Nimegundua formula ya kufanikiwa hii hapa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,569
44,791
Wakubwa zangu shikamooni poleni na mihangaiko ya maisha natambua shida haziishi wale mliokepesha endeleeni kuvumilia mtalipwa tu endeleeni kuwakumbusha.wale mliokopa punguzeni madeni yenu hata mdomdo yataisha ukipata kiasi fulani mpelekee.

Back to the topic nataka niwape mbinu ninayotumia Mimi kufanikiwa katika aspect za kiroho,kimwili,kuridhikiwa kiuchumi n.k

Mosi, amka alfajiri kabla ya 05:30 Kisha kunywa glass moja ya maji vaa bukta yako fasta au tracksuit Anza kukimbia hapohapo huku ukiwa unasikiliza biblia hasa nyaraka za Paulo au Quran sura yoyote (audio) kupitia earphones na kuizingatia deep.

Mbili, ukirudi mazoezi let's say saa 12 na madakika Kama unatumia mjani wetu ule wa kirasi ninaruhusu vuta walau joint moja dry ukimaliza wapigie simu watu unaowapenda na kuwajali Kama vile wazazi n.k wasalimie na Kisha ingia bafuni oga maji ya baridi Kisha chemsha chai au kahawa na bites kadhaa piga tea huku ukijiandaa Na mishe mishe za siku nzima ukimaliza chai piga ugali ule Kama na maziwa mgando au mboga yoyote uliyonayo aidha matembere kwa samaki piga Kisha nenda kazini

Tatu, ukifika kazini ingia jamiiforum peruzi Kama dakika kumi hivi Kisha nenda kwenye betting site tafuta options mbili zenye odds ya 1.12 zicombine Kisha weka stake ya Kama 50000 hivi sikilizia lazima ushinde(nimeshafanyia tafiti ya kutosha na kujiridhisha hio odd Ni ya maajabu niamini).

Nne, fanya kazi Kama kawaida usivute sigara,usiangalie matako ya wasichana barabarani,usinywe pombe,mchana kula matunda tu kwa wingi na stori za Hapa na pale.

Tano, jioni ukipata muda nenda hospitali katembelee wagonjwa hasa watoto na wazee uwape matumaini na muongee maneno ya MUNGU Yale uliyoyasikia katika vitabu vitakatifu wape hata zawadi ndogo ndogo Kama vile ndizi, Sabuni n.k.

Sita, Rudi home na jioni kabla hujalala fua nguo zako hasa za ndani Na zile ulizovaa mchana Ni chache jikaze tu roho zifue mapema

Saba, lala saa nne kamili usiku usiangalie x Ni Bora simu yako uiweke chaji kwa ajili ya ratiba za kesho kwenda kuwith draw pesa yako uliko bet. Mengine nitaendelea kuwapa kwa jinsi roho atakavyo Nipa maono.

NB: So lazima ufanye yote niliyokushauri za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Sasa kuangalia MAT*KO barabarani kuna uhusiano gani na kutoboa?
 
Back
Top Bottom