Nimeamka na homa kali

Nimeamka na homa kali

Nimejaa na wasiwasi wakuu,

Jana jioni nilianza kama dalili za mafua leo asubuhi nimeamka na homa kabisa, ila mafua yapo kwa mbaali. moyo umetanda hofu kwa kweli
Tumia njia hii hapa itaweza kukusaidia angalia hiyo video hapo chini

 
Sasa kama ana Corona si ndio anaenda kusambaza kwa watu wengine kwenye daladala, na hapo hospitali?

Maana si kama wenzetu ambao vipimo vya corona vipo hospitali zote

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni hatari najua sasa akikaa nyumbani bila tiba hali si itakuwa mbaya
Pitia posts za juu ameambiwa atumie tiba hiyo ya lemon .
 
Piga namba 199 au bofya*199# haraka sana upate usaidizi.

Mods wangeweka hizi namba kwenye tangazo lao hapo juu inaonekana watu wengi hawajui wafanyeje wakijiona wana hizo dalili

Jitenge na watu wengine mpaka itakapojulikana una tatizo gani
 
Ni hatari najua sasa akikaa nyumbani bila tiba hali si itakuwa mbaya
Pitia posts za juu ameambiwa atumie tiba hiyo ya lemon .
Kuna namba za simu zipo mtu unatakiwa kupiga kama unajihisi una dalili za Corona.
Utapata msaada.

Sio kwenda kusambaza zaidi kwenye basi na kwa wagonjwa wengine hospitali ambao unaweza kuta kinga zao ziko chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli mkuu.

sina mkuu, ila dalili zipo mana koo ipo kavu kama nataka kufanya mafua ni kikohozi
Sukutua kooni kwa maji ya uvuguvugu yenye chumvi
Chemsha tangawizi kali katia na ndimu au limao bila kumenye maganda kisha kunywa kikombe kimoja cha chai mara 2 au 3 kwa siku
Acha hofu mbona haya magonjwa yalikuwepo tu,si unajua bongo vumbi jingi

Kutoa homa chemsha
Chemsha malimao+tangawizi +muarobaini hlf jifukize
Utakuwa poa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejaa na wasiwasi wakuu,

Jana jioni nilianza kama dalili za mafua leo asubuhi nimeamka na homa kabisa, ila mafua yapo kwa mbaali. moyo umetanda hofu kwa kweli
Kanunue machungwa ya, kutosha mpk jioni hakikisha umekula walau machungwa 10-15 njoo kesho utwambie km bado unaumwa.

Kumbuka kunywa maji, na usikubali kulala ukiweza tembeatembea ila epuka kukaa na watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana na juzi nimeumwa sana nikajua navuta! Leo nimeamka vizuri kiasi, nahisi joto tu kidogo. Pole sana
 
Back
Top Bottom