Nimeamka nimekuta nimenyolewa nywele upande mmoja kichwani

Kidingi

JF-Expert Member
Aug 11, 2012
1,872
1,832
Habari wana JF

Leo asubuhi kimenitokea kitu kilichonipa maswali mengi sana kwa sababu sijawahi kutokewa na kitu kama hiki.

Mimi ninaishi peke yangu kwenye nyumba hizi za kupanga, na kabla sijalala huwa ninahakikisha nimefunga mlango wa chumba changu.

Cha ajabu leo nilipoamka nimekuta nimeona nimenyolewa kidogo upande mmoja wa kichwa kitu kilichonishangaza sana (ni vile tu ukristu wangu umenipa ujasiri) ni kama umeenda kwa kinyozi badala ya kukunyoa akakuchonga juujuu upande mmoja tu wa uso wako. Nimejaribu kutazama kwenye shuka sijaona nywele.

Hivi kimeshawahi kuwatokea hiki kitu? Nini hasa inaweza kuwa dhumuni la huyu mtu? au ni ushirikina tu? Maana mimi sidaiwi wala sina ugomvi na mtu..
 
Ni ushirikina tu. Usipende kulala bila kusali.

Hatua ya kuchukua sasa maana ishatokea.

simama na Isaya 54:17 na pia ongeza kuwa, kila mbinu na hila walizokuwa wamepanga kwa ajili yako unazifuta kwa damu ya Yesu.

Amin na usonge mbele.
 
Huo ni Uchawi mkuu. Hata hivyo uchawi wa namna hiyo hautakuletea madhar yeyote. hapa wachawi huwa hawana nia mbaya na wewe, isipokuwa wanakupima na kujaribu nguvu zao. hat hivyo wanaweza wakacheza na nywele zako na nywele zikachelewa kuota. Usihofu, walikuwa wanacheza tu.
 
Ni ushirikina tu. Usipende kulala bila kusali.

Hatua ya kuchukua sasa maana ishatokea.

simama na Isaya 54:17 na pia ongeza kuwa, kila mbinu na hila walizokuwa wamepanga kwa ajili yako unazifuta kwa damu ya Yesu.

Amin na usonge mbele.
mbona umeanza na ushirika?je labda alikula wali na mchuzi wa nyama baada ya kunawa akajisaau na kajishika kichwani na panya wakapita.au wewe ndio mwanga nini..
swissme
 
Kona za mshana jr ngoja tumskie ana lipi hapa au hli jambo na kwake huenda likawa ni jambo jipya! angalia na sehemu nyingine mkuu naskia kuna majini yanakula vipapa embu jaribu kukangua huko
 
mbona umeanza na ushirika?je labda alikula wali na mchuzi wa nyama baada ya kunawa akajisaau na kajishika kichwani na panya wakapita.au wewe ndio mwanga nini..
swissme
Wissme, sitaki uchokozi asbh asbh jaman., washirikina ni watu tu ila mimi nimetoa yangu ya moyoni, yaan mawazo yangu.

Ukiaamua kuamini mimi ni mshirikina poa tu ni mawazo yako pia.
 
Habari wana JF

Leo asubuhi kimenitokea kitu kilichonipa maswali mengi sana kwa sababu sijawahi kutokewa na kitu kama hiki.

Mimi ninaishi pekeyangu kwenye nyumba hizi za kupanga, na kabla sijalala huwa ninahakikisha nimefunga mlango wa chumba changu.

Cha ajabu leo nilipoamka nimekuta nimeona nimenyolewa kidogo upande mmoja wa kichwa kitu kilichonishangaza sana (nivile tu ukristu wangu umenipa ujasiri) ni kama umeenda kwa kinyozi badala ya kukunyoa akakuchonga juujuu upande mmoja tu wa uso wako. Nimejaribu kutazama kwenye shuka sijaona nywele.

Hivi kimeshawahi kuwatokea hiki kitu? Nini hasa inaweza kuwa dhumuni la huyu mtu? au ni ushirikina tu? Maana mimi sidaiwi wala sina ugomvi na mtu..
Popo bawa huyo
 
Mkuu, Nyumba unayokaa kuna watu ambao hukuona wa hali ya juu kuliko wao. Sasa wamekujaribu kidogo tu angalau uwaangalie.
Ati umesema weye ni mkristo hivyo huogopi. Hivi ukristo ni kuitwa John au Peter?? Sikutishii, kama kweli uliona kuwa umenyolewa, jua moja tu. Nywele ndio akili ya mtu, amekuchukua fikra zako. Atakuchezeshwa kindumbwendumbwe mpaka ukubali. Pamoja na ukristo wako leo utafahamu nnani bingwa. Kwa heri
 
Ni ushirikina tu. Usipende kulala bila kusali.

Hatua ya kuchukua sasa maana ishatokea.

simama na Isaya 54:17 na pia ongeza kuwa, kila mbinu na hila walizokuwa wamepanga kwa ajili yako unazifuta kwa damu ya Yesu.

Amin na usonge mbele.

Nashukuru mkuu, hapa wamegonga mwamba. Mungu yu pamoja na mimi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom