Baada ya hekaheka ya muda mrefu, hatimae sala zetu (pamoja na wana-JF) zimeleta mwanga. Jamaa yangu amepata msamaria wa kumsaidia na kwa uchunguzi wa awali - mambo ni mazuri.
Niliweka imani yangu JF na haikuniangusha.
Shukurani za kipekee ziwaendee wote walini-PM na kunipa faraja na maelekezo, na wengine wote waliochangia mawazo. Kwa umoja wetu, nasema: Mungu awaangazie njia nyoofu, milele.