Nimeamua kupiga kura yangu 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeamua kupiga kura yangu 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mokoyo, Sep 27, 2010.

 1. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,828
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kutoa topic hapa kuwa "Sintopiga kura kwenye uchaguzi wa 2010", nilikuwa serious kabisa na uamuzi ule kwa wakati ule. Ila baada ya tafakari ya kina na kusoma makala mbalimbali pamoja na kufuatilia kwa umakini umuhimu wa kupiga katika kuchagua viongozi halali na makini nimeamua kupiga kura yangu. Pia kilichonisukuma kupiga kura yangu ni baada ya kugundua kuwa kuna maelfu ya Watanzania ambao hawatapiga kura kutokana na sababu kama zangu hapo awali au zaidi ya zile; kwa mfano wiki moja iliyopita niliongea na kijana mmoja na akasema hawezi kupiga kura kwasababu tayari MSHINDI ANAFAHAMIKA, sasa watu wa aina hii kama wako miatano kila wilaya ina maana kuna balaa kubwa sana na hii kupelekea kuwa faida kwa wagombea wasiokubalika!

  NB:-Elimu ya uraia na ya kupiga kura bado inahitajika kama Tanzania inahitaji mabadiliko ya kweli kwenye uchaguzi wa viongozi na elimu hiyo ianzie vijijini kuja mijini tuache makelele tu kwa watu laki tano wakati watu milioni kumi na tano hawasikii hayo makelele.

  Niko katika harakati za kuhakikisha kuwa Watanzania wengi zaidi wanapiga kura ila sintoharakatisha Mtanzania yeyote kumpigia mgombea au chama fulani kura yake maana hata kura yangu ni siri yangu kwa kiongozi makini
   
 2. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hongera sana kumbuka kua "viongozi wabovu huchaguliwa na raia wazalendo wasiopiga kura''
   
 3. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hata mimi sitopiga kura kwasababu mshindi anajulikana, kunabaazi ya wagombea wa upizani mwaka 2005 hawakupata kura hata moja ktk majimbo yao, wakati wao wenyewe na familia zao walipiga katika jimbo hilohilo, kama si uchakachuaji ni nini? sipotezi muda wangu wakati najuwa uchaguzi wa Tanzania kuchakachua tu!.
   
 4. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Viongozi wabovu huwekwa madarakani na Watanzania wasiopiga kura. Hongera kwa kutokuwa miongoni mwao. Ubarikiwe
   
 5. K

  Kifoi JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: May 12, 2007
  Messages: 836
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Kura yako haina maana yoyote wala haitaisabiwa kwani tanzania hakuna uchaguzi kuna uchafuzi tu baadamu NEC ni CCM ni upumbavu tu kuipiga kura
   
 6. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  viongozi wabovu huchaguliwa na wazalendo kama wewe ambao hawapigi kura, so please change your mind
   
Loading...