Poleni na majukumu wana wa mungu!!!!
Nimekuwa kwenye mahusiano na binti Fulani hapa chuoni kwa kipindi kama cha mwaka mzima mpaka sasa.
Mwanzo nilimuona ni binti mstaarabu na asiependa makuu kwani hapendi kuvaa au kupendeza sana (anavaa kikawaida sana) kama wasichana wengine wa vyuoni……nilipo muona kwa mara ya kwanza niliona atanifaa kwa sababu asingeweza kuniingiza kwenye gharama za rejareja.
Sasa bwana!!!! Kumbe nilikuwa najidanganya sababu wanawake ni nyoka aiseeh!!! Tena wenye sumu kali sana tena sana…. Ipo hivi,juzi nilimkuta anachat na mtu nikamuuliza mbona siku hizi anachat sana akaniambia anachat na kaka yake(kuna jamaa alishawahi kuniambia ni kaka yake lakini Kumbe ndio mtu wake wa nguvu kabsa)……sasa bahati mbaya au nzuri mwamba akapiga simu,alipoona ile namba binti akagoma kupokea simu
Mimi:Mbona hupokei simu
Yeye:Huyu kaka yangu ananisumbua tu achana nae
Niliendelea kumlazimisha apokee simu lakini mwisho akapokea ila akamjibu;
Yeye;Kaka nipo kwenye kelele nipigie baadae
Kiukweli taa nyekundu ilianza kuwaka kichwani kwangu na nilianza kumfuatilia mpaka jana nilipo pata sababu ya kuandika haya,ilikuwa hivi;
Nilifanikiwa kupata namba ya huyo mwishowe nikampigia simu kama kumsalimia,nikamuuliza kama ana mdogo wake akaniambia hana….baadae nikamuuliza kama anamjua binti yule akanijibu ndio.
Mimi:Sawa kaka nashukuru kwa ushirirkiano wako
Jamaa:kwanini umeniuliza??? Na wewe nani yako? Niambie ili nikuambie mengi ambayo nayajua kuhusu huyo binti
Mimi:Kiukweli kaka nipo nae kwenye mahusiano ila nilikuta namba yako ndio imenitisha…….
Jamaa
😀aah!!! Kijana huyo binti ni mpuuzi sana tena kummk ….mimi nipo nae kwenye uhusiano mwaka wa 4 sasa na ata ada namlipia mimi kuanzia yupo advance mpaka sasa yupo chuo bado anatumia pesa yangu(hana mkopo wala boom) sasa nashindwa kuelewa huyu binti ananitaka nini…….nitamuua kummk aache kucheza na mimi
Mimi:Kaka nimekuelewa na Asante sana kwa ushirikiano wako
Jamaa
😀ogo usikate simu ngoja nikuunganishe nae ila usiongee chochote mpaka nikuruhusu sawa?
Mimi
😛oa kaka hakuna shida!!!
Jamaa akamuunganisha kwenye mazungumzo yetu….kiukweli niliyo yasikia kutoka kwa yule binti sikuamini,yani alikuwa anamsifia mwamba wazi wazi tena kwa Mahaba yote(alikuwa ananiambia hana mtu mwingine zaidi yangu) nilitamani kama angekuwepo nimchape ata shaba….
Waliongea mengi mwisho mwamba akaniambia:
Jamaa:Oya ebu zungumza na huyu baby wako nahisi umemsikia yote anayoniambia
Mimi:Mambo mrembo
Binti:Nzuri wee nani tena jamani???
Mimi:Ngwale jr(nikamtajia jina langu)…..Aliposikia jina langu akaanza kulia na akaniambia mbele ya jamaa anasikia eti nimsamehe na akakata simu baadae jamaa akaendelea;
Jamaa;Oya huyu binti nitamfanyia zengwe hataamini maisha yake na ikiwezekana nitampoteza na mimi nipotee kabisa(jamaa ana pesa sana maana anamiliki hotel kubwa moshi nyumbani kwao na huyu binti kwa taarifa nilizo pata )
Sasa leo huyu Delilah asubuhi kaamkia ghetto kwangu huku analia anataka anielezee kila kitu kumuhusu huyu mwamba…..nilikuwa nina hasira sana nikamjibu kuwa nahitaji aondoke maana sitaki ata nimuone,Alilia sana baadae niliamua kumtoa nje kwa nguvu na kuzima kabisa mpaka ile sim card aliyokuwa anaifahamu
Ninamuona kama muuaji kwangu maana tulikuwa tunatumia sana za kwake kumbe ni za jamaa yake….sasa baadae kama ningemuoa si jamaa angenifahamu akaniua!?
Sitooa!!!acheni nile kwanza maisha kama wanawake wenyewe ndio hawa wasio kuwa na plan yoyote kuhusu future…..nitaendelea kuwa single mpaka pale nitakapopata mwenye akili inayo endana na harakati zangu…….
Fear women
