Ambassador
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 933
- 78
Jiji la Dar limetawaliwa na udereva wa kihuni (kutofuata sheria) hasa ukiongozwa na madereva wa daladala. Sina uhakika kama hili linatokana na foleni au ni hulka ya madereva wa aina hiyo.
Ni jambo la kawaida kukuta magari yanayotoka upande fulani yanaedelea kuja kwa kasi na kuzuia yale yanayotakiwa kwenda wakati taa ya kuzuia magari hayo imeshawaka. Vilevile imezoeleka miongoni mwa madereva wa Dar kuchomekea ghafla katika foleni bila hata ishara yoyote, kama ilivyokuwa kulazimisha kupita upande usiotakiwa (kulia) na kuleta bugudha kwa magari yanayokuja kutoka upande huo.
Mara nyingi magari yanapotoka barabara za pembezoni na kutaka kuingia barabara kubwa madereva walioko kwenye barabara kubwa wanajitahidi kubana mpaka wale madereva wanaotoka pembezoni watumie busara zao kuomba kama sio kulazimisha. Kwa wenye magari yenye ngao kubwa hili si tatizo kubwa kwani unapotishia na nagao mara nyinigi wanyonge huwa wapole.
Tukija katika subject matter, kwa uzoefu wangu wa kuendesha jijini nimekuta wanaoongoza kwa kuwabania wenzao ni madereva wa daladala na madereva wa kike. Kutokana na sababu hii kwa muda mrefu nimekuwa nikiwabania madereva wa daladala kila wanapojaribu kuchomekea daladala zao. Nimefanikiwa kwa sababu gari langu lina ngao kubwa mbele na nyuma, ingawa hazina majembe kama yale ya daladala.
Ingawa kwa muda mrefu nimekuwa nikiwaonea huruma akina dada barabarani, nimekuja kugundua kwamba hawalipi fadhila. Kwa kifupi ni wagumu na wabana mno ingawa kwa kuomba wanaongoza! Sijui ni kwa sababu hawajiamini (inferiority complex) au wanahisi wanatakiwa kupewa priority? Ndo maana nimeamua kuwabania madereva wa kike kuanzia sasa!!