Nimeelewa kwanini Kagame alitudharau

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,266
2,870
Paul Kagame ni Rais ambaye kwa miaka 10 iliyopita alitudharau sana, nimewahi kumchukia kwa kufikia hatua kumtishia maisha aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Nchi kipindi hicho. Akijinadi kuwa angeweza kumgonga anytime.

Sikupenda jambo lile hasa kwa kuwa Cheo cha Urais ni nembo ya Taifa hata kama itatokea Jiwe likawa Rais wa Tanzania basi hiyo ni nembo yetu litakapokuwepo jiwe hili liheshimiwe.

Huwa siruhusu mtu mwingine amponde kiongozi wa nchi yangu zaidi yangu mimi mwenyewe ambaye nitamkosoa lakini isifikie hatua mtu akamchimba mkwara.

Sasa nimeelewa, Kagame ni kiongozi shupavu, mwenye akili ,dikteta kiasi fulani, mwenye kuipenda nchi yake, asiyejilimbikizia mali, mwenye nidhamu na serious. Hivyo hutaka kufanya kazi na watu wa namna hiyo. Kwa maneno haya hapa chini anamaanisha miaka 10 iliyopita Tanzania ilikuwa na ombwe la uongozi inasemekena kuna wakati hata Kagame alitamani aje aombe kujitolea kuwa Rais nchini yaani awe volunteer na hili ndilo lililo leta ukakasi sana kwa Utawala uliopita. Soma maneno haya aliyoyasema between the lines.

"You must know, first of all, that you are in your brother’s place.Since you were elected, you presence has been refreshing. Your words & deeds reflect our vision. Your stance against corruption is very refreshing. We are committed to working with partners who feel we have to raise our level of dignity because that is what we deserve.

We thank you for being with us tonight, the same night,22 years ago when what is not easy to describe happened to our nation. The effects of what happened 22 years ago still ring bells in our mind,hearts and our homes.

What happened here 22 years ago will never happen again. Rwandans who rebuilt their lives are as committed as I am to make sure it never happens again.
- President Kagame speaks at the official dinner hosted in honour of President Magufuli.
 
Mbona aliyoyasema ni kawaida sana kusikika katika dhifa za marais. Pamoja na uzuri wake ana mapungufu hasa linapokuja suala la DRC. Ame-destabilize sana eastern Congo. M23.
 
Mzee Mwanakijiji umekamata kwenyewe.Nadhani Mh.km amerudi ktk hii safu basi hii aiwekee note,ni extract muhimu.Serikali hadi leo bado wapo wanjisuasua kwa copywrites za wasanii tuu hawajui hata ktk patent kunaweza watoa wabongo kibao,kwani mtu km analowazo jipya na zuri akilewekewa patent analiuza au kukopea nalo na kuweza fanya kazi kwa kipindi fulani ambacho atakuwa amerudisha gharama zake na ndio sasa fungulia mbwa ianze ili kuleta upinzani.
Lakini leo hii hata jamaa wa chai maharage enzi zile,au chakula cha waathirika Arusha,Au mchoraji wa leo anaweza fikisha proposal yake bank leo ya kuomba mkopo kwa ajili ya wazo lake kesho akakuta hilo wazo limeshafanyiwa kazi na tajiri moja nguvu za kutisha.
Mzee mwanakijiji hii itapiga bao si utalii peke yake bali kila sector.Patakuwepo mfumuko wa mawazo na ubunifu wa kila nyanja ambao utaleta mafanikio makubwa.Mtaji wa kila raia utakuwa akili yake,na mafanikio ya makampuni yatakuwa mitaji yao.
Nimejikuta nacheka tu na nikamkumbuka ghafla mbulumundu Chilisosi
 
Lengo la lugha ni kufikisha ujumbe. Watanzania tumwunge mkono Rais wetu,tusimkatishe tamaa. Kiingereza si lugha yetu,ni ya wakoloni. Magu ongea hicho kikoloni inapobidi,mradi ujumbe ufike.
 
mpaka hapo sijaona bad comment ya Kagame dhidi ya mkwere.labda kama hujamaliza kutupia speech nzima!
 
Mimi sioni sifa mnazompa
km M23 tulieachapa ili kumpunguza kibri
mpaka wakadai Mke wa Mkulu no kabila yao
huyu mtu hamuwezi mfananisha na Kikwete au Magufuli
huwezi nga'ng'anoa madaraka mwisho ni vipindi viwili
 
Lengo la lugha ni kufikisha ujumbe. Watanzania tumwunge mkono Rais wetu,tusimkatishe tamaa. Kiingereza si lugha yetu,ni ya wakoloni. Magu ongea hicho kikoloni inapobidi,mradi ujumbe ufike.
Ni VILAZA pekee wana jali hilo
Ajabu ukileta mada humu ya kiingereza wanapita wima
 
WANYARWANDA BWANA MNASIFIA NA KITU AMBACHO HAKIPO: TATIZO MMEJIACHIA SANA HAPA TZ
 
Wajuzi , mambo vipi itakuwa mahusiano yetu na Congo baada kuonekana tunawakumbatia Rwanda na wale M23 Congo wanadai ni Rwanda? Wana Diplomasia waje hapa!!
 
Sasa ni kitu gani alichoongea hapo ambacho wewe umeona ni point sana mpaka umuone ana "akili sana!?"Au wewe ni wale mazwazwa ambao kwasababu tu alikuwa anaongea hiyo broken yake na magufuli,basi imekuwa ni point!
 
Back
Top Bottom