Nimeingia cha kike nimeuziwa kitu ambacho siyo "spray". Je, ni nini hiki?

Pole.

Hiyo ni deodorant. Inapuliziwa makwapani. Kuzuia joto na harufu ya jasho.

Siyo perfume wala siyo spray. Jijengee tabia ya kusoma maelekezo. Kwa chini kabisa imeandikwa 'soft, smooth and beautiful underarms'.
Deodorant haipulizwi.😊
 
Nilienda shop nikakutana na hii kitu nikamuuliza muuza duka ni mdogo tu (wa kiume) nazani kawekwa hapo shop kama mfanyakazi nikanogewa na ili kopo nikamuuliza kwani hii ni spray akaniambia ndio nikanusa juu ya kizibo nikaona inanukia poa bei sh elfu sita.

Jana kulikuwa na pati somewhere nikavaa gauni langu jeusi nzuri kabisa, nikasema ngoja sasa nichukue spray nipulizie kwenye gauni nikashangaa kuona sehemu zote nilizopulizia zina asili ya unga unga sasa nauliza hii ni kitu gani jamani au inatumika kwenye nini? "Nimesoma comment zenu mmeniambia ya kwapani,nimejaribu kupulizia kwapani mbona kwapa linakuwa jeupe kama powder kwaiyo nikishapuliza naacha ivyo ivyo ayo mapowder?
Bado lina thamani usijali, mpelekee fundi koroboi atakutengenezea taa nzuri sana(royal bedside lamp).
 
Wewe ni wa kiume ndio maana ukaingia cha kike,ila sasa unavaaje gauni?weka kapicha hebu tukuone ukipaka kwenye kikwapa.
 
Soma maelezo vizuri, kipindi nipo O level yalinikuta hayo, sema kwa kuwa shati lilikuwa jeupe ikawa sio kesi.
 
Back
Top Bottom