Greg50
JF-Expert Member
- Feb 11, 2014
- 1,953
- 2,431
Za asubuhi wanaJF,
Katika pitapita zangu leo nikabahatika kuskia maongezi ya kikao cha management ya moja ya biashara kubwa hapa mjini ya mhindi. Kikao hicho walikuwepo mamanager kadhaa watu wazima wa kama miaka 50 hivi, pia alikuwepo boss na mwanae wa kike (kwa muonekano ana kama miaka kati ya 18 hadi 20 hajazidi hapo).
Basi nikajua boss ndio ataongoza kikao kile lakini cha kushangaza mwanae ndie aliongoza kikao mwanzo mwisho. Tena alikua anaongea kwa confidence kubwa na mamanager wale, anauliza kwanini wafanyakazi wanachelewa kazini, mipango ikoje kwa wiki zijazo na mambo mengine nyeti. Boss aliingilia sehemu chache tuu alipoona mwanae anakwama.
Baada ya kikao nikawaza sisi wabongo tunafanyaga hivi kweli? Au ndio mtoto anajua tu wazazi wana biashara flani lakini hafahamu inaendeshwaje.