Nimeamua kuachana na dini, nitamuabudu Mungu kwa utaratibu wangu mwenyewe

change formula

JF-Expert Member
Sep 8, 2020
694
1,463
Nimejiridhisha kuwa hizi dini zetu hasa hizi kubwa ukristo na uislam ni dini za uongo na uzushi, zipo kwa ajili ya maslahi ya makundi maalumu ili kujinufaisha na kutawala dunia kwa kuwafanya watu wao kuwa wajinga ili watu wachache waishi kwa jasho na damu la watu wengine.

Kuna sababu kubwa nne kuonyesha hizi dini ni utapeli mtupu
Kwanza dini zimeleta vitabu na kujimilikisha hivyo vitabu na kuviita ni neno la MUNGU wakati ni uongo mtupu, tukianza na kitabu cha waislamu kinachoitwa Quran inasemekana maandishi ya hicho kitabu yalitoka kwa MUNGU kwa kuteremshwa kutoka mbinguni!! Na aliyeteremshiwa hayo maandishi ni mtu alieitwa Muhammad, hakuna ushahidi wowote kuonesha ni lini na wakati gani hayo maandishi yaliteremshwa zaidi ya maneno ya uyo mtu Muhammad aliamka tu asubuhi na kuja na hekaya zake kuwa ameshushiwa maandishi na MUNGU.

Ukitizama mengi ya hayo maneno yamejaa chuki,visasi,ghazabu,ubaguzi n.k hapa kuna maswali ya kujiuliza kuhusu uhalali wa hayo maandishi hivi MUNGU kweli aliewaumba watu wake bila ushauli wa kitu chochote, na mwenye uwezo wa kuwafanya chochote muda wowote watu wake aliowaumba, harafu awatumie maandishi ya kuwatisha kuwabagua kwa kuwaita majina ya kutisha kana kwamba hakuwaumba yeye!?

Hapo ndipo unapongundua maandishi hayo hayakutoka kwa MUNGU bali ni mbinu na hekaya za watu ili kuwatawala wenzao kwa manufaa yao.

Tukija kwenye kitabu cha wakristo kinachoitwa biblia!! Unagundua kuwa hakikutoka kwa MUNGU bali ni maandishi ya watu wachache kuweka mawazo yao ili kutawala wenzao kwa manufaa yao ya kisiasa,kimwili na kipesa.

Leo hii tizama maisha ya watu wanaojiita viongozi wa kidini mapadre,wachungaji nk wanaishi kwa jasho la wenzao kwa mahubiri ya kutisha,kuwafundisha kuwapa wao sadaka na kila kitu,uku waumini wakibaki masikini wa kutupwa na wao kukaa mezani na watawala kunywa na kula uku nyumba zao zikizungukwa na ukuta mkubwa walinzi, camera na mbwa wakali!

Wakivaa nguo za gharama,vito vya dhahabu,manukato ya gharama na magari ya kifahari,na wale waumini wenye pesa ndio wanaruhusiwa kuwakaribia ila wale masikini wanaishia kuombewa na kutolewa mapepo!! Masikini wana mapepo!! Matajiri wana neema!!

Ndugu zangu hizi dini zimeleta chuki, mauaji,ubaguzi, zimeondoa umoja zimeleta matabaka na ujinga,tujiulize tu kwa akili ya kawaida zimetoka kwa MUNGU kweli au ni miradi ya watu wabunifu tu wa kale kama waliobuni magari,ndege,simu,umeme nk?

Jibu hizi dini ni miradi ya wabunifu wa kale ambao walizibuni ili kututawala na kula bila kutoa jasho jingi. Mimi binafsi yangu hizi dini naziona kama za utapeli siziamini wala kuzikubali, nina amini MUNGU yupo kabisa sio kwasababu ya dini ni kwasababu ya mazingira na majira,nitatenda mambo mema kwasababu ninapenda amani na ustawi wa watu wote,nitatoa sadaka ila sio katika vikapu vya hawa matapeli ya kiislamu na kikristo ila nitatoa sadaka kwa watu na waitaji wengine ila sio kuwapa hawa viongozi wa dini hizi za kitapeli wanaotaka kula bila kufanya kazi wakati hawana ulemavu wowote.

MUNGU hana ubaguzi wowote kama wanavyofundisha hawa matapeli masheikh na wachungaji.
 
Nimejiridhisha kuwa hizi dini zetu hasa hizi kubwa ukristo na uislam ni dini za uongo na uzushi,zipo kwa ajiri ya maslahi ya wa dini hizi za kitapeli wanaotaka kula bila kufanya kazi wakati hawana ulemavu wowote.

MUNGU hana ubaguzi wowote kama wanavyofundisha hawa matapeli masheikh na wachungaji.
Nenda na umuabudu Mungu kwa Heshima na Amani.

Amen..
 
Twende mbele turudi nyuma swali linakuja je wale mababu wa mababu zetu waliofariki kabla ya ujio wa hizi dini 2 ni kwamba hawataiona pepo AKA mbingu ?
Hapo ndio unagundua hizi dini ni ujinga,utapeli ni ubunifu wa matapeli na wanazuoni wa kale waliobuni njia ya rahisi ya kumchinja kuku bila kumkimbiza ili mradi yupo bandani.
 
