Nilizalishwa na kudhalilishwa

Nilizalishwa na kudhalilishwa

Jan-uary

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
1,050
Reaction score
1,144
Katika harakati za kutafuta mkate nilikutana na mwanaume ambaye hatimae akawa mzazi mwenzangu, tuliishi kipindi kirefu sana tukiwa kama mke na mume, mwisho wa siku jamaa akaamua kuachana na mimi kwa mbwembwe na udhalilishaji wa kimataifa, mabaya mengi sana alinizushia ili tu azma yake ya kutaka kuniacha kiholela ipate waungaji mkono.

Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa wengi walimuunga mkono, kejeli matusi vilikuwa vikipishana mitaani vikinisaka mimi na haikuwa mimi tu mpaka familia yangu iliunganishwa kwenye hiyo dhihaka, kilikuwa kipindi kigumu sana haijawahi kutokea, maradhi msongo wa mawazo viliandama kiasi kwamba niliichukua dunia, nilijuta kwanini nilizaliwa.

Wakati mwingine nilitamani nife niondokane na haya mateso, lakini nilikuwa nikimwangalia mwanangu naishia kulia, nawaza nikifa leo huyu kiumbe asiyekuwa na hatia nitamwacha katika mazingira gani?

Mungu si James, kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele nikawa naizoea hali ile, nikaikubali hali ile na niambiwe au nisikie nini sikuweza kuumia tena, mpaka naandika uzi huu nina amani na yaliyopita yamebaki simulizi tu wala hayaniumizi tena. Kilichonileta kwenu ni hiki -mpuuzi yule ana kila dalili ya kutaka kujiletaleta kwangu, najua iko siku ataleta swaga zake za kiduwanzi, nimetafakari ikitokea nimjibu nini ili naye ayapate maumivu mara mia ya niliyoyapata mimi nimeshindwa.

Nisaidieni wana MMU.
 
Mtu kama huyo unakaa nae mbali wala husimkaribishe kuongea nae.

Yaani mwacha apite huko.. akitaka mwanenu kumuona panga mtu unamuamini tena wa kiume awe anapeana nae.

Hayo ya kutuuliza usemeje ukiambiwa umwambie bado unampenda utamwambia!?
 
Mtu wa namna hiyo unamvutia kiti anakaa akisha ona amefika unaanza kumlipa moja baada ya jingine hakikisha uwe na detail ili ujue ni wapi patakamo muuma na wewe utakapo anza hakikisha unamdharirisha mpaka ajione mavi kabisa........!!***
Hata kama bado unampenda we msomeshe namba
 
Mtu kama huyo unakaa nae mbali wala husimkaribishe kuongea nae.

Yaani mwacha apite huko.. akitaka mwanenu kumuona panga mtu unamini tena wa kiume awe anapeana nae.

Hayo ya kutuuliza usemeje ukiambiwa umwambie bado unampenda utamwambia!?
Shukrani saaaaaaaaaana
 
Back
Top Bottom