Nimeamini kwamba Sumaye ana nia ya kweli ndani ya CHADEMA.

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
8,511
10,986
Kafanyiwa visa na vituko lakini bado alitoka na kusema hadharani kwamba hatorudi CCM.

Tumemuona Lowasa akitangaza kurudi ccm mchana kweupee, lakini Sumaye hakutetereka, anatikiswa lakini kakataa kutikisika ni wakati sasa watu kumuamini na kumpa heshima ndani ya chama.

Binafsi naona huyu mtanzania mwenzetu, anayo nia ya kweli kuitokomeza ccm tumuunge mkono.
 
Awanie uenyekiti wa chama kama hajatekwa mtaniambia, shida iko hapo, yeye aendelee kuwa mpigania chama wa nje, siku akitaka kuingiza mkono wake Mgabe atamkata.
 
Sumaye yupo Chadema kusaidia Ccm na kayasema hayo hadharan sasa arudi Ccm kufanya nini wakati yeye kishasema yupo huko kutusaidia
 
Never say, "Never"

Kwenye siasa kila kitu kinawezekana.
Kuna watu kwenye Nyuzi kadhaa humu walisema haitakuja kutokea E.L kwenda CDM na akapokelewa yaliyotokea kila mtu alishuhudia. Ikasemwa tena hawezi rudi alikotoka akarudi na tena akapokelewa kwa heshima kubwa. Hili ni somo muhimu kuwa usiwaamini sana wanasiasa.
 
Kafanyiwa visa na vituko lakini bado alitoka na kusema hadharani kwamba hatorudi CCM.

Tumemuona Lowasa akitangaza kurudi ccm mchana kweupee, lakini Sumaye hakutetereka, anatikiswa lakini kakataa kutikisika ni wakati sasa watu kumuamini na kumpa heshima ndani ya chama.

Binafsi naona huyu mtanzania mwenzetu, anayo nia ya kweli kuitokomeza ccm tumuunge mkono.
Sumaye ni shujaa na atakumbukwa daima katika siasa za Tanzania
 
Back
Top Bottom