Nimefeli form four, nisaidieni nisifeli maisha

genious wa kijiji

Senior Member
May 1, 2014
173
249
wakuu!

nimehitimu form four mwaka jana.
matokeo yangu sio mazuri kwani nilipata four ya 32.
kiswahili: C
english:C
biology:D
masomo mengine nilifeli.
kwa sasa nafikiria kutafuta chuo nikasome ualimu wa shule ya msingi maana huko kunaweza kuwa na unafuu wa ajira ukilinganisha na kozi zingine.

mimi ni mtoto wa kike na natoka familia duni hivyo naomba mnisaidie kupata majawabu ya maswali haya.

1. je naweza kupata admission kwenye college yeyote kusomea ualimu wa shule ya msingi kwa ufaulu wangu?

2. je ada za masomo kwa college za serikali ni kiasi gani kwa ualimu? (average)

3.je applications zinaanza/ zilianza lini kwa wahitimu wa form four 2017?

4. je ni vyuo gani vya ualimu vya serikali naweza kupata kwa mikoa ya singida na dodoma? mimi ni mkazi wa dodoma.

naomba mnisaidie wakuu. nipo katika wakati mgumu sana. nimefeli form four na naona nakaribia kufeli maisha. kujiajiri siwezi kama ambavyo wengi wetu hatuwezi kutokana na ugumu wa maisha.

****huyo ni binti aliyemaliza form four, kaniomba nimshauri ila nimeona ni vema mnisaidie ushauri******
 
Kama una D nyingine mbili kuchanganya na hizo C (yaani pass nne, maana D ni pass) unaweza kusoma certificate kwenye vyuo vya elimu ya juu mfano CBE, IFM, Mwalimu Nyerere na Dar es salaam Institute of Accountancy. Umejitahidi hujapata bashite.
 
Fanya mpango wa kujiajiri tu hilo wazo la kusoma piga chini hiyo pesa ya ada anzia mtaji
 
ndio waalimu wa dodoma wamewafundisha kuwa ukiwa na c mbili na d moja unakuwa na four ya 32
au tuachane na waalimu umeamua kutudanganya kuwa mtu ukiwa na c mbili na d moja ndio four ya 32 ukweli ni kuwa four ya 32 masomo matatu uliyoorodhesha hapo juu,umepata D na mengne umepata F(in gwajima voice) ningekusaidia lakini jifunze kusema ukweli
 
Nenda veta usomee ufundi stadi...hautajuta mfano unaweza kusomea ufundi umeme, bomba, kupaka rangi kwenye nyumba, ufundi simu au umeme kwenye magari.
 
Kama una D nyingine mbili kuchanganya na hizo C (yaani pass nne, maana D ni pass) unaweza kusoma certificate kwenye vyuo vya elimu ya juu mfano CBE, IFM, Mwalimu Nyerere na Dar es salaam Institute of Accountancy. Umejitahidi hujapata bashite.

Duhhhhh!!!!!!!! mbavu zanguuu
 
Ahaaa pole mdogo wangu unamzidi bashite, ikishindikana kuwa fundi cherehani utojutia ugumu wa maisha
 
Pole sana. Mwenzio alifeli darasa la nne akakomaa, mara darasa la saba nalo kafeli. Akazidi kukomaa kwa kuingia sekondari private na kuishia kupata F F F zote hata ya Kiswahili na Siasa. Na bado hakukata tamaa lakini akaamua kubadilisha strategies kwa kuja na jina tofauti ...angalia, mbinu hiyo imemfanya kuwa kiongozi mkuu kabisa Tanzania a.k.a waziri asiye na wizara maalumu!
nakushauri na wewe usichoke kufikiri, soma huwezi kujua miaka ijayo mimi naweza nikawa ndiye amiri jeshi mdogo!
 
Pole dogo.
Umefail still unaendelea kujiita Genious.
Achana na hilo jina. Na hayo matokeo ya biology ni alama gan hiyo?
 
Sijui mfumo gani umetumika. Ila kwa matokeo ya C 2 na D 1 ulistahili kupata four ya thelathini,
 
ndio waalimu wa dodoma wamewafundisha kuwa ukiwa na c mbili na d moja unakuwa na four ya 32
au tuachane na waalimu umeamua kutudanganya kuwa mtu ukiwa na c mbili na d moja ndio four ya 32 ukweli ni kuwa four ya 32 masomo matatu uliyoorodhesha hapo juu,umepata D na mengne umepata F(in gwajima voice) ningekusaidia lakini jifunze kusema ukweli
Bro mimi nna
Civics-D
Biology-D
Math-F
Kiswahili-D
Geography-F
History-D
English-C

UNANISHAURI NIKASOMEE NINI...?
 
Back
Top Bottom