Nimeacha kazi leo

Nimeacha kazi leo

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,533
Reaction score
3,837
Nimefanya kazi katika kampuni hii kwa miaka minne kama afisa manunuzi. Kutokana na ugumu wa soko, ikabidi team ya "sales" iongezewe nguvu na ndipo watu kutoka vitengo vingine ikabidi tuhamishiwe kitengo hiki.

Kwa wasiojua, Sales Officer kazi yake ni kutafuta wateja wa bidhaa za kampuni.

Katika maisha yangu, nilipanga mwaka 2020 haitavuka lazima nitaacha kazi na kujikita kwenye kujiajiri kwa asilimia mia. Hivyo tayari nilikuwa najiwekea akiba na pia nilishaanza kufanya biashara yangu.

Kwanini nimeacha kabla haijafika 2020? Ni kwa sababu nimehamishiwa kitengo cha Sales. Nimeona si akili kutafuta wateja kwaajili ya kampuni kuanzia asubuhi mpaka jioni wakati namimi nina biashara yangu natakiwa kutafuta wateja.

Hivyo, nitatumia muda ambao nilikuwa natakiwa kutafuta wateja wa kampuni kutafuta wateja wa biashara yangu. Najua sio rahisi lakini nitaweza.

Usipotaka kujiajiri kutimiza ndoto zako basi utaajiriwa kutimiza ndoto za wanaume wenzio. Usiku mwema

12/12/2018, 09:12 Pm
 
Umefanyaa maamuzi magumu na mazuri piaa, kuajiliwa na kuolewa vinatofautiana kdg tu.
Kwan kuna tofauti gani kati ya Mshahara na Mahali? Au kusubiria majibu ya barua ya App na kusubiria uletewe barua ya posa?
Asalaaale njemba zinaolewa bila kujijuaa,

Hahaa TUCTA OYEEEE?
CCM OYEEEE?
25% OYEEE?

Shaaaabash tutakutana either kileleni au bondeni, hamna kubak katikati shwain kbsa, asahv kusurvive ni vitu viwili tu vinahtajka, either utumie ubongo au utumie ulimi, namaanisha uwe smart sana kichwani au uwe mnafk kiwango cha lami mdomoni
 
vp mshalipwa pesa yenu na clouds/fiesta?
mola akujaalie ama baada ya kutumika kuchafua kampuni za watu asaiv umeamua ujiongeze.... bravo
washtue na Mataahira wengine apo
 
Kila la kheri kama ulianza biashara yako.

Kuna jamaa sales aliamua kuondoka kwenye kampuni akarudi kuomba kazi tena
Lakini wewe sio yeye don't get me wrong
 
Acha upuuzi.

Afisa manunuzi anayetaka kununua tuuuu wakati wengine wanahangaika kutafuta wateja.
Unahamishwa kitengo unaacha kazi.

Ulikopelekwa ndo muhimu kwa mtu anayetaka kujiajiri.
KUTAFUTA WATEJA. ungebaki hapo ukajifunza mbinu ningekuona wa maana.

Kwa atitude hii ya kuzira sitashanga kujiajiri kukawa kaa la moto.

Badilikaaa
 
Kwani wanaoajiri ni wanaume pekee? maana hapo mwishoni naona kutimiza ndoto za " wanaume wenzio".
 
Back
Top Bottom