Nimefikiria kiapishio na usomaji

Nimefikiria kiapishio na usomaji

Wilderness Voice

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
921
Reaction score
1,652
Mhe. Rais wetu mpendwa, huyu waziri alie shindwa kuapa. Hivi ni kweli kashindwa au alipatwa na kihoro, ambacho wakati mwingine uleteleza kupatwa na wasiwasi, baridi nyepesi, ambayo umfanya mtu kutetemeka, au kupoteza nguvu ya macho kuona vizuri. Nimemwangalia kwa makini utaona anaangaika kuangalia maandishi.

Alijaribu kusogeza kiapo karibu wakati mwingine kukiweka mbali ya macho walau aone kilichoandikwa. Hali hii umpata mtu yoyote wakati wowote, ndo maana wengine hata uanguka jukwaani, au hata kushindwa kuongea na kubaki kimya.

Ombi, langu mhe, Rais. simjui huyu naibu waziri wala sina ukaribu nae, Ila naomba umpe nafasi na muda zaidi kuliko kumtumbua kwa sababu ya hali iliyompata. Hajafanya kosa la jinai, au hakuwa katika usaili. Ebu mtazame mja wako kwa mara nyingine uenda akawa wa kukufaa zaidi hapo mbeleni. Nikawaida ulimi kuteleza, hofu na kutoamini kinachotokea, huu ni udhaifu wa mwanadamu.

Hata Nabii Musa akuweza ongea uzuri, alijitetea kwa Mungu, Mungu akampa msaidizi wake, lakini Musa alifanya mengi juu ya wana wa Israel na kutokuongea kwake uzuri. Fikiria familia yake iliyokuwepo, akiapa! Mke, watoto, ndugu, jamaa na marafiki. Watoto watajisikia vipi na mke wake! Mhe. Rais unasamehe wengi, hata leo tunashukuru umesamehe wafungwa.

Mwangalie kwa jicho la pili. Namwombea masamaha huyu naibu waziri, Francis. Nilishawahi fungisha ndoa za kiserikali; Bwana au Bibi harusi ufikia wakati wakatetemeka na kushindwa kuapa, si ndoa za kiserikali tu hata makanisani, hutokea mmoja wapo kashindwa, je tumnyang'anye mke au mme kisa kashindwa kuapa?

Je, Kushindwa kwake kuapa kutaaminisha kwamba bibi harusi au bwana harusi hatoweza majukumu ya familia? Inahitaji Tafakuri! Ikiandikwa hivi watu upenda kudhania ni mhusika ndo kaandika au kutumia mtu wanae fahamiana. La hasha! Simjui ni mara ya kwanza kumsikia, ila nilikuwa nafatilia viapo vya mawaziri na manaibu wao. Kwa sasa nipo nje ya Tanzania. Mungu akubariki Mhe, Rais na tunakuombea kwa mazuri yote ufanyayo.

Naomba kuwasilisha!
 
Mhe. Rais wetu mpendwa, huyu waziri alie shindwa kuapa. Hivi ni kweli kashindwa au alipatwa na kihoro, ambacho wakati mwingine uleteleza kupatwa na wasiwasi, baridi nyepesi, ambayo umfanya mtu kutetemeka, au kupoteza nguvu ya macho kuona vizuri. Nimemwangalia kwa makini utaona anaangaika kuangalia maandishi..
Rais magufuli hajabadilika,ni huzuni kubwa!!Uamuzi umekuwa wa haraka mno kwa huyu bwana. Kama kawaida yetu hapa JF tunatumia fursa kukumbusha na katika hili JPM akumbuke Kikwete alianguka jukwaani (Ex soldier aliyepitia kozi zote ndogo na kubwa) lakini alikuja kuwa Rais kwa miaka kumi (CCM hawakuondoa uteuzi wake kwa sabau anadondoka "ovyo"jukwaani).Hard science ya JPM inamfanya akose kitu fulani cha muhimu kutoka katika social sciences.
 
