Nimeanza kuishi kwa woga!

Nimeanza kuishi kwa woga!

bendaki

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
952
Reaction score
346
Vita huletwa na watawala. Vita huja wakati wachache wawaonapo wengi kuwa ni majuha na watakavyo ndivyo na sivinginevyo. Hutokea pale vyombo vya dola hudanganyika kwa matakwa ya wachache na kutii hata kuua ili wachache watawale watakavyo. Hutokea pale wengi huanza kuwa na uelewa wa kuwa wamekuwa wanadanganywa na vitu visivyo na thamani.

Hutokea pale ardhi inapokuwa haikidhi haja tena aidha kwa kukosekana au mazao ya kilimo kutokithi matakwa. Hutokea pale ajira hazipo na zilizopo wanapeana wachache. Hutokea pale viongozi kuwa na mikakati ya wao na wanaowataka kuendelea kuongoza wakati walio wengi kuwa wamewachoka. Hutokea wakati rasilimali za nchi zinapomilikiwa na wachache kiujanjaujanja.

Hutokea pindi wanafanikiwa kiujanjaujanja kuanza kuwakejeli watawaliwa kwa kutumia matusi, mipasho, nk. Hutokea pindi ahadi zinapokuwa hazitimizwi. Hutokea pindi rushwa, ufisadi, ubadhirifu na serikali kutokuwa na bajeti inayotekelezeka. Hutokea pindi serikali inapo wabebesha watu wake deni kubwa na viongozi kuishi kwa anasa.
 
Mkuu naona umepata maono labda njoo na alternative maana tunaelekea kubaya wao wanaona vyombo vya dola ndivyo vya kuvitegemea kukandamiza maamuzi ya umma.
 
Unabii huu unainyemelea TZ.
Ee Mungu pishia mbali janga hili kwa kuturudisha kwenye mstari.
Amen.
 
Mkuu naona umepata maono labda njoo na alternative maana tunaelekea kubaya wao wanaona vyombo vya dola ndivyo vya kuvitegemea kukandamiza maamuzi ya umma.

sometimes MUNGU hupanga haya makusudi .
 
Vita huletwa na watawala. Vita huja wakati wachache wawaonapo wengi kuwa ni majuha na watakavyo ndivyo na sivinginevyo. Hutokea pale vyombo vya dola hudanganyika kwa matakwa ya wachache na kutii hata kuua ili wachache watawale watakavyo. Hutokea pale wengi huanza kuwa na uelewa wa kuwa wamekuwa wanadanganywa na vitu visivyo na thamani.

Hutokea pale ardhi inapokuwa haikidhi haja tena aidha kwa kukosekana au mazao ya kilimo kutokithi matakwa. Hutokea pale ajira hazipo na zilizopo wanapeana wachache. Hutokea pale viongozi kuwa na mikakati ya wao na wanaowataka kuendelea kuongoza wakati walio wengi kuwa wamewachoka. Hutokea wakati rasilimali za nchi zinapomilikiwa na wachache kiujanjaujanja.

Hutokea pindi wanafanikiwa kiujanjaujanja kuanza kuwakejeli watawaliwa kwa kutumia matusi, mipasho, nk. Hutokea pindi ahadi zinapokuwa hazitimizwi. Hutokea pindi rushwa, ufisadi, ubadhirifu na serikali kutokuwa na bajeti inayotekelezeka. Hutokea pindi serikali inapo wabebesha watu wake deni kubwa na viongozi kuishi kwa anasa.

Kayamgo hayo ni maono halisi ambayo Mungu amesema nawe! Ni vigumu mno kwa utawala dhalimu kuyaona hayo! Utawala dhalimu cku zote hutengeneza manabii wa uongo! Hausikilizi unabii wa kutoka kwa Muumba wetu! Ukiona mawingu wenyewe hutoa nguo za kuanika ukidhani jua laja! Ukiona Moshi unafuka unatafuta nyasi kufunika Moshi huo! Utawala dhalimu cku zote unaweka pamba masikioni! Wakati wewe unafumba macho kuogopa anguko lijalo ama maafa yajayo viongozi dhalimu wanakuwa name sherehe kila kukicha!
 
Huu ni ukweli, tena tena ni ukweli mchungu kwa watawala, anguko laja sio muda mrefu.
 
Mungu angekuwa binadamu angeua wabunge wooooote wa ccm
 
Kama una ogopa vita, tena vita ya ukombozi kwa kweli unatakiwa kuwa kaburini, jifunze kwa wa libya, misri, ukraine etc walivyo jikomboa
Hata mafundisho ya vitabu vitakatifu yanakataza woga!
 
Watala rudisheni.mali za umma mlizojilimbikizia mambo yanaenda kombo hapa nchini,wananchi imani kwenu inapungua na tunapo hoji ni kutoa kucha.na meno watu nasi tunaweza kujibu
 
Wewe vp unaweza nn?
 
Mungu angekuwa binadamu angeua wabunge wooooote wa ccm

Hamna mi nafikiri angeyageuza mang'ombe ili majike tuanze na sisi kuyakamua maziwa walaau tujenge afya na midume ikalimishwe mashambani ili kufidia kodi zetu walau hata kidogo.
 
Back
Top Bottom