazi kuwa hutakunywa maziwa yake?" Swali hili lilinijia ghafla na kufanya niwe na mgongano mkubwa wa mawazo ndani ya halmashauri ya ubungo wangu.

  Nilinyanyua simu kuiweka sikioni lakini ghafla mkono wangu ukapoteza mawasiliano na akili na kujikuta nikishuhudia simu yangu ikiteleza na kuangukia ndani ya glasi ya juice na kuifanya glasi na simu vyote kwa pamoja kupasuka na kutawanyika. Nilipigwa na butwaa nisijue la kufanya. Niliwaza kwa haraka nikajua wazi kuwa Angel asingeweza kuwa na wazo tofauti na kutafsiri kuwa nilimzimia simu makusudi, sikuwa na namna yeyote ile ya kukwepa hizo lawama kwa wakati huo.

  Kesho yake asubuhi nilijidamka mapema sana na kuingia ofisini. Mawazo juu ya huyu binti yaliendelea kusumbua kichwa changu na kwa kiasi nilihisi performance ya kazi zangu ofisini ikizorota kwa kasi. Cheo changu kiliruhusu kupata simu toka ofisini. Niliwasiliana na sekretari wangu kumuona office manager anipatie handset nyingine. Wakati huo, nikiwa nimelemewa na fikra hizo, ndipo likaja wazo la kumuona rafiki yangu huyu ambaye niliwahi kusuluhisha migogoro ya ndoa yake zaidi ya mara kumi na kwa neema ya Mungu niliweza kufanikiwa kuwaweka pamoja. Leo hii, si yeye tena aliyekuwa na shida bali ni mimi. Nilisikia kitu kikinong'ona kichwani pangu kikisema "What goes around comes around!" Nilihisi kuzimia. Kwa haraka nilinyanyua receiver ya simu yangu ya mezani ofisini kwangu na kupiga namba 204 na ghalfa nilisikia sauti nzito ikiitika "Johnson Katunzi" sauti ilisikika vzr masikioni pangu. "HorsePower Francis Kufakunoga anaongea, naweza kukuona sasa hivi ofisini kwangu? " Nilimuuliza kwa sauti nzito yenye uchovu. "Mkuu, hahahaa …., nije kwa kazi za kiofisi au binafsi? Maana wewe ni mtu wa mbwembwe sana, wewe ni simba mwenda pole aliyeboboa kwenye kula vinono kisirisiri!" Aliuliza kwa utani. "Binafsi" Nilijibu kimkato. "Unamaanisha zile deal zetu?" Katunzi, naomba uje achana na maswali yasiyo na tija kwa sasa". Nilijibu kwa hasira huku nikirudisha receiver kwenye cradle yake.

  Katunzi, rafiki yangu huyu toka Bukoba tulikuwa tumeshibana naye vilivyo. Mambo mengi ya kikazi na deal binafsi za mtaani tulikuwa tukifanya naye pamoja. Ni kijana aliyeshiba elimu, na ufahamu mpana, mwenye busara na mtizamo wa kisomi, akijawa na kila namna ya majivuno na misifa kutokana na senti mbili tatu tunazobahatisha hapa ofisini. Mara kwa mara nilijikuta nikijiuliza ni kwa vipi kijana mwenye akili na ufahamu mkuu kiasi hiki anashindwa kuisimamia ndoa yake! Sikupata Jibu.

  "Mtaalamu HP, kulikoni kuitana asbh asbh hivi …!" Alianza mara tu baada ya kusukuma mlango wa ofisi yangu na kuingia. "Sina muda wa kupoteza nina jambo linanitatiza!" "Jambo gani?" aliuliza na nilichukua nafasi hii kumsimulia yaliyonikuta bila kumtaja binti huyu kuwa ni wa hapa ofisi kwetu. "Laaa, pole sana Mkuu …. Lakini umewezaje kumpenda mtu ghafla namna hiyo?" aliuliza "Sifahamu, mapenzi hayana maana , ni kama accident, yanatokea popote. Nahisi nilipata ajali ya Mapenzi" Nilijibu. "Sasa tatizo lako ni nini?" "Nampenda sana lakini moyo wangu unasita …." "Nilimjibu. Kwa nini?" "alinitamkia kuwa ana mtu na …" "Hilo ni jibu la kawaida kwa wanawake mara ya kwanza unapokutana nao … Jaribu kumfuatilia kwa kuongea naye mara ya pili …" Alinikatiza. "Hilo nalifahamu, lakini moyo wake na hisia zake wakati anaongea zilionyesha uthabiti wa kile alichoongea, nina uzoefu na hili ila kwa huyu nafikiri alikuwa ni mkweli …" Nilijibu."HP umekuwa mshauri mzuri sana hapa ofisini hata huko jamii forums, inakuwaje jambo hili dogo linataka kukushinda?" Aliuliza. "Sijakuita kwa hotuba, nahitaji ushauri" Niliunguruma kwa jazba "Jibu unalo si kakwambia ana mtu, sasa unataka nikushauri nini? Unakumbuka kilichokukuta miaka 3 iliyopita?" Niliumia roho. Nilikumbuka kisa hiki na niliwahi kukipost kwenye jamii forums (Gonga hapa). Nilihisi moyo ukilipuka na kujikuta najiinamia. Kabla sijatulia, nilisikia mlio wa simu yangu ya mezani iikiita. Nilinyanyua receiver na kukutana na sauti nyororo ya Angel toka upande wa pili ikizungumza. Nilihisi kizungu zungu!

  ******** Naenda lunch mara moja nikirudi, nawamalizia hiki kisa. Samahani kwa usumbufu *******
   
 2. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  kaka HP wahi mkuu jazi au juzi naona kikao kilikuwa kirefu mno.leo wahi mkuu.
   
 3. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Na wewe umezidi kila siku vikao ? Mnauza ngozi za binadam nini ?
   
 4. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Kumbe uliandika ukiwa hujakula bado!!
   
 5. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hehe naisubiria part 6.
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Niliaga jamani naenda kula siyo kikao .....
   
 7. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  haya mkuu . Rusha hiyo kipande iliyobakia fasta.
   
 8. Twande

  Twande JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duu ghafla nimejikuta kwenye tamthilia! Siangaliagi sababu ya kuwekwa pending namna hii na ukishaingia hutoki kama hivi! mwendelezo basi. . siku hizi hata za luningani wakikuzingua unaenda kudownload kwenye net! Horsep. . please come faster we mkaleee. .
   
 9. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  oya ndio umeingia choo cha kike kweli ????????
   
 10. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Bucho acha vituko, ulikuwa wapi siku zote?
   
 11. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  mbona nipo hapa hapa? sijaona patr 6 ? au bado upo lunch ?
   
 12. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Punguza munkari, sehemu ya sita ni ya mwisho, ni ngumu mno na imeniacha mdomo wazi mpaka leo hivi ndo maana nimewapa break ili nitakapoimalizia mchangie mawazo ya jinsi gani naweza kutoka nje ya choo cha kike, baada ya kuingia mwenyewe!
   
 13. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180

  kwi kwi kwi kwi........... angalia usije ukakimbia kama hutaki unaacha kule kwenye siasa.
   
 14. Twande

  Twande JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh! tumesubiri mpaka tumeimalizia wenyewe lol. .
   
Loading...