Nilishiriki mapokezi ya ndege boeing 737 - MAX 9

Shirika la hizo ndege miaka nenda linazalisha hasara tu badala ya faida! Na hii ni kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za kila mwaka, kutoka ofisi ya CAG! Ila viongozi wako hata hawakomi! Wanaendelea tu kununua hizo ndege.

Hivi watakuwa wamerogwa au!! Maana kwa sisi tunaofanya biashara, hakuna kitu tunakiogopa kama kile cha kufanya biashara isiyo na faida!! Au ni kwa sababu hizo hela wanazo zichezea, hawazitolei jasho?
Miaka Nenda, Miaka Mingapi???
 
Unapambana sana!

Nataka nikupime kama una uwezo wa kuwa kiongozi katika Tanzania hii iliyopo kwenye dunia ya ushindani.


Nisaidie kwa mawazo yako. Unadhani Tanzania ijike kwenye maeneo gani na ifanye nini ili kuhakikisha inakuwa Nchi ya Uchumi wa Kati au Juu katika miaka 50 ijayo?
Dada mshushie nondo,hii jf kuna watu vichwa sana kwa hiyo tegemea kukutana na maswali
Konki

Ova
 
Serikali imepanga kupokea ndege nyingine ya Boeing 787-8 ya nini wakati moja tu kati ya sampuli hiyo ndio inayofanya kazi ya kwenda China na India?

Boeing 787-8 (5H-TCJ) imekwama Kuala Lumpur Malaysia tangu mwaka jana mwezi wa kumi.

Hizi ndege huenda sio mpya, zinakarabatiwa kuu kuu na kuziuza kwa mafisadi na kupambwa na sherehe za mapokezi kama mpya. Ndege mpya kabisa inatengenezwa kitu gani kwa miezi 8 wakati haikuwahi kuafanya kazi sana baada ya kupokelewa?
 
Kulala kwenye ndege ni adhabu kubwa sana kwenye vitu vya economy...nilisumbuka sana wakati tunatoka Guangzhou to Dar.
Kama wameviondoa kama ukivyosema basi kuna shida kubwa sana.
Kwenye hiyo ndege Business haina tofauti na economy
 
WACHENI TUTIWE MJINI
Tanzania ya Ujamaa haikomi kula hasara.
hakuna kinachowezekana kuwa cha Umma kikasimama Afrika.
Kama ATCL itapewa wakala wa kuiendesha na kurejesha faida serikalini utaona faida kede kede, lakini kwa kuendeshwwa na serikali yenyewe tutarajie majanga , mwisho ndege zitaibiwa vipuri na kuingiziwa vibovu.
 
Back
Top Bottom