Nimejiridhisha kuwa hizi dini zetu hasa hizi kubwa ukristo na uislam ni dini za uongo na uzushi,zipo kwa ajiri ya maslahi ya makundi maalumu ili kujinufaisha na kutawala dunia kwa kuwafanya watu wao kuwa wajinga ili watu wachache waishi kwa jasho na damu la watu wengine.
Kuna sababu kubwa nne kuonyesha hizi dini ni utapeli mtupu

Kwanza dini zimeleta vitabu na kujimilikisha hivyo vitabu na kuviita ni neno la MUNGU wakati ni uongo mtupu,tukianza na kitabu cha waislamu kinachoitwa Quundisha hawa matapeli masheikh na wachungaji.
Uko sahihi kwakuwa hao tunaoambiwa ni watumishi wa Mungu ndiyo matapeli wetu namba moja, Mungu amewatuma waje watufundishe neno lake bure, wao wanatukamua upepo kila tukutanapo nao, wanatuambia wanauwezo wa kutuombea tuondokane na shida lakini wao wenyewe wanapopata shida hawamwombi Mungu wanakimbilia kututoa upepo waumini, sisi tukiumwa wanatuambia tumuombe Mungu, wao wakiumwa wanakuja kututoa upepo sisi
 
Nimejiridhisha kuwa hizi dini zetu hasa hizi kubwa ukristo na uislam ni dini za uongo na uzushi,zipo kwa ajiri ya maslahi ya makundi maalumu ili kujinufaisha na kutawala dunia kwa kuwafanya watu wao kuwa wajinga ili watu wachache waishi kwa jasho na damu la watu wengine.
Kuna sababu kubwa nne kuonyesha hizi dini ni utapeli mtupu


MUNGU hana ubaguzi wowote kama wanavyofundisha hawa matapeli masheikh na wachungaji.
Mkuuu! Weee unafikiri kwa nini watu wanamtafuta Mungu? Hakuna jinsi binadamu anaweza kuishi bila Mungu! Na Mungu ni mmoja na hajipingi! Kama Mungu wa Biblia ni Mungu! Basi wa vitabu vingine sio! Na kama mungu wa vitabu vingine ndiye basi Mungu wa Biblia sio! Sasa angalia! Dunia hii kuna shetani na huwezi kumshinda shetani bila msaada wa Mungu! Watu wa zamani walojua hivyo na kutengeneza utaratibu wa kumtafuta na kufanya mapenzi yake kwa njia ya dini!

Dini sio mpango wa Mungu! Mungu hakuleta dini bali alileta ushirika na binadamu kuishi pamoja katika nyanja zoote na maisha ili afanikiwe na kumshinda shetani ambaye kisheria naye anaishi dunia hii hii tunayoishi baada ya kuasi Adam katika bustani ya Edeni! Njia pekee ya wewe kusimama peke yako na ukamshinda shetani ni kuokoka!

Mlokole ndio pekee anayeweza kumtafuta Mungu na akamuona kupitia imani katika Yesu Kristo na kuvuta nguvu zake na kumshindia katika nyanja zooote ikiwemo uchumi eneo am alone walokole wanafeli na kuonekana masikini wakati hizo nguvu zinauwezo wa kuwawezesha kufanya biashara au kudumu katika ekima ya ajira! Okoka mkuu vinginevyo hutoboi!

Uwezi kumshinda shetani bila kuokoka! Kama ulivyosema dini ni utapeli! Na mimi nakubaliana na wewe hawa ni matapeli wanakwiba hela, mali ya kondooo!
 
Mi mwenyewe na wasiwasi ,eti israel taifa teule,ina maana sisi wengine ni wanyama,nashangaa wayahudi walifanikiwa vipi kueneza propaganda zao duniani? quran nayo ilikopiwa kutoka kwenye torati, ..dini imefanya watu kuwa wapumbafu yaani,magaidi nakutokuwa na maarifa,kuna jamaa wa ujeruman kiuhalisia aliniambia kiuhalisia hakuna shetani wa moto,dini zimeletwa ili kuleta hofu na kutawalana,wenzetu wamefikia kwenye kiwango kikubwa kwakuweka mambo ya dini pemben,
 
Mkuuu! Weee unafikiri kwa nini watu wanamtafuta Mungu? Hakuna jinsi binadamu anaweza kuishi bila Mungu! Na Mungu ni mmoja na hajipingi! Kama Mungu wa Biblia ni Mungu! Basi wa vitabu vingine sio! Na kama mungu wa vitabu vingine ndiye basi Mungu wa Biblia sio! Sasa angalia! Dunia hii kuna shetani na huwezi kumshinda shetani bila msaada wa Mungu! Watu wa zamani walojua hivyo na kutengeneza utaratibu wa kumtafuta na kufanya mapenzi yake kwa njia ya dini! Dini sio mpango wa Mungu! Mungu hakuleta dini bali alileta ushirika na binadamu kuishi pamoja katika nyanja zoote na maisha ili afanikiwe na kumshinda shetani ambaye kisheria naye anaishi dunia hii hii tunayoishi baada ya kuasi Adam katika bustani ya Edeni! Njia pekee ya wewe kusimama peke yako na ukamshinda shetani ni kuokoka! Mlokole ndio pekee anayeweza kumtafuta Mungu na akamuona kupitia imani katika Yesu Kristo na kuvuta nguvu zake na kumshindia katika nyanja zooote ikiwemo uchumi eneo am alone walokole wanafeli na kuonekana masikini wakati hizo nguvu zinauwezo wa kuwawezesha kufanya biashara au kudumu katika ekima ya ajira! Okoka mkuu vinginevyo hutoboi! Uwezi kumshinda shetani bila kuokoka! Kama ulivyosema dini ni utapeli! Na mimi nakubaliana na wewe hawa ni matapeli wanakwiba hela, mali ya kondooo!
Mkuu hebu kuwa serious kidogo
 
Back
Top Bottom