Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

nimekwambia naamini mungu yupo,,,ila shetani jini sijui uchawi hivyo vyote siamini hata dhambi siamini kama kuna dhambi
Ukishaamini Mungu yupo, kimsingi unakosa sababu ya kukataa kuamini uwepo wa shetani na uchawi.

Unaamini Mungu gani?
 
Usiye na akili ni wewe unayeamini UJINGA

Imani ya kichawi ni sababu kubwa iliyowarudisha nyuma watu weusi

Badala ya kuwekeza katika elimu na teknolojia wakawekeza katika Imani ya kishenzi kama unayoamini wewe Mshenzi

yaani wewe ni mjinga kabisa
 
Ukishaamini Mungu yupo, kimsingi unakosa sababu ya kukataa kuamini uwepo wa shetani na uchawi.

Unaamini Mungu gani?
Mungu alietumba sisi binadamu naamin yupo,,ila izi mambo za uchawi mashetan majini malaika siamin kama vipo
 
Hio challenge uli toa maelezo haya ?

*majina yako matatu

*majina ya baba yako na mama yako

*tarehe yako ya kuzaliwa

*picha yako

Weka haya maelezo au MPE haya maelezo mtu anayetaka kukuloga halafu uje utoe ushuhuda kama lakini utakua hai
Nipo tayari kutoa details zote hizi..nipe namba za huyo mchawi nimtumie WhatsApp
 
Usiende unless ushajipigilia FIREWALLS za kutosha
Mimi nilikuwa sinaga Habari kabisa na uchawi, lakini yalivonikuta hadi mji wangu mwenyewe nikaukimbia.

Nawaza narudi vipi kwenye boma langu
 
Kuna explanations nyingi sana.

Nitaje mbili tu kwa sasa.

1. Wewe muongo, umetunga hadithi. Vinginevyo, thibitisha. Hii ilitakiwa kuwa habari kubwa sana, lakini hatukuisikia popote.

2. Hata kama wewe si muongo, hakuna kitu chochote ulichoelezea kinachothibitisha uchawi. Kumbuka, kuona kitu ambacho hukielewi kimetokeaje hakuthibitishi kitu hicho ni uchawi. Ukikimbukia jusai huu ni uchawi kwa sababu huelewi kitu tu, huo ni uvivu wa kufikiri.
acha kubisha usichokijua mkuu, huduma za ziada wanatoa sana madaktari hasa kwenye matatizo yanayoleta utata, kama una marafiki madaktari jaribu kuwaulizia utapata jawabu.
 
mnaopinga uwepo wa uchawi mnajifurahisha tu na wala hamna lolote, majuzi tu hapa wife alikua na ujauzito wakagombezana na jirani ajili ya watoto, kilichofuata siku za kuzaa zikapitiliza tukienda hospital akipimwa hamna tatizo, mwisho dokta akanishauri yawezekana kafungwa kichawi hivo akanielekeza nikanunue dawa fulani maduka ya asili, nikaileta akakorogewa akainywa baada ya kunywa hakuchukua muda akajifungua bt cha ajabu mtoto alitoka kazingirwa mfuko wa plastic hii ilozuiwa kutumika, kama hayajakukuta ya ulimwengu chunga sana ulimi kuongea usoyajua.
Huyo daktari ni wakumfukuza kazi kabisaa...

Dawa uliotumia haihusiani kabisa na uchawi ni dawa za kawaida kabisa za mitishamba zilizotumika na mababu zetu.

Mke wangu nae alipitiliza siku za kujifungua tukaenda hospital sikutaka maneno mengi nikaacha uchawi wa kizungu ufanye kazi,akala kisu chap mtoto katoka salama kabisa na mama yake akawa vizuri kabisa,ila ninge zubaa pale ningeanza kuletewa ngonjera za kua kafungwa na mambo mengine kibao ya kipuuzi
 
Usiende unless ushajipigilia FIREWALLS za kutosha
Walinirudisha nyuma sana, kila ninachofanya hakiendi biashara zote zikafa na mwisho wakaamua waninyoe nywele, wakanyoa mara ya kwanza ikabidi niende saluni kuzikata zote maana hazikufaa Tena kuwa hivyo, zilivyoota mara ya pili wakaninyoa tena. Nikaona bora niondoke kwanza nikae mbali na hapo.
 
