Nimeanza Mwaka kwa Mazoezi

Duuh kweli tuko tofauti, basi mi nikipiga zoezi ndo appetite ya kumwaga, sema huwa najicontrol kula, vinginevyo ndo nazidi kuumuka
Hujanisoma vizuri au?! Hata mimi nikifanya mazoezi ndio nakula sana kwahio mwili unaongezeka vizuri, nisipofanya mazoezi naweza kula mara moja kwa siku tu.
 
Hongera. Mimi nimeanza kwa diet ila mambo ni tight. Nikisikia harufu ya wali nachanganyikiwa kabisa kwa kuutamani
Diet muhimu, maanake unaweza kuwa unafanya kazi bure.
 
Nilianza jogging,planking na push ups lakini nimejikuta nimeacha bila sababu ya msingi.
 
Safi sana,
Ongezea kuruka kamba mkuu. Kwa kweli mazoezi ni dawa tosha, sikumbuki mara ya mwisho kuumwa ni lini.
Mtu unatakiwa ufanye zoezi na uwe na nidhamu na maisha, yaani anasa weka kando.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…