Ni baada ya kuona dalili kuwa muda wa kuoa umekaribia, ni lazima kutoa vitu visivyohitajika kwa mwenzangu au vile vitu vyenye kukera pale mtarajiwa atakapoingia ndani, hivyo basi nimeanza kupekua kila kona na kila kichochoro cha chumba changu ili kusafisha kabisa mabaki yasiyotakiwa, mabaki hayo ni kama yafuatayo, nguo zilizosahaulika na wanawake wengine enzi hizo, picha zote za wanawake waliopita, kadi za mapenzi nilizopokea kwa kipindi chote na vijizawadi vyote toka kwa wanawake.