Kuna jamaa alikuwa ni mfagiaji kwenye ndege. Siku moja wakati anafagia chumba cha mapilot akakuta kitabu kilichoitwa,'Jifunze kurusha ndege kitabu cha kwanza' Kufungua ukurasa wa kwanza, kukawa na maelezo' Kuwasha injini bonyeza kitufe cha kijani, akabonyeza na injini zikawaka akaona raha, Ukurasa wa pili ukawa na maelezo ukitaka ndege ianze kutembea bonyeza kitufe cha bluu, akabonyeza ndege ikaanza kwenda mbele, ukurasa unaofuata ukawa na maelezo ukitaka ndege ipae bonyeza kitufe chekundu, akabonyeza ndege ikapaa akajiona mjanja saaaana. Akaanza kutafuta namna ya kutua , akafungua kitabu mpaka mwisho akakuta sentensi inasema kwa maelezo ya kutua, nunua 'Jifunze kurusha ndege kitabu cha Pili'.