Nimeamua kuanza kujifunza computer programming (back end development)

Ninaomba kuuliza kusoma udemy kozi kwa kulipia faida yake ukilinganisha na kusoma bure. Vipi vya ziada unapata ukilinganisha ukiangaika na tutorials?
 
kwanini unaichukia sana php mkuu
 
asante kwa ushauri mzuri nitaufanyia kazi kikamilifu kwa uwezo wa mungu, kama unafahamu resorce nzuri za kujifunza na kupractice php naomba unisaidie pia,
 
kwanini unaichukia sana php mkuu

Ina performance mbaya alafu ilitengenezwa ovyo ovyo.

Mfano methods za php naongelea core achana na libraries, unakuta method nyingine zinatumia camelCase, huku method nyingine zinatumia under_score, unakuta method nyingine zimeandikwa kijinga hadi unacheka camelCase_under_score. Ukiwa unatengeneza software unatakiwa kufuata style moja when it comes to naming things sio unachanganya changanya ovyo bila sababu yoyote, inaonyesha php imetengenezwa na watu kibao ambao walikua hawawasiliani au aliyekua anafanya code review alikua anapitisha ovyo tu bila kujua style wanayotumia ni ipi.

Ni 2019 multicore CPUs zimekuwepo for a whole decade now, kutumia cores zote za CPU kwa kutumia php unaweza lia, concurrency ni mbaya kupita kiasi, kama hutumii load balancer on top ispin up new threads kuserve requests umeumia, php yenyewe haikutengenezwa for concurrency, ni ya zamani enzi hizo kila kitu ni single core tu. Language nyingi sana zinaperform better than php, hata node ambayo pia siipendi inajitahidi kuhandle concurrent tasks kuliko php.

Sababu ya kutumia php mwaka huu imebaki tu kua php inatumika kwenye websites nyingi sana, ni moja ya languages ambazo zilipata adaptation kubwa mno wakati zinatoka, tofauti na hapo hakuna faida nyingine yoyote ile. Jaribu kusoma language kama Rust, Golang kwa backend uone kama utarudi kugusa php.
 
Mbona node ipo vizuri tu mkuu.
 
Mbona node ipo vizuri tu mkuu.

Node.js runtime environment ni nzuri sana, yaani tangu nianze kuitumia sijawaza kingine chochote, ilivyo fast haswa kwa kutumia uwezo wake wa non-blocking na pia uwezo wa kuengeneza web server yako mwenyewe, na zaidi uwezo wa kutumia technology moja ya Javascript both fronted and backend.
Halafu ilivyo na wingi wa packages, leo hii kuna zaidi ya 500,000 freely available packages.
 
Mbona node ipo vizuri tu mkuu.

Kwa kazi unazofanya, ila kuna kazi ambazo kufanya kwa node ni kulazimisha tu, software zinazodeal na calculations kibao au highly concurrent applications ni uvivu kutumia node coz itakua na performance mbaya.
 
Kwa kazi unazofanya, ila kuna kazi ambazo kufanya kwa node ni kulazimisha tu, software zinazodeal na calculations kibao au highly concurrent applications ni uvivu kutumia node coz itakua na performance mbaya.
Kwa hiyo mkuu Graph wewe kwenye kazi zako unapendelea sana kutumia programming language zipi???
 
Kwa hiyo mkuu Graph wewe kwenye kazi zako unapendelea sana kutumia programming language zipi???
Kwenye hesabu na ufanisi wa hali ya juu utahitaji lugha zinazo support angalau concurrency. Node ni single threaded. So hapo ni lugha kama C++, Erlang/Elixir, Golang et al
 
asante kwa inspiration, coz my point is to become software developer so nilikuwa nataka nianze na kitu ambacho hakitanikatisha tamaa then baada ya kuwa comfortable ndio nianze kupambana na lugha nyingine ambazo kwangu naziona ngumu kidgo like JAVA
 
Kwa hiyo mkuu Graph wewe kwenye kazi zako unapendelea sana kutumia programming language zipi???

Rust, C++, Golang. Kazi zangu nyingi zinahitaji very high performance, hizi ndo language tatu nazocheza nazo kila siku.
 
Kwa front end development tafuta kitabu kilichoandikwa na Jon Duckett HTML & CSS Kizuri mno haitaji sana kusaidiwa na mtu nilianza kujifunza mwenyewe kupitia kitabu chake kwakweli utakipenda
 
Jifunze php ufanye kazi. Mengine utajifunza when you need to. Nawajua watu wanajua ma c++, python, Golang.. Ila unakuta mtu akipata bug anachukua wiki kusolve kisa hakuna community nzuri, leo hii ukipata tatizo lolote la php unapata suluhisho la haraka na kazi zinaendelea.. I love php when you only need to get the job done na hauangalii sana mambo ya performance.. Ila kama unaandika software yenye processing nyingi its not advised.

Mara nyingi mature programmers tunasahau kwamba beginners jus want a place to start. Kwa ushauri wangu php ni kianzio kizuri sana kwa backend web development maana ata sehemu za kuhost zipo nyingi..tofauti na language zingine.. almost every server has a LAMP stack. Endelea na php mkuu.. Master it and then think about upgrading later.. For now don't stress about performance.

As Zuckerberg would say.. Code now, Fix later.
 
mimi pia natumia node.js mkuu hakika ipo vizuri mnooo
 
Mkuu, nimependa vile umejibu swali.
Nadhani unaweza kunipa mwanga kidogo kwa hiki nnachotaka kujifunza.
Mie nataka kujifunza mobile app development from scrach, natakiwa nifahamu nini na nini ilhali sina ujuzi wowote wa programing zaidi ya kupenda kujifunza?!

Nimekuwa nikitengeneza native mobile apps kupitia 'appyet' na 'thunkable' lakini napenda kujua zaidi mkuu!

Msaada plz!
 
ni kweli ni lugha mbili tofauti ila javascripts akiilewa vizuri php itakuwa very simplekwakwe kuelewa
Kwa ushauri wa aina hiyo then inabidi ajifunze C ambayo hizo zote mbili zimekuwa inspired nayo directly au indirectly!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…