Zinduna
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 2,378
- 3,379
Mwaka mmoja uliopita nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya kutunza mazingira hapa chuoni kwetu na nilipitishwa kwa kura nyingi sana na wanachuo wenzangu na kupata ushindi wa kishindo.
Lakini jana katika mkutano wa mwaka wa kamati ya kutunza mazingira, taarifa yangu ya mafanikio yaliyofikiwa na kamati yangu yameonekana kuwa kinyume na matarajio ya wanachuo wenzangu, kwani kulikuwa na malalamiko mengi sana ya uchafu katika mazingira ya chuo, mitaro kuziba kutokana na uchafu, mazalia ya mbu kutothibitiwa na hivyo kusababisha wanafunzi kuugua malaria kwa kiwango cha kutisha.
Nilikubali udhaifu wa kamati yangu katika kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika muongozo wa kamati yetu, hivyo niliamua kujiuzulu ili kupisha mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza.
Nawausia wana JF wenzangu na wananchi wote kwa ujumla, muige mfano wangu, pale inapoonekana mmeshindwa kutekeleza majukumu yenu mliopangiwa hata kama ni majumbani kwenu, basi mkubali kuwajibika na kuachia ngazi.
Nawasilisha!