nimechoka na huyu mume msaada

Davina mama why are you behaving like that my dear? Kumbe hana tatizo kama anacare kwa mahitaji yote ya family isipokuwa ni kujisahau tu kwenye simu kwa ubusy wa kazi. Nahisi wewe uliolewa bado mdogo sana hivyo hujakua. Sababu unazonipa hapa ni za kitoto sana kwa wewe kutaka kufikia hayo maamuzi.

Tulia mtoto mzuri mumeo anakupenda sana na anamenyeka kwaajili yako na watoto. Wanaume kukumendea hilo lisikudanganye coz wao huwa na hurka ya kutamano. Kumbuka kutongozwa siyo uzuri au siyo ndo kupendwa coz hata vichaa au walemavu hutongozwa na kuzalishwa tena na watu wa maana huwezi amini.

Kunamigubeli humu haijawahi bahatika kuolewa itakushauri uachane na mumeo mzuri na wamaana, au itakwambia utafute wa pembeni weee koma kabisa mamangu dunia hii imeharibika vibaya sana, utakuja kufa ungali mbichiiii..kuna watu wanapesa na mvuto na miili safi ilojengeka, wenye magari, elimu na kazi nzuri but wanaishi kwa vidonge na wanapendeza sana kwa macho. Kuwa mwangalifu mama kondom siyo ya kuiamini, we hayaaaa weeee utajakumbuka haya maneno nikufundayo mama.

Tulia tuliii ktk ndoa yako mtoto mzurii mumeo hana shida ila wewe ni wivu unaota unaibiwa kumbe siyo. Kumbuka wakupendao hukwambia ikweli daima, we have enough experience ktk ndoa thats why twakuonya mama. Usiache kuomba daima Mungu akupe amani.

What a lovely advise! I really like this, thanks!
 
kwani manka na davina ni mtu mmoja? Kwani sasa watuchanganya. Au manka nawe umeguswa?

hiyo ndiyo JF bwana, the home of great thinkers... kuna wengine wanabadilika jinsia humu kila wakati kulingana na post iliyopo mezani - sijui ni transgender/ transsexual!
 
kama hapo juu ni sawa, basi wewe una lako jambo na si swala la mawasiliano tu. wewe una motives zingine zaidi ya mawasiliano na ndiyo maana kuna sehemu umesema wapo wengi wanaume wanakutaka.

Ushauri wangu; ithamini ndoa yako na ipende familia yako. Achana na hao wanaokudanganya, kwani I can assure you that siku ukimwacha mmeo na kuhamia kwake huyo anayekudanganya kwasasa, ndipo utakapojua kwamba kuna wanaume wengi sana wanapenda kuwa na wake za watu na sababu kuu ni kuhusu suala la gharama. Lkn, siku ukimwambia nimeachana na mme wangu na mimi nitakuwa wako jumla kuanzia leo ndipo utakapojua ni kwanini kuna wanaume wanapenda wake za watu.

Achana na uongo wanaokuambia ohooo mimi nakupenda na nipo tayari kukuoa kama ukimwacha mmeo, sasa jaribu uone matokeo yake. Yaani miaka 7 kwenye ndoa, then leo simu inataka kuvunja ndoa? je mna watoto? hivi unapata hata muda wa kuweza kufikiria role anayoplay mmeo kwenye nyumba?

Mimi nahisi huyo mwizi anakuchanganya kwa mapenzi motomoto na labda ni vitu ambavyo unavimisi kutoka kwa mmeo na sasa unaona giza tu mbele kwa udanganyifu unaofanya dhidi ya mmeo. Davina, si ajabu kwasasa hao wanaume kibao wanaokutokea wanafanya hivyo kwasababu umependeza sasa na hii ni kutokana na care anayotoa mmeo na si ajabu hata sehemu ya hizo care ndiyo unatumia kutimiza tamaa zako. Hii inakuwa na negative impacts kwenye ndoa.

Tafadhali achana na mawazo hayo ya kuona unatongozwa na wengi na hivyo kumwona mmeo hafai na UMPENDE MMEO NA FAMILIA YAKO. Ebu ishindi hiyo roho chafu inayotaka kuvuruga ndoa yako na future yako.
RDI.

umeeleza vyema sana mkuu; tatizo ni kwamba baadhi ya hawa dada zetu huwa hawajifunzi mpaka yawakute
 
Mmh pole mama, ndoa znakua ndoa, badae ndoano mwisho inarud kuwa ndoa.vumilia
 
mh haya JF haiishi mambo na vijambo!wapo wanaopendana humuhumu,wapo wanaoachana,wapo wanaotafuta wapenzi,bila kusahau wanaume wapigaji wanaotaka kulelewa yan ilimradi jamvi liko bize.kaaaaaaaaaaaaaaaaazi kweli kweli.
 
anatafuta huruma na visisngizio vya kukimbilia kwa hiyo mijamaa

yaani hiyo ya kuzima simu ilikuwa ni kisingizio tu................... hapo cha kufanya ni kumwambia tu nimekuchoka nataka kwenda kujaribu kuishi na mwingine
 
tatizo hapo ni kuvumilia kwa tabia ya mumeo ya kutotulia,ulijipa moyo kwa kuwa ni mwanamke mpambanaji halitakusumbua,ukweli limekusumbua na maumivu yake yamekuwa yakiaccumulate to the point hayavumiliki anymore....mwaya kama yamekushinda bwaga manyanga life is too short!!!
 
Davina dear, mumeo ndivyo alivyo; ukianza kuassume vitu utaviona hata kama havipo. Inaonekana una freetime ya kuzidi kiasi kwamba unatumia muda mwingi kufikiria mumeo atakuwa anafanya nini na nani.

Ushauri wangu, tafuta kitu cha kuoccupy muda wako ili atleast nawe uwe busy japo kidogo!

Huwezi kumbadilisha; so stop trying. Ukiamua kumuacha na waweza kumpata anayeongea na wewe while yuko kwenye kifua cha mwanamke mwingine n trust me wa hivyo ni wengi (I am speaking from experience ya kuwa na mume wa mtu, na kuibiwa vile vile).

yaani umeongea points tupu. Inabidi a-print kabisa hii post aiweke kwenye pochi
 
Back
Top Bottom