Sikununu
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 341
- 100
Nilifika mkoa flani kutafuta maisha ambapo nilianza kwa kusua sua na hali ngumu ya maisha ndipo nilipokutana na binti mmoja ambaye nilimtokea akanikubali hivyo tukajikuta tunafanya ngono bila kinga kwa mara kadhaa.
Binti huyu alikuwa msaada mkubwa kwangu ikizingatiwa nilikuwa na hali ngumu ya kiuchumi ambapo alikuwa ananiliwaza sana na kunitoa kwenye sononeko la maisha, ghafla nilianza kupata mafanikio ndani ya mwaka mmoja na biashara zikaanza kuninyookea ndipo aliponiambia ana ujauzito (mimba) wangu nilipigwa na butwaa nisijue la kufanya lakini mwisho wa siku huruma na mapenzi nikamkubalia.Nilitoa huduma zote mpaka anajifungua mtoto ,niliamua kwenda kwa wazazi wake kujitambulisha ndipo tukaanza kuishi pamoja kama mume na mke
Nimepata mafanikio makubwa sana kwa kiwango cha kuridhisha katika umri wangu huu wa miaka 27 ambapo nimeshajenga nyumba nzuri na ya kisasa hapa mkoani na mashamba kama mawili nalimisha pia gari ya kutembelea pamoja na ya mama mtoto.
Mimi ni mnywaji mzuri sana wa pombe (kila siku lazima nitandike bia za kutosha) na kutokana na shughuli zangu nakua na campani kubwa ya mambo ya bata na hapa na pale,kuna siku tukiwa kwenye pombe na kilaji kuna jamaa akanijoke kwamba mimi nalea mtoto ambaye siye wangu na watu wote wanajua nilishtuka lakini nikajikaza kama sijasikia na utani huu ukajengeka kwangu ikawa kama mazoea.
Ndipo nikatafuta siku nikamuuliza wife kwa kumtega mbona huyu mtoto sijafanana nae na kwetu hajafanana na mtu yoyote,wife alijichanganya mwishowe akaniambia ukweli kwamba huyu mtoto sio wangu bali ni wa kijana mmoja kinyozi mimi nilimkuta tayari wapo kwenye mahusiano na yule kijana na pia kwavile aliikataa mimba na alivyoniambia mimi nikakubali basi ikabidi tuendelee.
Nilikasirika sana kama binadamu na kijana wa kiume nilitafakari na kumuuliza kama kuna mtu yoyote anayejua suala hili akanijibu hajamwambia mtu yeyeto hata wazazi wake hajawaambia,nikaamua kumsamehe na tukakubaliana tufanye siri maana tulishakuwa ndani ya ndoa.
Katika hali ya kawaida tunagombana isitoshe tabia yangu ya unywaji sana wa pombe haipendi lakini sasa nimechoka maana hata huyu mtoto wetu imefikia hatua anamwambia mbele yangu kwamba mimi sio baba yake na hatakiwi kuniita baba kwani baba yake si ameshamuonyesha,pia ananitukana matusi makubwa mpaka ya wazazi wangu.
Ninavyoandika hivi sijarudi nyumbani kwangu siku ya 5 na ninapanga kuvunja ndoa muda wowote maana huyu mwanamke ananidhalilisha sana pia nimepata habari leo amerudi nyumbani kwao kwa wazazi wake.