Nimebaki na maswali tu

Nimebaki na maswali tu

Monda kubwa

Senior Member
Joined
Jun 20, 2019
Posts
121
Reaction score
157
Usiku wa leo ni mrefu sana. Kuna dada mmoja nilianza kumfukuzia tukazoeana ila sijamgegeda kwa sababu naona kama haeleweki.

Sasa yeye ana rafiki yake wa karibu sana. Huyo rafiki yake ana mtu wake ambaye ni mume wa mtu na namfahamu. Huyo rafiki yake alipata shida kidogo maana Alifikia kwa ndugu lakini wakawa wamepishana kidogo akawakimbia ndugu.

Sasa huyo ninayemfukuzia akaniandikia message usiku wa leo kuwa wana shida mwenzake hana sehemu ya kulala niwasaidie.

Nina hela ila sikutaka kuwapa. Nikamwambia njooni mlale kitandani mimi nitalala kwenye sofa maana nakaa mwenyewe. Akaniambia rafiki yake atatangulia halafu yeye atafata baadae. Nikamwambia poa.

Rafiki yake akaja nikamkaribisha tukawa tunacheki movie tu. Nikamuuliza mbona mwenzako haji? Akaniambia simu yake imezima kwa hio atalala kule kwa baba yake mdogo.

Daaah, nimebaki na maswali tu kichwani. Mpango wao ni nini? Wanawaza nini?

Nimelala hapa lakini nawaza sana.
 
Akili kumkichwa!
Wajinga ndio waliwao
 
Mjomba, hapo umeandaliwa mazingira ya kubambikiwa mimba ya mume wa mtu kuwa yako. Sasa wewe endekeza zinaa tu ubebeshwe mimba. Achana na huyo mwanamke wewe jilalie zako. Monda kubwa,
 
Mkuu wako wapi???nina room hapa ipo tu haina mtu niwasaidie
 
Hapo kuna pande mbili za shilingi. Kuna kichwa na mwenge!?

Fikiria kwa kina zaidi. Usiendeshwe na kichwa cha chini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom