enjai ya kyasha
JF-Expert Member
- Apr 6, 2017
- 3,096
- 3,651
Wakuu habari za mchana,
Kama heading inavyosomeka mpaka mda huu nimefura kwa hasira natamani kila kitu nnachokiona mbele yangu nikipasue pasue.
Stori iko hivi; Jana majira ya sa tatu nilianza kuchati na kimwana mmoja niliyekutana nae Eid akanipa namba yake. Kusema ukweli mtoto yule kajaaliwa uzuri ulitukuka ana bonge la msambwanda ni hatari yani kiujumla ni mrembo wangu wa dunia. Toka anipe namba sikuwahi kumtafuta ila ye Jana usiku kanitafuta huku akinilaumu kwanini sijamtafuta toka anipe namba, (si unajua tekniki za wakwere tukipewaga namba huwa tunakausha siku tatu alafu ndo tunaanza mashambulizi)
Sasa baada ya kujitetea kidogo tukaendelea na maongezi mtoto nikamtia vokali (vocals) akajaa mzima mzima kidume nikashangilia kwa nguvu getoni kwangu nikachukua glass ya maji nikanywa kujipongeza kwa kumsajili nyota mahiri ndani ya kikosi changu tena bila dau.
Tukaendelea na maongezi mtoto akadai anataka aje kwangu ili nimuone alivyojaaliwa manake anadai huenda siku ile sikumuona vizuri basi nikamwambia ajifeel free kwanza mi ni bachelor naishi alone, basi mtoto akapendekeza tufanye kesho asubuhi maana wazazi wake wanaamkia safari ya mbali na watarudi baada ya siku mbili, basi nikasema haina noma maana toka juzi niko off, nikamuelekeza mitaa ninayokaa akaielewa na akanisisitiza nile ugali wa maana (nikajua kesho ni Eliclasico ya hatari).
Mzee nikamwambia poa tukaishia hapo baada ya kumaliza nikaamua kulala huku nikiomba pakuche mapema. Leo nimeamka saa 12 nikapanga geto langu likapendeza nikaenda kununua vitafunwa na madikodiko kibao ili mtoto akija akute kila kitu kiko poa. Saa 2 mtoto akanipigia simu kuwa ameanza safari basi kidume nikafurahi nkaanza kuzunguka ndani huku napiga mluzi (furaha iliyoje).
Mida ikazidi kwenda nikaona mtoto hafiki nikavumilia nikasema labda njiani kuna foleni nikamtext hajibu text nikampigia akapokea akasema anakarana karibia kishuka, nikajipa hope. Ikafika sa 5 mtoto hafiki nikapiga simu akikata nikajipa hope nikajua labda yupo kwenye kelele nikasubiri wapi, nikituma text hajibu ikaenda mpaka saa 7 basi ikawa kila nikipiga simu anakata.
Mpaka mda huu hajapokea simu na sijui kinachoendelea yani mpaka naandika huu uzi nimefura kwa hasira natamani kila kilicho mbele yangu nikivunje vunje.
Yani kati ya siku ambazo demu amecheza na akili yangu ni Leo.
Naomba kuwasilisha