Kurunzi
Platinum Member
- Jul 31, 2009
- 10,175
- 11,572
Mkuu naomba uwe unatupa updates ya maisha mapyaNimefanya kazi katika kampuni hii kwa miaka minne kama afisa manunuzi. Kutokana na ugumu wa soko, ikabidi team ya "sales" iongezewe nguvu na ndipo watu kutoka vitengo vingine ikabidi tuhamishiwe kitengo hiki.
Kwa wasiojua, Sales Officer kazi yake ni kutafuta wateja wa bidhaa za kampuni.
Katika maisha yangu, nilipanga mwaka 2020 haitavuka lazima nitaacha kazi na kujikita kwenye kujiajiri kwa asilimia mia. Hivyo tayari nilikuwa najiwekea akiba na pia nilishaanza kufanya biashara yangu.
Kwanini nimeacha kabla haijafika 2020? Ni kwa sababu nimehamishiwa kitengo cha Sales. Nimeona si akili kutafuta wateja kwaajili ya kampuni kuanzia asubuhi mpaka jioni wakati namimi nina biashara yangu natakiwa kutafuta wateja.
Hivyo, nitatumia muda ambao nilikuwa natakiwa kutafuta wateja wa kampuni kutafuta wateja wa biashara yangu. Najua sio rahisi lakini nitaweza.
Usipotaka kujiajiri kutimiza ndoto zako basi utaajiriwa kutimiza ndoto za wanaume wenzio. Usiku mwema
12/12/2018, 09:12 Pm