Wakuu naomba msaada wenu nimeibiwa kadi original ya gari na vibaka waliovunja kioo cha gari na kuiba pamoja na vitu vingine. ni nini nahitaji kufanya police tayari nimetoa taarifa je nahitaji kwenda TRA pia. vipi kuhusu usarama wa gari.
Kama umekwishakwenda Polisi na kupata report yao bila shaka kuna utaratibu wa kupata kadi original nyingine.
Huyo aliye na kadi yako ya awali haimsaidii kwa vile haina jina lake - sana sana ni bomu kwake kwa sababu ya kuripotiwa polisi. Haiyumkini amekwishaitupa.
nenda polic na kopy yako utapewa lost report nikama sh mia tano, kisha unakwenda trafik unapitia kama hatua 3 pale ikiwemo kukagua gari kisha unakwenda tra na gari wanakagua unalipia 10000 unapewa kadi ingine
Inasumbua kidogo maana lazima pia uende na faili lenye karatasi zote zinazohusiana na hilo gari. Ila TRA ni lazima pia uende. Kimbembe kitakuwa kama kadi hiyo haiko kwa jina lako!
Inasumbua kidogo maana lazima pia uende na faili lenye karatasi zote zinazohusiana na hilo gari. Ila TRA ni lazima pia uende. Kimbembe kitakuwa kama kadi hiyo haiko kwa jina lako!