Nimeamua kusitisha matumizi ya mtoto mpaka nipate uhakika kwamba ni damu yangu

Karot

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
1,159
1,309
Jumapili iwe njema nyote wana JF...
Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Kisa ni kikubwa lakini nitajaribu kufupisha ili nisiwachoshe kusoma.

Ni kwamba kuna binti mmoja niliwahi kutembea nae mwaka jana. Lakini tulifikia hatua baada ya wiki mbili akanambia anajihisi ya kwamba ni mjamzito.

Sikuwa na shaka kwakweli maana niliamini kwakua nilikua kila wikiend nikiwa free kazini nakutana nae. Sikubahatika kwenda kumpima kutokana na majukumu kuwa mengi. Nilisafiri kikazi mwaka mmoja na miezi miwili.

Lakini wakati nipo safarini alikua akinipa taarifa mbali mbali za maendeleo yake ya kiafya na mimi nikawa namsaidia. Ikafikia hatua akanambia ameshajifungua salama na hakuna tatizo lolote lililojitokeza kikubwa nimuhudumie mtoto.

Sikuona shida nikawa nafanya hivo lakini kwa shida sana maana nilishawahi kubambikiziwa mimba hewa nikaliwa vyangu mpaka nikachakaa.
Na huyo wa kwanza nae nilikua safarini.

Lakini pamoja na yote, niliku nashindwa kumwelewa kwanini nikimuomba anitumie picha za mtoto inakua mbinde mpaka naanza kumtilia mashaka???

Nilimuomba anitumie picha hizo hadi ikakata miezi kama minne ndo akanitumia... Sasa nikabahatika kutimba nyumbani lakini kwa bahati mbaya yeye alikua Iringa mimi nikawa Zenji.

Mungu si Athumani wiki jana akanambia yupo Dar na mimi kwa bahati nzuri nikawa nina mpango wa kutimba Dar. Nikasema poa itajulikana mbivu na mbichi. Kwa bahati tu jana nimetua Dar na nikajaribu kumtafuta nimuone mtoto wangu.

Nilienda mpaka ghetoni kwake alipopanga, kweli mtoto anae lakini kimbembe kikawa hapa.....
Na hapo ndo nikajua ukweli kwamba kuna kitu nadanganywa.
ITAENDELEA......
 
Ninapenda sana watoto hata asiwe wangu nitamlea maana hakuna mtoto haramu.

Mimi mwenyewe sina uhakika kama huyu baba niliyenae ndiye baba yangu. Kama unaweza kulea lea ila kama huwezi subiri upate uhakika.
Ni mara mia Uwe na mwanamke ulomkuta ana mtoto.

Au ulomkuta na mimba.

KULIKO KUA NA MWANAMKE ALOKUAMBIA MIMBA NI YAKO ,UKATUNZAA WEE, ALAFU MWISHO ULAGUNDUA SIO WAKO.


Kwahili tuwe wawazi na wakweli !!....
 
Hatakuwa ameniumiza hata kidogo nina moyo mgumu na mbaya kuliko shetani.

Maisha yenyewe yako wapi ya kuanza kukimbizana kisa watoto wa nje ya ndoa?
Ni mara mia Uwe na mwanamke ulomkuta ana mtoto.

Au ulomkuta na mimba.

KULIKO KUA NA MWANAMKE ALOKUAMBIA MIMBA NI YAKO ,UKATUNZAA WEE, ALAFU MWISHO ULAGUNDUA SIO WAKO.


Kwahili tuwe wawazi na wakweli !!....
 
Hatakuwa ameniumiza hata kidogo nina moyo mgumu na mbaya kuliko shetani.

Maisha yenyewe yako wapi ya kuanza kukimbizana kisa watoto wa nje ya ndoa?
Duuuhh mkuu ilo mm siwezi kulivumilia hata siku moja.

Mara mia nimkute kazaa au anamimba ila nmempenda.

SIO anizuge , binafsi na Hasira, ,ivo kuepusha Shali , ni kuachana naye tu
 
hivi hatuwezi kuwa na mfumo ambao ujinga ujinga untupiliwa mbali kabla akili kubwa haijausoma?
 
Ninapenda sana watoto hata asiwe wangu nitamlea maana hakuna mtoto haramu.

Mimi mwenyewe sina uhakika kama huyu baba niliyenae ndiye baba yangu. Kama unaweza kulea lea ila kama huwezi subiri upate uhakika.
Wanawake wata like Sana comment yako
 
Updates:

Kwa bahati nzuri jana nilipofika kwake nikamuona mtoto kwa mbali kafanana na mimi, ila nikamuomba nipate vithibitisho vya vyeti vya mtoto.

HAPA NDO PALIPONIFANYA NILETE UZI HAPA.

Nilijaribu kumuomba vyeti vikiwemo kimoja alicho akihudhuria clinic kingine cheti cha kuzaliwa cha mtoto. Wakati yupo Iringa alinambia mtoto hajatahiriwa nikajaribu kumtumia pesa ya tohara na pesa ya kubadisha jina la mtoto kwa upande wa cheti cha kuzaliwa.

Alinijibu ameshafanikisha yote, "nikamwambia sasa naomba nipigie picha hicho cheti halafu nitumie nione umeandika majina gani? isije umekosea" ikawa shida kufanya hivo.

Ikabidi nianze kujikausha nisitume tena chochote maana niliona kuna mchezo nachezewa. Baada ya kukaa kimya kwa mda mrefu akawa anaanza kunitishia kunipeleka kwa Makonda au ustawi wa jamii. Na mimi nikamwambia itapendeza sana ukinipeleka huko maana naamini nitaenda kupata uhakika zaidi kuhusiana na hili.

Hakuishia hilo ikawa ananitishia hata kuniuwa eti tukose sote. Nikamwambia usipate tabu kutaka kuniuwa itakua umejipotezea mda zaidi na pia utakua hauna ulilofanikiwa, subiri unipeleke kwa Makonda ili upate haki za mtoto.

Kimya kilitawala, hakujua afanye nini baada ya kuona kila analofanya nalitolea nje.
Jana nilipofika kwake baada ya salam nikajaribu kumuomba cheti lakini akanambia kimo kwenye beg na limejaa sana, nikamwambia nitavumilia mpaka atakapomaliza shughuli zake ili nipate kukiona.
Na yeye alinihakikishia kunipa...

Basi ikabinidi ni mvumilivu kidogo. Nilivumilia sana mpaka nikaona uzalendo unaanza kunishinda. Nikatoka nje kwenda kuongea nae maana alikua uwani na palikua na wapangaji wenzake. Sikuona busara kutaka kuanzia maneno mbele za watu ilihali keshawatambulisha kwamba mimi ndo baba mwenye mtoto.

ITAENDELEA...
 
Kwamba ni story ya Kitabu itaendele kila mudaa...???? Acha uzwazwa ndo maana umepigwa pesaaa...na cheti jina limeandikaa la mwingne... Pole mzeee mwenye jina kwenye hicho cheti ndo mwenye mtotoo kisheria...Wajingaa ndio waliwaooooooo
 
Back
Top Bottom