Mhe. Rais wetu mpendwa, huyu waziri alie shindwa kuapa. Hivi ni kweli kashindwa au alipatwa na kihoro, ambacho wakati mwingine uleteleza kupatwa na wasiwasi, baridi nyepesi, ambayo umfanya mtu kutetemeka, au kupoteza nguvu ya macho kuona vizuri. Nimemwangalia kwa makini utaona anaangaika kuangalia maandishi...
Kwa nini umeandika 'mja wako'? Unamimilikisha binadamu kiumbe mwenziwe? Mja huwa ni muumba mbingu na ardhi peke yake.
 
Kuna mtu ana PHD lakini alishindwa kutamka "Entrepreneurship"akaishia kusingizia eti oooh!si lazima msomi kujua Kiingereza. Sa mbona huyu kashindwa kuapa kutokana na hofu anafukuzwa? Uonevu tu![emoji15][emoji15][emoji15]
 
Mhe. Rais wetu mpendwa, huyu waziri alie shindwa kuapa. Hivi ni kweli kashindwa au alipatwa na kihoro, ambacho wakati mwingine uleteleza kupatwa na wasiwasi, baridi nyepesi, ambayo umfanya mtu kutetemeka, au kupoteza nguvu ya macho kuona vizuri. Nimemwangalia kwa makini utaona anaangaika kuangalia maandishi...
Peleka uchafu wako huko kwenu. Atatekelezaje majukumu yake kama hata kiapo kinampa kiwewe. Akienda nje ya nchi ataweza kuzungumza mbele wa mawaziri wengine?
 
Mleta mada hata mimi nimekumbwa na hisia kama zako, kupata kitetemeshi au ganzi ya kutamka jambo huwa ni jambo la kawaida sana na hutokea ghafla pasipo muhusika kutarajia.

Mh Rais ampe nafasi tu, asiteue mwingne kwasababu kitendo cha kusema kuwa watachunguza elimu yake na mengineyo maana yake hapo ni kuiaibisha na kuitilia mashaka mamlaka yake ya uteuzi inayohusika ktk kuwafanyia vetting wahusika ktk nafasi mbalimbali wanazoteuliwa
 
Mhe. Rais wetu mpendwa, huyu waziri alie shindwa kuapa. Hivi ni kweli kashindwa au alipatwa na kihoro, ambacho wakati mwingine uleteleza kupatwa na wasiwasi, baridi nyepesi, ambayo umfanya mtu kutetemeka, au kupoteza nguvu ya macho kuona vizuri. Nimemwangalia kwa makini utaona anaangaika kuangalia maandishi...
Kwasasa nipo nje ya Tanzania.

Asante kwa andiko zuri.

Kama Bwana angehesabu maovu na weakness zetu, nani angesimama...
 
Mhe. Rais wetu mpendwa, huyu waziri alie shindwa kuapa. Hivi ni kweli kashindwa au alipatwa na kihoro, ambacho wakati mwingine uleteleza kupatwa na wasiwasi, baridi nyepesi, ambayo umfanya mtu kutetemeka, au kupoteza nguvu ya macho kuona vizuri. Nimemwangalia kwa makini utaona anaangaika kuangalia maandishi...
Inawezekana jamaa ana matatizo ya macho anahitaji miwani.

Hakusoma kwa uoga, inaonekana alikuwa na tabu kusoma.

Ila ilibidi atambue hilo ajiandae hata kwa kukariri kiapo.

Kiapo kinajulikana, si kirefu, angekariri tu.

Halafu kama ana matatizo ya macho apate wataalamu wampe miwani itakayomfaa.

Rais John Kennedy wa Marekani alikuwa anataka kumteua Robert McNamara kuwa Waziri wa Ulinzi. Akaambiwa McNamara ana matatizo ya kusikia. Kennedy akasema tutampa kifaa cha kumsaidia kusikia (hearing aid).
 
Haya tuliyatarajia, wizi Wa kura halafu unaapa kwa vitabu vitakatifu. Kufuru itawapata tu
 
Back
Top Bottom