Niliyomuahidi mke wangu kwenye 'game' naweza kuyatengua?

Kazwala mkuu

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,034
2,250
Salaam,

Mahusiano hayana darasa wala uzee na kila siku hujitokeza mapya hivyo si vibaya kubadilishana mawazo hata kwa vitu vidogo vidogo ili kueneza upendo kwa wenza wetu.

Jana nilikuwa na muda mzuri sana na mke wangu na akanifanya nijione nimezaliwa upya haswa kwa uzuri wake na jinsi anavyojua kuutumia kunako mambo yetu, naam ulikuwa ni muda maridhawa sana ulionifanya nimshukuru Mungu kwa kunipa mke huyu kwani hachoshi na sijutii kumuoa kabisa.

Sasa ndugu zangu, kumbe jana nilipokuwa kiunoni mubashara nilikuwa nilikuwa nikimwambia kuwa leo nitamnunulia au kumfanyia hiki au kile.

Sasa kumekucha yupo hapa pembeni yangu ananikumbushia ili nimpe aende madukani akanunue niliyomuahidi na nikicheki orodha ni ndefu wakuu.

Je, nipasue pochi nimpe au nitengue kauli kwa kusema niliahidi wakati wa shinikizo, wakati wa kutojitambua? Nikitengua itakubalika kwa sheria za kitanda?

Nawasilisha
 
Hongera kwa kutambua uzuri wa mkeo na kumshukuru Mungu kwa hilo, ninachokushangaa ni kwamba kwanini uone tabu kumhudumia mkeo? iwe alikuridhisha au hakukurithisha, Kama utaona tabu kumhudia mkeo tambua kwamba wapo watu ambao wanajua kujali na kuhudumia na mkeo akiangukia katika mikono yao usijerudi JF kuomba ushauri, tambua ya kwamba wewe ndio chanzo na msababishaji mkuu!!
The choice is your!
 
Usimpe uone watakaompa baadae uje ulalamiem hapa,,mke wala haitaji ushaur ni bora ufilisiwe ma mkeo mwenye watto wako kuliko michepuko ambayo baadae itakucheka
 
Kama ni mke wako na upendo wakutosha unaupata na mambo anakupa hadi unajisahau kama upo duniani au ahera unashindwaje kumpa mkeo ulicho muahidi, kumbuka unavyo toa ndio utakavyo pata zaidi kutoka kwa mkeo …
 
Dah kwa proud ya kiumeni inatakiwa ute tu ila next time be cautious on what you are promising bro
 
Ahadi ni deni,,,kama orodha ni ndefu basi mpe vichache kwanza ambavyo vipo ndani ya uwezo wako alafu mueleze vizuri kuwa umepungukiwa hivyo vingine utamalizia as soon as mambo yakiwa sawa na ujitahidi kweli kutafuta pesa umalizie hiyo orodha iliyobaki,,,ukileta longolongo watakuja watakaompa mara 5 ya orodha ulioiahidi kwaiyo jitahidi utimize ahadi zako.
 
Wewe mgeni eeh?
Jumla ya ahadi zangu zoooote ukizi convert kwenye cash unajenga shule ya kata
 
Usiwe unaahidi kitu ukiwa na furaha sana... Ya wahenga hayoo....

Mpe mkeo zawadi yake bhana, we unafikiri ni shughuli ndogo kumridhisha mwanaume...., tena mpaka akusifie hadharani!!!!
Mpe jamani
 
Back
Top Bottom