Nimeathirika

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,431
Ndugu wana Jamii forums,
natangaza rasmi mbele ya kadamnasi hili kuwa mimi ni muathirika.
Nikiamka asubuhi sifanyi kitu kingine zaidi ya kuingia Jamii,
Kazi haziendi bila ka window ka jamii kuwa minimized mara maximazed.
akili yangu inawaza Jamii Forums.
Kweli mimi ni muathirika na hii kitu imemeza kabisa ufahamu wangu.
Je kuathirika huku ni kwangu mie tu au na wenzangu wapo?
 
tupo wengi sana... kiasi naogopa sasa kazi itakuaje
 
duh yani nimestuka maana wikend tulikuwa wote nikajua kama umepata huohuo duh kale katoto sijui kangebaki na nani?labda jenny
 
hapo tupo wengi!
lakini IT'S OKAY WITH ME
 
tuko wengi mie pia nimeathirika na ka JF ugonjwa.
 
ugonjwa huu una tiba kweli jamani??? am kinda scared as am sailing in the very same boat ya VJF!!!!
 
pole sana mkuu, tatizo la huu ugonjwa hauna ARVs ungetumia labda!
 
hahahaha yaani mie nilivyoona heading nikajua umeathirika na haya maradhi yetu
hehehehe kuendelea kusoma kumbe ni kale ka ugonjwa ka wote
 
hahahaha yaani mie nilivyoona heading nikajua umeathirika na haya maradhi yetu
hehehehe kuendelea kusoma kumbe ni kale ka ugonjwa ka wote

afu kifo cha wengi harusi !!!!!
 
huo ugonjwa unanitesa pia, siku hizi naona nimekua najitahidi kumeza ARV za facebook lakini wapi.
 
..Mkuu haka kaugonjwa nadhani bora yako wewe...Mimi nikiwa kazini ndio kabisaaaa Jf mpaka basi, nikiwa nyumbani ndio yale yale week end busy kwenye blackberry....! sijui kama kuna dawa hapa! maana akili haikubali eti siku ipite sijachungulia jf.
 
Mh, mimi nimewaambukiza hata jamaa wawili hapa ofisini!

Afadhali ya wewe umeambukiza wawili, Miye nimeambukiza ofisi nzima , mpaka za Jirani, nimesambaza mpaka ofisi za mbali. Sasa ni saa nne kasoro nimefika ofisini saa 2 kamili bado niko JF tu.
 
Poleni kwa kuathirika, mi waaala!

hahaaa hilooo!!! hata baa we si unasahau serengati unanogewa na masredi....mara kibao tu usitake nimwage siri hapa!!!!! mule mule tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…