Walinirudisha nyuma sana, kila ninachofanya hakiendi biashara zote zikafa na mwisho wakaamua waninyoe nywele, wakanyoa mara ya kwanza ikabidi niende saluni kuzikata zote maana hazikufaa Tena kuwa hivyo, zilivyoota mara ya pili wakaninyoa tena. Nikaona bora niondoke kwanza nikae mbali na hapo.


Hatari sana hao wachawi wanadharau.
 
mkuu Hazard CFC ni ngumu kukuelewesha ukanielewa bt nakushauri jenga urafiki na watu wa afya kisha katika maongezi uwe unawaulize juu ya haya mambo, pia kitu kingine kama uliwahi shuhudia hata mazingaombwe wakati upo shule basi itatosha kujua kua uchawi upo.
 
Muwe mnasikai tu fulani karogwa, anasumbuliwa na wachawi usiku, n.k haya mambo yakiwakuta.


Nguvu za giza haziwezi kuonekana kwa macho yetu ya kawaida wala kupimwa na vifaa vya kisayansi, Ni sawa na kurekodi ndoto ya mtu uione kwenye video, haiwezekani, hata mtu akirogwa bado ipo gizani ndio mana hata ukienda hospitalini utaambiwa mashine haziwezi kugundua chanzo cha ugonjwa wako

Binafsi nilikaa nyumba moja, ikifika saa saba kuna vishindo mithiri ya mtu anakwangua ukuta kwa nondo, na hii ilikuwa kwa wapangaji wote ila ukitoka nje kucheku huko nyuma hakuna kitu.

Ni mpaka siku moja mida hio saa saba kikalia kishindo kikubwa sana paaaa! juu ya bati kila mpangaji alitoka nje ila hakukuonekana kitu, baada ya kufatilia kumbe kuna mlangaji moja alikuwa anateswa na hawa watu usiku, babu yake alikuja siku hio hapo na kuweka mtego wake.

Tukio lengine kuna mtoto moja alikuwa na miaka mitano alikuwa mzima wa afya, ghafla akawa kipofu, kiziwi na hata kushindwa kuongea, Wazazi wake wakagundua hii hali si kawaida, walimpeleka hospitali nyingi muhimbili, kcmc, n.k ilibidi apelekwe kijijini kwa mzee wake, siku hio hio walirudi na mtoto akawa hali ya kawaida kabisa

Hapo zamani sijui kama sikuhizi bado vipo, Mashuleni ya porini huko boarding visa vya wanafunzi kukutana na vibwengo ilikuwa ni kawaida sana

Mwengine nakumbuka alivimba sana miguu, walimsihi sana waende kwao kuchekiwa ila alikua haamini hvi vitu, hata miezi miwili haikufika tukamzika.
Nakubaliana na wewe kabisa.

Mimi nimeshuhudia zaidi ya mara 5 nikiwa muhusika.


Uchawi upo aisee
 
Unajuaje huu ni uchawi na hiki ni kitu ambacho sijakijua tu?

Mababu zetu walioishi miaka 140 iliyopita wangeoneshwa TV na internet leo, wangesema uchawi.

Lakini si uchawi, ni sayansi tu ambayo hawakupata kuijua.

Unahakikishaje hicho unachosema ni uchawi si kitu tofauti tu ambacho hukijui?
Uchawi siyo just supernatural power & knowledge of exceptional mysteries, pia lengo lake ni ultimate control of humanity, degradation na destruction. Hata mtu anaeenda kwa waganga kutafuta njia mkato ya utajiri, kwa nguvu za giza anaweza kupata lakini hatimaye lengo kuu ni kumwangamiza yeye na kuwaangamiza wengine kupitia kwake. Kwa hiyo, utajiri unakuwa kama chambo tu cha kunasia.
 
Back
Top Bottom