Habari wana JF!
Mwaka jana ulipoanza niliweka nia ya kujifunza website development, nashukuru nimefanikiwa kutengeneza website yangu na kilichobaki kuifanyia minor improvements na kuihost (nitaileta mrejesho hapa nikisha i host)!
Sasa huu ni mwaka mpya umeanza na nimeona ni vyema nikajiongezea ujuzi katika hii anga ya teknolojia. Kwa kifupi nimeamua kuanza kujifunza programming, regardless of my background naamini nitatoboa!!
Haya ndio malengo yangu mwaka huu!
My vision: Kuwa android developer.
My mission: Kujifunza java programming na android development na kufanya practice mpaka niweze!
Hii safari itagawanyika katika sehemu mbili!
Sehemu ya kwanza ni kujifunza programming!
Sehemu ya pili ni kujifunza android development!
Nitatenga
atleast masaa matatu kwa siku(yanaweza kuongezeka), yaani atleast lisaa limoja ni kusoma new ideas kupitia vitabu na youtube videos then masaa mawili niku practice/ku-code nilichojifunza!
NB: Nakaribisha wenzangu wenye nia tuanze hii safari ambayo kiuhalisia si safari rahisi ila penye nia pana njia na nna amini tutafanikiwa!
Nakaribisha mawazo yenu wadau!!