kabiriga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 1,163
- 1,214
Ni juzi tu nilipokea simu kwa mtu nisie mjua,kwa maelezo kuwa nimemsahau na kumtelekeza wakati najua ana mtoto wangu,nilijaribu kujitetea lakini hakunipa nafasi bali aliongea mfululizo huku na lawama kibao,kisha simu ikakatika.Nilitafakali sana kisha nikaamua kumpigia jana,alipo pokea simu akanza kulalamika tena,nikamuuliza unajua unaongea na nani? akasema umeanza mambo yako yaani mimi sikujui wewe, si unaitwa fulani(alitaja jina,si jina langu) kisha nikamwambia dada sikiliza naona umekosea namba mimi si huyo umtajae na mimi sikujui wewe,akasema nawajua nyie wanaume mkisha aribu mnaanza kukataa sasa ukae ukijua huyu mtoto siwezi kumtunza peke yangu inakubidi uje umchukue sasa ni zamu yako kulea na usinitanie kabisa vinginevyo nitakavyofanya usinilaumu.Nili msihi sana kuelewa kuwa anaeongea nae sie mhusika akasema wewe ndie na namba hii amenipa mama yako,kisha nikamuomba ombi lilelile kuwa umekosea namba na jaribu kurudi huko ulikochukua namba,akasema uwezi kunifundisha la kufanya nimekwambia uje umchukue mwanao.sasa sijui nifanye nini kwani isije ikawa antakakufanya jambo baya(kujidhuru au kumdhuru mtoto) na ikaonekana mtu wa mwisho kuongea nae kwenye simu yake ni mimi kisha nikawa kwenye hatia.ushauri wenu jamani