Nimehuzunika sana, siamini kama leo hii na shahada yangu nimekuwa mtu wa kuandalia watu chai mezani

5997

JF-Expert Member
Jan 19, 2019
514
1,204
Kweli wakuu elimu bila pesa ni useless tu,

Leo hii mimi naandalia watoto wadogo wa certifacete nawaandalia chai mezani mimi? Yaani nkuchu nkunchu eti nawaletea vikombe kabisa eti karibuni chai tayari!

Mimi huyu naandaalia watu chakula mezani mimi huyu?

Nilimaliza shahada ya ualimu nikaingia JKT nako mambo yalienda kinyume. Tuliporudishwa home nikaomba kazi kampuni ya ulinzi Malipo yao upuuzi tu kazi ngumu nikapiga chini.

Sasa hivi nimepata shirika linadili na mambo ya afya kwenye refugees camp. Yaani position niliyowekwa ni kituko

Yaani mimi nawaandalia watu chai mimi? Kabisa nawaletea mezani wanywe wakishiba nikatoe vyombo!

Watu wenyewe madogo tu wa Certificate za Nursing, Pharmacy kweli kabisa jamani ndugu zangu

Dah basi bwana ngoja nikomae

Namchukia sana Rais Magufuli niseme waziwazi tu!

Any way ngoja nipumzikepo kidogo hapa nasubiri waivishe cha mchana nikawaandalie wadogo zangu chakula mezani waje wale.
 
Tatizo unaamini the universe owes you.

Yani unaamini kwa kuwa una degree basi kuna hadhi/status flani dunia inabidi ikupe.

Yaani uliaminisha ukisoma ukawa na degree dunia itakulipa kwa kukupa maisha mazuri.

The world owes no one. You take what you can get from it.

Do not ask what the world should do for you, ask what you shall do for the world. Ongeza thamani kwenye maisha ya mtu, pesa itakuja kwako kama response.

Zalisha mali, zalisha huduma. Tumia elimu yako kurenovante existing businesses na kuziongezea thamani. Tumia connections zako. Tazama kila opportunity inayopita kwako hata kama ni ndogo sana.

Punguza mzigo. Usizae. Usioe. Usiwe na mpenzi. Pambana, alone.

Mindset ya kuwa you deserve something haitakufanya upambane.
 
Sent using Jamii Forums mobile app
Humu jf Kuna watu waongo waongo sana
 
kweli wakuu elimu bila pesa ni useless tu,

Leo hii mimi naandalia watoto wadogo wa certifacete nawaandalia chai mezani mimi?
Yani nkuchu nkunchu et nawaletea vikombe kabisa eti karibuni chai tayari!

Mimi huyu naandaalia watu chakula mezani mimi huyu?

Nilimaliza shahada ya ualimu nikaingia jkt nako mambo yalienda kinyume,
Tuliporudishwa home nikaomba kazi kampuni ya ulinzi ya Gardaward.
Malipo yao upuuzi tu kazi ngumu nikapiga chini,

Saiv nimepata shirika linadili na mambo ya afya kwenye refugees camp

Yani position niliyowekwa ni kituko

Yaani mimi nawaandalia watu chai mimi?
Kabisa nawaletea mezani wanywe wakishiba nikatoe vyombo!

Watu wenyewe madogo tu wa certificate za nursing, pharmacy kweli kabisa jamani ndugu zangu

Dah basi bwana ngoja nikomae

Namchukia sana Magufuli niseme waziwazi tu!

Any way ngoja nipumzikepo kidogo hapa nasubiri waivishe cha mchana nikawaandalie wadogo zangu chakula mezani waje wale
Kaitumikie hiyo shahada ikupe mshahara....watu na ujivuni wenu
 
kwanza unatakiwa ushukuru Mkuu hapo una uhakika wa kupiga chai msosi wa mchana ukashiba, ukishashiba sasa ndio akili inatakiwa ifanye kazi, tafuta connections mpya hapo hapo hivi unaonekana una cheo kidogo watu wanakuwa wanakuchukulia huna madhara hivyo hiyo ndio njia ya kutoboa, fanya yako chinichini ukija ibuka uko juu yao, hapo tumia elimu ya kitaa maana ya shuleni ishafika mwisho jiongeze, wengine tumeamka hapa hatujui tunaelekea wapi saa hizi na tuna mavyeti kama yako lakini amini mkuu mm sijatoka home mpaka Muda huu hakini niko nyuma ya keyboard nishaingiza 70tsh ndani ya dakika 40...siendi kumtumikia kafiri yoyote, naenda zangu shamba kupanda kunde, je ningeajiriwa na mvua hii sa hizi ingekuwaje? Stress tupu, jiongeze mkuu tafuta fursa piga hela, nguv kidogo akili nyingi. usiibe tu au kutapeli, tafta laptop yenye uwezo kuwa nayo hapo Camp alaf akili ingine itakuja
 
Ushukuru Mungu wewe una hata sehemu ya kupata chochote kitu, watu wanataabika na hawajapata hata hiyo kazi unayoidharau wewe.
 
Back
Top Bottom